Taarifa: waandamana kupinga ujio waBUSH


saa hapo facts zipo wapi?? hamna cha kweli hata kimoja!!! umeongea kaa mtu yeyote pro war and pro israel atakavyosema!!! THEY KNEW FROM DAY ONE KWAMBA SADDAM HAKUWA NA WMD's!!! unasemaje kuhusu "yellow cakes" from Niger??

sema something that, I don't know!!!
 

WEWE umekosa hoja hivi Hitler alipowaua mayahudi millioni sita ni muislam Hitler?
IRELAND kuna watu wa kikundi cha IRA wamelipua sana mabomu jee ni waislam?
wakatoliki walikamatwa na mabomu ya kupiga Westminster Parliament kwenye 1800s jee ni waislam soma historia. kifupi uislam hauhusiki na ugaini.muulize YVONNE RIDLEY uislam ni ugaidi?huyu ni mwandishi muingereza alikaa na hao wanaitwa Talaban na hatimaye akaingia uislam.

KICHUGUU.

wewe ulipochukua PHD ulifuata wapi utaratibu wa kuwa na PHD?

mambo mengi hata mfumo wa serikali yetu tumekopi kwa wageni.

walimu wako waliokufundisha walikopi kwa wazungu au wageni na kutuletea title kama PhD, wazee wetu hawakuwa nazo.

hivyo hivyo kama waislam wamechoma moto bendera za Bush ni kuonesha chuki dhidi yake sio tatizo.

umesema chuo kikuu kilijengwa na Waisrael sijakataa kama una kumbukumbu nzuri kuna wakati serikali yetu ilikataa kuwa na uhusiano na Waisrael na Africa ya kusini, kuonesha kukerwa na matumizi mabaya ya nguvu kwa raia wasio na hatia ilikuwa ukipewa pasiport unakatazwa kutembelea Israel.vipi wewe msomi unashangaa kuona watu wanaandamana?

jamani Wamarekani rafiki yao kivita ni Muingereza lakini raia wa UK na Marekani wameandamana na kulaani sisi hatutakiwi kuandamana kisa udini?
kwenye maandamano hayo yupo professor Mkristu wa UDSM alishiriki sababu ni open minded sio kama nyinyi.

kuchomwa moto kitambaa cha marekani ni sawa na maelfu ya watu wanaokufa IRAQ? unaweza kuwa unafurahi kuona wanaouliwa wa IRAQ ukidhani ni waislam ila ujue si kila muarabu ni muislam.

pia watu wa mashirika ya kimataifa wanakufa huko.vipi viwanja vyao vya ndege, mahosptial,vyuo vikuu n.k vinaharibiwa wewe msomi KICHUGUU unafurahia?

mbona walioleta dini hii ya ukristu hawana chuki mbaya kama ya KICHUGUU NA MWANKIJIJI?

Kichuguu waislam hawamchukii Bush kama mkrisitu na hawaandamani kwa dini yake NO.
mwaka juzi ulifanyika mkutano mkuu wa kuhusu USENGE kanisani, ulifanyika Tanzania nchi zote za duniani zilihudhuria hakuna muislam aliyeandamana kupinga utashi wa kanisa juu ya ushoga.

waislam waliheshimu uhuru wa kuabudu na kila mtu anaruhusiwa kuabudu anachotaka.

ningependa huu mjadala akauona BUSH atafurahi sana kuona anapata watu kama KICHUGUU NA MWANAKIJIJI wanao support wezi na uhalifu wake duniani.

Mwanakijiji kama Bush mwema hatukumuona kwenye mafuriko yaliokuwakuta wamarekani weusi huko NEW ORLEANS maarufu kama HURRICANE KATRINA.

PIA JIULIZENI BUSH hajawahi hata siku moja kushiriki kampeni ya kumnadi JOHN MCCAIN anayekiwakilisha chama chake. sawa na Mkapa asishiriki hata siku moja kampeni ya kumnadi Kikwete. na MCCAIN hajataja neno Bush kwenye kampeni yake yote.
 
intel mbovu ilikuwa inatoka Tel Aviv na kwa wale kina INC ya Chalabi!! Uranium from Niger ilikuwa intel ya kiyahudi, turned out to be a lie......unakumbuka ile screaming headline, "sexed up intell........." ilikuwa lini kwani??
 

Kwa hiyo unasema kuwa bush hana makosa kuivamia Iraq?
 
