maneno yako ya kejeli hayafanyi hojayako iwe na nguvu.
a. Ulimwengu anaweza kusema lolote analotaka kusema lakini hoja hupimwa kwa nguvu zake. Yaani kweli wewe unaamini kuwa Bush anakuja kwa ajili ya "Ughaidi"? Kama unaamini hilo unaweza kujikuta bado unaamini kuwa kuna mama na mwanae mgongoni kwenye mwezi!.
b. Hivi nchi ambazo si za kighaidi kama Iran, Saudia na UAE wametusaidia kwa kiasi gani kupambana na Ukimwi, Malaria, ujenzi wa barabara n.k ? Jamani tujenge hoja, ni nchi gani inatoa misaada mingi kwa Tanzania? NIna uhakika Marekani haiko mbali.
Hivi kweli watu wanataka Marekani isaidie tu bila kupata chochote? MBona nchi nyingi hatutumii kipimo hicho hicho au kwa vile hatutaki wanachotaka kupata? Hivi Iran kwanini inajaribu sana kuwa karibu na Tanzania?
c. Tatizo siyo kuandamana wanaweza wakaandamana mchana kutwa na usiku kucha wakipenda! Hoja ni kuwa vile vitu vya kitaifa waviweke mbele; wasimame kuwatetea wananchi wenzao na kusimamia masuala ya Taifa. Siyo pale tu yanapogusa Waislamu ndio watu wanakimbilia kuandamana. Hivi mkataba wa Richmond ungeuza kiwanja kimoja cha Waislamu unafikiri kina Issa Ponda wangekaa kimya?