Taarifa ya Al Jazeera kuhusu mauaji kule Jazira imetangazwa faster kuliko kawaida

Taarifa ya Al Jazeera kuhusu mauaji kule Jazira imetangazwa faster kuliko kawaida

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
9,616
Reaction score
22,521
Al Jazeera wametangaza hii habari haraka haraka sana hakuna coverage hata ya kuhoji watu ambao wanasema Ile ni massacre.

African news nao Wala hawatangazi kuhusu Sudani.

Taarifa yote iko Gaza Ina cover Kila sekunde hadi mistari ya kuchukua chakula milio ya ndege n.k

Africa is for Africans huko kwingine hapatuhusu tupige kelele amani ya Sudani ni muhimu ningetegemea watu kama Kipa wa Azam awe hata na banner inayotaka "peace for Sudani"lakini unaweza Kuta nae anataka amani ya Palestine.
 
Hivi waarabu wa Sudan hawawataki watu weusi wa huko
Siyo...

Ova
Yah refer kauli ya Mseveni akiwa msuluhishi wa mgogoro wao wale wasudani wenye nywele laini kama wale waliokuja Muhimbili hawataki kabisa kuchangamana na wale kina John Garang
Japo mgogoro wa Sasa ni WA wao wenyewe
Ni kama alivyosema Nyerere Leo ukiwabagua watanganyika kesho utawabagua wapemba au waunguja
 
Alafu kwanini yanayotokea huko Sudan wapiga kelele huku,wanapigaga kimya

Ova
Hili ndio swali kwa wengi kwanini vyombo vya habari havitoi uzito kwa mgogoro wa Sudan kama vile wanavyotoa kwa Ukraine na Palestine!?
Imefikia hatua na waafrika wenyewe hawaoni mgogoro wa Sudani nao wanabeba mabango ya Palestine,Un inaongelea Palestine na Ukraine hata ICJ nayo inaongelea huko huko huku afrika ikifumbiwa macho
 
Dar nlikuwa napishana na liprado
Limoja linabendera la Palestine
Gari imeandikwa free 🇵🇸

Ova
Hilo li Prado limeona shida kuweka Pray for Sudan nchi ambayo kwa Sasa imesimama kabisa hakuna michezo hakuna elimu hakuna maji hakuna umeme Kila kitu kimeganda
 
Hata Afrika nzima imekaa kimya, kazi kushadadia mambo ya race zingine.
Niliangalia interview ya Ruto Jana Al Jazeera Kila akijitahidi kuongelea Sudan mtangazaji anampeleka Palestine hadi jamaa akawa kama haelewi mtangazi anajiliza pale kwa kutana women and children Ruto anahamia Sudan
Ni kama international media hazitaki kabisa ya Sudan yajulikane
 
Hili ndio swali kwa wengi kwanini vyombo vya habari havitoi uzito kwa mgogoro wa Sudan kama vile wanavyotoa kwa Ukraine na Palestine!?
Imefikia hatua na waafrika wenyewe hawaoni mgogoro wa Sudani nao wanabeba mabango ya Palestine,Un inaongelea Palestine na Ukraine hata ICJ nayo inaongelea huko huko huku afrika ikifumbiwa macho
Mahawara zao hawajasema chochote. Wanasubiri bwana zao wakiongea, hawa waafrika wapuuzi wafuate upepo wa mwenye mbwa.

Shame on us African
 
Back
Top Bottom