Hivi nyinyi mnana ajabu gani ikiwa waIslam wanaandamana kumpinga kichaka? Hamjuwi kuwa uIslam unafundisha kutenda mema na kukataza maovu? Naomba mtueleza, hivi nyinyi mnaona ni sawa kichaka alivyofanya Iraq? hivi mnaona sawa akiendelea kuwasaidia waisrael kuwauwa waPalestina? hivi mnaona sawa akiendelea kuuwa waAfghanistan bila sababu yoyote? hivi mnaona sawa anapowatisha wa Iran kwa kutaka kutengeneza nuclear energy? naomba majibu.
 
Kichuguu,
Kwa hiyo watu hao wanaunganisha wengine wote wanaokosoa kitendo cha wasilamu kuandamana kupinga ujio wa Bush kwa madai kuwa wote hao ni maadui wa uislamu. Hiyo siyo kweli na huenda inavuruiga kabisa thamani ya mjadala huu.

Ndugu yangu baada ya maneno hayo nilifikiria kuwa wewe mwenyewe hukuweka madai ya upande mmoja ambayo sisi tunayaona wrong kama vile unavyoona wewe.
Kinachovuruga mjadala huu ni neno moja tu WAISLAAM nje hapo tunadanganyana hapa. Mnachotazama hapa ni why Muslims...Kama maandamano hayo yangefanyika toka UDSM isingekuwa hoja kwa baadhi yenu isipokuwa sababu ni waislaam.
Na kwa mtazamo huu ndio maana baadhi yenu mliuliza kwa nini wasiandamane ktk maswala ya Richmond na mengineyo, still kidole kinawaashiria waislaam as if ni swala la waislaam tu kuandamana.
Having said that, kama nyie mnajitoa ktk maswala ya kuandamana ktk maswala ambayo sisi tunaona ni ukiukaji wa haki za binadamu inawapa shida gani haswa kama sisi tutaamua lipi la kufanya na pengine kati yenu wapo watakao ungana nasi.
Kumbuka hata harakati za Uhuru wetu mlisema haya haya na ni waislaam waliokuwa wakiandamana... lakini kwa baraka zake Mungu walikuwepo wakristu walioona sababu na nia ya kujiunga kama taifa moja na ku raise sauti yetu kwa pamoja.
Hukukatazwa ku join na hata kama kesho kutatokea maandamano yaliyotayarishwa na Mtikila kuhusu Majasusi ama swala lolote linalotukera sote nina hakika tutaungana naye bila kujali maandamano hayo yameanzia wapi ama kanisa gani.
Shukran zaidi ni pale uliposema mwenyewe kuwa mauaji ya Iraq ni kwa dini zote, waislaam na wakristu which make a very strong point kuwa WANAONEWA... haijalishi rangi wala dini ya mtu. Ukiambiwa a muslim country haina maana nchi hiyo hakuna dini nyinginezo...At a big picture Iraq leo hii wanapigana vita ya kidini na ni waislaam wanaoumia zaidi kutokana na policy za Marekani hasa chini ya Utawala wa Bush ambao umegawa tawala za majimbo ya nchi hiyo kulingana na madhehebu ya dini zao kuunda uadui kati yao...(devide and rule tactic)... Nafikiri unaelewa hilo.
Swala la Afghanstan, Ossama kisha ondoka yuko Pakistan why msimfuate huko kama mlivyofanya Afghanstan?... swala ni Ossama sio wananchi wa Afghanstan na waliolipua 9/11 ni wa Saudia, why Afghanstan wabebe mzigo wa watu wa nchi nyinginezo.
Hata baada ya Marekani kuingia hapo wamekuja gundua kuwa Ossama muda mwingi yupo milima ya mipakani na Pakistan on Pakistan side not Afghanstan... sasa adui amekuwa Taliban ambaye hahusiki kwa njia yeyote ile na 9/11. After all hawa ni matunda ya serikali ya Marekani yenyewe kama alivyokuwa Saadam why punish all people kwa makosa yenu wenyewe?...

Hii ndio sababu kubwa ya waislaam kupinga utumiaji wa nchi zao kueneza Politics ambazo malengo yake ni kuchukua tawala ya nchi kiuchumi. Wewe unashindwa kuiona hii kwa sababu either unaishi Marekani ama unaishi Tanzania ambako generation hii hawafahamu kabisa athari za Kutawaliwa...

