Taarifa ya ajali: Mwana JF mwenzetu Ushimen kapata ajali mbaya na sasa yuko Muhimbili hospital

Taarifa ya ajali: Mwana JF mwenzetu Ushimen kapata ajali mbaya na sasa yuko Muhimbili hospital

Na hii ndio taarifa yake

Habari ya asubuhi wana familia.

Sisi tunaumwa, nilipata ajali mbaya tarehe 5 October na ilionekana nimepata fracture kwenye mguu, siku tatu mbela ikaonekana nimepata clavicle dissociate (mfupa wa bega ulipishana.

Na nilimuona bingwa wa mifupa tukapata matibabu (arm sling na figger of 8).

Niliendelea kupata nafuu hadi tarehe 24 ghafla nilianza kupata maumivu mapya upande wa kulia kama kichomi kikali, tulipata rufaa na sasa tupo muhimbili Sewahaji 17 room 12.

Nimetobolewa pafu baada ya kugundilika lili pata kuvia dam na uzembe ulifanyika kwa kutokugundua tatizo hilo na nikakaa na shida hiyo kwa wiki 3.

Kwakifupi hatuendelei vizuri sana lakini nashkuru Mungu naendelea kutoa damu kwenye pafu na sasa nikama inatoa usaha.

Leo kuna vipimo tutafanya pamoja na kukaa na wataalam, kama ikiwa bora zaidi tunaweza sogea kwa nchi yenye wataalamu zaidi ili tupate kupona.

Naomba mtuweke kwenye maombi n Mungu atawabariki sana.

NB: Kwenye ajali hiyo mbaya iliyohusisha madereva wawili pamoja na Ushimen! Dereva wa kwanza ambaye ndie alisababisha ajali hiyo mbaya alikufa pale pale.. Dereva wa pili aliyekuwa na Ushimen alifariki siku tatu baadae

Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuepusha ndugu yetu na kifo.. Tumuombee nafuu ya mapema
Aiseeeeeee!!!
 
Classmate Ushimen It is well...

Zaburi 20:1-4
[1]BWANA akujibu siku ya dhiki,
Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

[2]Akupelekee msaada toka patakatifu pake,
Na kukutegemeza toka Sayuni.

[3]Azikumbuke sadaka zako zote,
Na kuzitakabali dhabihu zako.

[4]Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako,
Na kuyatimiza mashauri yako yote.

Zaburi 103:3-5
[3]Akusamehe maovu yako yote,
Akuponya magonjwa yako yote,

[4]Aukomboa uhai wako na kaburi,
Akutia taji ya fadhili na rehema,

[5]Aushibisha mema uzee wako,
Ujana wako ukarejezwa kama tai;
 
Back
Top Bottom