Nadhani nimeandika mengi ya kutosha kukupa picha ya madai ya hawa waislaam ambao wewe huwaoni isipokuwa kwa rangi zao na ndio maana umesisitiza sana wapi maandano yameanzia na who is who badala ya issue yenyewe.
 
Tanzania tutazidi kuwa nyuma siku zote kwa kukumbatia misaada sasa 46 years ya uhuru- msaada utoke kwa Bush au Uarabuni!

It is a great shame to Tz! Huu umatonya ni aibu kubwa kwa nchi yenye raslimali nyingi kama TZ!

We should never be proud kwa kuwa tunapata msaada mkubwa! Ni aibu kubwa!
 
Wasomi UDSM wapinga ujio wa Rais Bush wa Marekani
Na Kizitto Noya

UMOJA wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), kwa kushirikiano na taasisi mbalimbali za kijamii na za Kutetea Haki za Binadamu, umepinga ziara ya Rais George Bush wa Marekani aliyewasili jana nchini.

Umoja huo ulieleza kutoridhika kwake na ziara ya rais huyo jana katika mdahalo wao ulioandaliwa kwa kushirikiana na wanaharakati hao kwenye Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.

Akisoma tamko la pamoja, Mwenyekiti wa UDASA, Datmas Nyaoro, alisema Umoja wa Wanataaluma chuoni hapo unaamini kuwa kidemokrasia Tanzania haina jambo lolote jema la kujifunza kutokana na kuwa rafiki wa karibu wa rais huyo wa Marekani.

"Hii inatokana na ukweli kwamba, chini ya utawala wa Rais Bush, haki za Wamarekani weusi zimeendelea kuvunjwa, idadi ya wafungwa kutoka katika jamii za Wamarekani weusi imeongezeka huku huduma za kijamii hasa afya na elimu zikidorora," alisema.

Kwa mujibu wa UDASA, Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutegemea ufadhili kutoka nchi zinazotoa misaada yenye masharti kandamizi kama Marekani, hivyo mkataba wa dola za Marekani 608 milioni unaotarajiwa kusainiwa kati ya Rais Bush na Tanzania akiwa nchini, hauna maana yoyote zaidi ya kuendeleza ukandamizaji huo.

"Tunaamini pia katika kujitegemea na kujitawala wenyewe. Kuongezeka kwa kiwango cha misaada kutoka Marekani katika kipindi hiki ambacho uchumi wake umedhoofika na upinzani dhidi ya ubabe wake umeongezeka, kunatufanya tuamini kwamba ufadhili huu una agenda ya siri ambayo ni Africom," aliendelea kusema Nyaoro.

UDASA ilitoa wito kwa Watanzania kulinda misingi ya uhuru na utaifa, kulinda na kutetea utu, haki, usawa, amani na umoja wa Afrika badala ya kuendelea kuikumbatia Marekani na kupoteza misingi iliyojengwa tangu enzi za mababu.

Awali wakizungumza katika mdahalo huo, baadhi ya wanaharakati na wawakilishi wa taasisi za kijamii walisema kuwa ziara ya Rais Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania isipokuwa kwake binafsi na taifa lake la Marekani.

Kwa upande wake, Amiri wa Shura ya Maimam, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema ziara ya Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania zaidi ya taifa kujitengenezea maadui kwa kuunga mkono sera ya ugaidi.

Alisema sheria ya ugaidi nchini inapaswa kuangaliwa upya kwani inapingana na sheria za nchi na ndiyo inayosababisha mapigano katika mataifa mengi duniani.

Hussein Mmasi wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema Bush hana utaratibu wa kufanya ziara zenye manufaa kwa nchi wenyeji na kuwa ziara hii ni mwendelezo wa utaratibu huo wenye misingi ya kuzinyonya nchi maskini.

Profesa Azaveli Lwaitama, Mhadhiri wa UDSM, aliitaka serikali kuchagua marafiki wa kweli wanaoweza kutoa ushauri wa haki kuhusu maendeleo yake badala ya marafiki wanafiki kama taifa la Marekani.

Alisema Rais Bush amekuja nchini kwa kivuli cha misaada, lakini ukweli ni kwamba ana agenda kubwa yenye masilahi binafsi na taifa lake.

Ndani ya ukumbi kulikofanyika mdahalo huo kulikuwa na mabango kadhaa yaliyoelezea hisia za wanaharakati hao juu ya ziara ya kiongozi huyo wa taifa kubwa duniani.

Baadhi ya mabango hayo yalisomeka 'Mfumo tulionao wa demokrasia wakilishi haufai, tunadai demokrasia shirikishi... Bush sitisha vita Iraq, Amani na Haki siyo vita'.

source:http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4529
 
Mtalii, Zomba na Mkandara.

Someni ile post yangu kwa makini tena. Vile vile ningeshauri mtalii awe mstaarabu kwa kusikiliza upande wa pili baadala ya kukurupuka na kuweka labels za ajabu kwa watu asiokubaliana nao.

Mkandara, hiyo paragraph uliyokopi, ina fact nilikuwa nina maana ya Mtaliii alipodai kuwa mimi ni kardinali.

Mimi sikusema kuwa ni vibaya kufanya maandamano; in fact nilishaandika kuwa maandamao hufanyika sehemu zote duniani anakoenda Bush, kwa hiyo hata kwetu Tanzania nilitegemea kuwepo maandamano au upinzani wa aina fulani. Nilichokosoa ni utaratibu mzima na ujumbe uliotumwa na maandamano yale ya waislamu. Maandamano hayo yalikuwa ni ya waislamu tu, yameanzia msikitini na ujumbe wake ni kuwa Bush aache kuwaonea waislamu. Wangekuwa na ujumbe kama Bush aache siasa za ubabe kunyanyasa nchi ndogo kusingekuwa na tatizo, ila kitendo cha ku-single out kuwa Bush ananyayasa wasilamu tu ilikuwa ni makosa. Kwa vile maandamano hayo yametokea masikitini, sijui nimalizie vipi ili muone kuwa njia ile haikuwa sahihi na imepunguza kabisa uzito wa ujumbe wenyewe. Kufanya jambo kwa ajili "kutetea waislamu" tu ni message ambayo imekuwa inatumiwa na wapiga propaganda za kiislamu siku zote kwa ajili ya faida zao binafsi. Mabango yale yalindikwa kabisa kuhusu waislamu: "Uhuru kwa Iraq, Palestine, Lebanon na waislamu wote"

Maandamano ya waislamu yalikuwa na malengo tofauti kabisa na yale ya UDASA, ambayo yalilenga dhidi ya sera za Marekani kwa jumla, siyo kwa ajili ya kundi moja tu katika jamii.

Zomba,

Hivi kweli umesoma sentensi hata moja ambapo nimeandika kuwa kuvamia Iraq ilikuwa ni sahihi? Mimi nimeuliza ushahidi unaoonyesha kuwa kuivamia Iraq kulikuwa na lengo la kuwanyanyasa waislamu tu. Nimesema kuwa walioathirika na vita Ira ni wairaq wote bila kujali dini zao. Watu wote wanoandamana dhidi ya vita ile wanaangalia atahri zake kwa maisha ya watu hawesemi kuwa kuna dini fulani imefaid na nyingine kuonewa. Ukiangalia mgawanayo wa dini utagundua kuwa uvamizi ule umewapa waislamu power zaidi ya wakati wa Saddam ambapo baadhi ya mawaziri waandamizi walikuwa wakristo, na kwa sasa hivi hakuna mkristo hata mmoja.


Mtalii,

Kuiga mambo ni vizuri lakini tuwe waangalifu kujua tunaiga nini na kwa sababu gani; tusiwe bendera fuata upepo tu.


Mkandara,

Ukizungumza ubaya wa sera za Marekani kwa nchi ndogo nitakuelewa. Tunapotofautiana ni pale unapoelekea kuunga mkono kuwa sera hizo ni za kukandamiza waislamu tu. Kumbuka kuwa wakati wa Saddam, Iraq haikuwa nchi ya kiislamu ingawa raia wake wengi walikuwa waislamu. Kwa hiyo uvamizi wa Iraq haukuwa umeilenga kama nchi ya kiislamu; Bush alikuwa na usongo wake binafsi dhidi ya Saddam na mafuta yake wala hakuwa na sababu ya dini yake. Vile vile kumbuka kuwa Marekani waliitetea Kuwait mwaka ule dhidi ya Saddam siyo kwa sababu Kuwait walikuwa wakristo.

Kukubali kuwa marekani ndio waliwatengeza Al-Qaeda kwa kuwasaidia Mujahedeen dhidi ya Urusi ni ushaidi tosha kabisa kuwa lengo lao halijali dini bali wanaangalia zaidi maslahi yao. Taliban na Al-qaeda walikuwa against interests za Marekani. Hata kama Osama angekuwa Christian Evangelical (dini ya Bush,) angefuatwa vile vile.
 


This is the point. Hili ndilo jambo ambalo nilitegemea waandamanaji wetu wawakumbushe viongozi wetu.
 
mmhhhh, interesting, but nadhani nilikwambia kua mi niko fair na nikasema kuwa intel can purposly be created to mislead others.kwenye ulimwengu wa sasa hiyo pia ni effective strategy, na inaweza kutumika kuogopesha au inaweza kutumika kuficha madhambi, na ndo mana mfano siku za uhuru kwenye baadhi ya nchi ndio siku ya kuonyesha military powers zao ili adui aogope au ajiulize mara mbilimbili kama alikua na lengo la kuvamia, kwa hiyo hii inadhihirisha kuna nchi hupenda kuogopesha nyingine.tumeona watu wakipitisha long range ballistic missiles, vifaru vya ajabu,makomandoo wakipita kwa mbwembwe, ndege n.k.sasa basi, powell aliposema satellites zimeona wanachosema waliona na walikamata mawasiliano kati ya wairaq na watu wa niger, sisi tusio ndani ya hizi nyumba mbili(nadhani niseme mimi sijui we mwenzangu), hatuwezi jua who is right here! to be fair, inawezekana marekani walipika story lakini pia inawezekana waliona na kuskia walichosema.afu unaposema intel ilitoka tel-aviv, una fact na hili swala? au umesoma article ya mwandishi mmoja? kuhusu kusema kwamba walijua saddam from day one hakuwa na WMD's, hizi facts zako zinatoka wapi? tunavyoelewa waliingia vitani kutokana na poor intel wakiamini kua jamaa alikua na WMD's, afu unajua kwamba vita kwa mataifa makubwa watu hawakai tu wakaamka na kusema twaingia vitani, every variable in the economy is counterchecked to see how it can be effected by the war, going to war its risky bwana na kwa jinsi nnavyojua isingekua rahisi kwa marekani kutumia billions for something which was not a threat to them.naomba nikukumbushe am not saying they were right what am saying, waliamini in wrong intel.
 

nothing new! wrong intel is wrong intel, period..sasa wewe unadhani ni sahihi ku-cook intel? kama yes, basi ndio hapo mimi na wewe tupo tofauti! kumbuka story za "baghdad bob" au Rummy..kuna known knowns, kuna known unknowns, kuna unknown knowns na unknown unknowns! sasa wewe upo wapi hapo? haya sio mambo ya ushabiki mkuu, hatuishi kwenye karne ya 12! FACTS MATTERS, na sio justifications za kipuuzi!! picha ya soldier asie jicho ina ku-define!! LOL.
 
mmhhh, interesting! tufanye umeshinda mtu mzima mwenzangu!i like your arguments!!!especially about the knowns and the unknowns!!
 
Chuma,

Wewe ndio mmoja wa fanatics anaowaongelea IO kwenye posting yake, maana wengi wenu wanaopenda peace wanasema:

Na Said Mwishehe

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema ziara ya Rais George
Bush wa Marekani ina faida kubwa kwa Watanzania wote, hivyo limeiunga
mkono, huku taasisi zingine za Kiislamu zikisisitiza kuwa Waislamu
wachache wanaopinga ujio huo, hawana hoja za msingi.

Shekhe Mkuu Shaaban Issa Simba, aliwaambia waandishi wa habari Dar es
Salaam jana, kuwa Rais Bush anakuja kwa mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete,
hivyo Watanzania wote wakiwamo Waislamu, wanapaswa kuunga mkono ujio huo.

"Tunaamini Rais Kikwete amemwalika Rais Bush kwa sababu za msingi,
kutokana na ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili na hata ukiangalia
Marekani imekuwa ikiisaidia zaidi Tanzania katika mambo mengi yakiwamo ya
miradi ya malaria na UKIMWI," alisema Shekhe Simba.

Alisema mbali ya kusaidia katika miradi, ziara ya Rais Bush ni ya
kiserikali na hakuna sababu ya kupingwa bali wananchi wanatakiwa kuungana
na kumpokea kwa mikono miwili.

Alisisitiza kuwa Waislamu wachache wanaopinga ujio huo kwa kutaka
kuandamana, wanapaswa kumpokea kwanza, baadaye waoneshe hisia zao kama
zipo, lakini kumpokea kwa mabango hakutasaidia.

"Kinachoonekana hapa ni kwamba baadhi ya watu wanaingiza siasa za
kimataifa katika ujio wa Rais Bush, lakini wanapaswa kufahamu kuwa masuala
ya kimataifa yana taratibu zake za kushughulikia, kwani Bush anakuja kwa
ajili ya Tanzania na si kwa ajili ya siasa za kimataifa," alisisitiza
Shekhe Simba.

Naye Katibu wa Kamati ya Maimamu ya Kuokoa Mali za Waislamu Tanzania,
Shekhe Khalifa Khamis, alisema Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, imetumia
sababu zisizokuwa na msingi kupinga ujio wa Rais Bush wakidai kuwa ziara
yake ni kwa ajili ya kuweka kituo cha kijeshi nchini jambo ambalo si
kweli.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa taasisi hizo zinapaswa kufahamu kuwa Rais
Bush ambaye sera zake hazifai, amekwishafanya ziara katika nchi za
Kiislamu hadi Saudi Arabia na kupokewa na Mfalme Abdallah ambaye ni
mdhamini mkuu wa misikiti mitakatifu ya Makka na Madina na kuvishwa joho.

"Mbona Waislamu wa Saudi Arabia hawajaandamana Bush alipokuwa huko? Au
sisi ndio Waislamu sana?" alihoji Shekhe Khalifa.

Alisisitiza kuwa kikundi hicho ambacho kimepanga kufanya maandamano ndicho
hufunga na kufungua Ramadhani kwa kufuata matangazo ya Saudi Arabia na
ndiko aliko kiongozi wao, inakuwaje wanashindwa kuiga mfano wa Saudia
ambayo ni nchi ya Kiislamu na Rais Bush ameshaitembelea kabla ya kuja
nchini.

"Wanaopanga kuandamana nadhani hawana hoja ya msingi, kwani jumuiya na
taasisi hizo zimetufedhehesha sana Waislamu wa Tanzania, kwa kutetea
mahabusu wa Guantanamo, ambao wanashikiliwa kwa kuhusishwa na ulipuaji wa
majengo mawili ya Kituo cha Kimataifa cha Biashara Marekani na kuua maelfu
ya watu wasiokuwa na hatia wakiwemo Waislamu," alisema.

Alisema wakati umefika kwa Waislamu kukataa kutumiwa na watu wachache kwa
maslahi binafsi na kusisitiza kuwa kikundi hicho kiliwahi kuandaa
maandamano ya kumuunga mkono Rais wa zamani wa Iraki, marehemu Saddam
Hussein na Osama bin Laden na mwisho wa maandamano, wakawataka Waislamu
wachange fedha ili wapeleke msaada, lakini fedha hizo hazikufika.

Kwa upande wa uongozi wa Taasisi ya Taibah Haj Umra and Social Services
Trust, umesema ujio wa Rais Bush una manufaa kwa Watanzania na hasa
ukizingatia kuwa Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, hivyo kuja
kwa Rais Bush kutatoa nafasi ya kujadiliwa kwa matatizo mbalimbali ya Bara
la Afrika.

Taibah ilisema kitendo cha kupinga ujio wa Rais Bush kitamtia aibu na
kumfedhehesha Rais Kikwete, ambaye ndiye mwenyeji wake na katika utamaduni
wa Afrika, mgeni hupokewa kwa shangwe na anapokuta kuna mabadiliko
huondoka na picha mbaya.

Uongozi huo ulisisitiza kuwa Waislamu wanaopinga ujio wa Rais Bush
wanapaswa kufahamu, kwamba kabla ya kuja nchini, tayari ameshafanya ziara
katika nchi nyingi za kiislamu, lakini Waislamu wa nchi hizo hawajafanya
maandamano. Kwa mantiki hiyo, imewataka Waislamu waliopanga kufanya
maandamano kuacha mkakati huo.
 
Mkandara:
1. Kwa Nini Marekani ilishambulia Afghanistan?
Kwa sababu tu Mullar Omar alimficha Osama ambaye anasadikiwa kufanya ughaidi dhidi ya interest za marekani East Africa na Kubomoa trade Centre. Kumbuka aliyeanza kurusha zile misiles alikuwa Clinton. Clinton alibomoa kiwanda cha madawa Sudan, na kuharibu key areas ambazo zinatrain magaidi Afghanstan. Bush alimuomba sana Mullar Omar kuwa amkabidhi Osama, lakini omar alikataa kata kata. Alipewa muda hata ulipofikia muda huo umoja wa mataifa na SIYO Bush uliamlisha jesh la NATO kufanya kazi yake. Matokeo sasa Bush anabeba msalaba.

2.Kwa nini Marekani alitaka kumwondoa Sadam
Sadam, kwa wana Siasa wengi duniani husema, mdomo wake ulimponza! Makosa makubwa ya Sadam ilikuwa ni kuvamia Kuwait. Na hata baada ya kuvamia Kuwait sadamu aliendelea kuongea kama kweli na yeye ni a Super Power; amewahi kusema mara nyingi kuwa angeweza kuigamiza Marekani na hata Israel. Mtaifa yalioyoogopa Iraq ni pamoja na Iran yenyewe, Saudi, Israel, Kuwait, UAE nk.
Kosa la pili lilommaliza, baada ya Umoja wa Mataifa, mara mbili kwenda kutafuta uhakika wa Silaha Hatari (WMD= Weapons Of Mass Destruction)Sadam alitia mkwara, kuonyesha umwamba. Ilifikia kuwa ingawa CIA haijapata crues kuhusu ukweli wa nguvu za Sadam, lakini maneno yake yalikuwa mazito. Hata kama ukikumbuka, Baraza la umoja wa mataifa lilimwoba sana Sadam akubali, lakini yeye alikataa. Baada ya grace period aliyopewa, alidhani Mataifa kama Russia, china watamkomboa.

3. American Foreign Policy:
The bad thing is; September 11, happened during Mr. Bush's presidency; think, if Obama was a president at that time what he could do? America has its own foreign policy; and all the presidents must follow it; otherwise will never rein! tunamchukia Bush, si Kweli inabidi tuichukie America!
 
Hapa wengi we are bitting around the bush kwa kuogopa kuwa branded, wadini, bigots, fanatics etc....But ukweli ni huu na lazima tuuseme:

Bush is not against Islam, he is interested in American interests..so if it happens that those interests will rub with Islam, Christianity, Buddhism... so be it. He will persue them.

I have tried to observe this, lakini kitu ambacho kiko open BAADHI ya waislamu wakisha pata nafasi wanapenda sana kuimpose values zao kwa wengine! Which is totally unacceptable! To me my freedom is alpha and omega. Kuniambia nivae nini, nile nini...its non of your business. We have seen it Northern Nigeria, Sudan, Niger, Egypt nk ambako waislamu wamelazimisha kwamba Sharia itumike (kisa? wao ni majority na wakristo/animist ni wachache..harafu wanasema eti wataheshimu haki za wengine wasio waislamu!-very unrealistic) Hivi vitu ndo vinawafanya wengi wanakuwa very sceptical na haya mambo ya dini! Mtu unaambiwa uvae nini, nguo yenye urefu gani! This is unfair...Ndo maana migogoro haishi, kwa sababu watu wanataka kujikomboa katika chains kama hizi! Huwezi ukaamrisha kila mtu asome Qurani au Bible! Its absolutely unfair!

Mfano: Ukienda Khartoum, kununua au kunywa pombe ni crime! na Khartoum is a cospmopolitan city ya waislamu na wakristo! sasa jiulize...hiii mambo gani haya? KUNA SOUTHERNERS KIBAO...sasa jiulize wanalazimishwa ku-give up haki zao za msingi..kisa dini... Jamani tukubali ndugu zetu waislamu lazima wawe all inclusive, usipokubaliana nao..wewe ni Kafir au religious bigots!

Personally I drink! I once worked in Khartoum in late 90s...huko hata diplomats wanaingiza pombe kwa kujificha! Darasani Bashiri alipiga marufuku kutumia kiingereza! watu wanasoma kwa Kiarabu..we have seen people protesting, kwa sababu hawana namna! Kifupi uhuru wa watu unakuwa muzzled na hawa watawala na wale wanaojifanya kwamba wanayajua maadili mema kwa kila mtu, the likes of Turabi and co..Yaani wewe usipokuwa Muislamu katika hizi nchi..Honestly you will have hard time! Tanzania is a paradise I can tell you...hawa wachache wanaoleta/wanaotaka kuleta udini..wakemewe mno...Tutafika point, tutaanza kudemand kwamba kwenye baraza la mawaziri..tuwe na wakristu wangapi, waislamu wangapi..etcs..once ukishajiona wewe unaonewa..you will forever be so! Hata utendewe nini!

Sasa basi kwa Tanzania..mi namshukuru Mwalimu sana, kwamba Islam and Christianity/African Tradition Religions can co-exist. But hii mambo ya kuleta sijui kujiunga na OIC, sijui Vatican... sijui nini..I think tuachane nayo....Kifupi tusiingize dini katika maisha na mahusiano yetu kama taifa. We have our common enemy which is UFISADI, UMASKINI, MARADHI ambayo hayachagui dini! Lets confront them together. Dini kila mtu ajijue na Mungu wake! what is necessarily good virtues au maadili kwako..does not necessarily be so to me!! So why IMPOSE YOUR VALUES ON ME? AU WHY SHOULD I IMPOSE MINE ON YOU?

Ingawa Zomba kasema eti Islam maana yake ni way of life! Kwa kweli to me..anything which is likely to interfere with my freedom, I will fight it to the last drop! Hivi jiulize bongo tungekuwa na sharia, kungekalika kweli? eti siruhusiwi kula bia yangu pale Rose Gargen, eti dada yangu haruhusiwi ku-cross street akiwa mwenyewe, ati harusiwi kuonekana na mwanaume in public ambaye siyo mume wake......kisa eti kuran hairuhusu....yaaaah!!!No way waacheni watu wapractice maisha yao...

Iwe bible, iwe quran, Lazima iheshimu haki za watu!
 
Eti watu wanaandamana .....walikuwa wanapinga nini?

zile 700m USD,au joji mtembezi kichaka kuja bongo au marekani na sera zake za nje au marekani na sera zake za ndani au nini hasa...

maana naona wamechoma hadi bendera ya marekani ...

kazi kweli kweli....
 
masanja,
makelele mengi umepiga hapo juu, kiasi ukanichanganya ni chepi hasa ilikuwa lengo lako! "kapriensi" yako Sudan isiwe justification ya jazba ulonazo.
maswali ya kujiuliza, walioandamana ni takribani watu 2000, je Tanzania ina waislamu wangapi? supposedly walioandamana wote ni waislamu, je number hiyo ni asilimia ngapi ya waislamu wote wa TZ? hayo mambo ya sharia ulozungumzia kijumlajumla umesikia waislamu wangapi wa TZ wanaunga mkono? umeshawahi kusikia waislamu wa TZ wana-demand mabaa yafungwe wakati wa mwezi wa ramadhani?
uislamu ni dini moja, lakini upo shaped sana na mazingira na culture ya nchi husika! umetoa mfano wa northern nigeria, ukweli ni kwamba udini ule una ukabila ndani yake(u-hausa), hivyo basi dini ni kama fimbo tu ya kupush agenda zao fisadi.
hivi nini kiliwapata waislamu wa southern uropa hasa spain ktk medieval time? kosovo n.k....
hivi labda nikuulize tena umetembelea nchi ngapi zenye waislamu wengi?mfano indonesia ndio nchi yenye waislamu wengi kabisa hapa duniani, je sheria zao zipo influenced na uislamu? kupiga tungi ni marufuku?..jibu, I bet ni no!! narudi kule juu kwamba uislamu unakwenda na mazingira, scenarios zote ulotoa hazina nafasi Tz na wewe mwenyewe unalijua hilo!
hata hapa US kuna wakristo siasa kali, kuna "dry areas" kibao..dry areas hawaruhusu kinywaji. Kuna counties flani flani in northern Arkansas just across the border from Missouri, ukishikwa na kinywaji umekwisha. sheria hiyo ipo influenced na the likes of mike huckbees. Je wajua kwamba hao siasa kali wakristo wanataka kuangusha roe v/s wade hapa US?je waislamu wangapi bongo umesikia wame-bomb arbotion clinic au kumtwanga risasi doctor mtoa mimba?
kwanini unapenda sana ku-generalize mambo ndugu yangu? watu 2000 hawawezi kutumika kukandamiza na ku-stereotype watu wengine zaidi ya mil 18!..hao siasa kali unaongelea wewe hawafiki hata 5 per ya waislamu wote duniani!
jaribu ku-research uone ni kina nani na kwanini wanafanya wafanyavyo na sio kukandamiza dini nzima.
siku nikidondoka bongo nitakutafuta tukapige tungiz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…