Taarifa ya awali kuhusu hukumu ya Mahakama Kuu masjala kuu Dar es Salaam, kuhusu Wanachama 19 waliofukuzwa CHADEMA

Taarifa ya awali kuhusu hukumu ya Mahakama Kuu masjala kuu Dar es Salaam, kuhusu Wanachama 19 waliofukuzwa CHADEMA

Hii taarifa ya kukurupuka sana haieleweki. TUIPUUZE. Sultani Mbowe ingependeza kama angeachia ngazi kwa sababu ni aibu kwa chama kilichojaa wanasheria kugaragazwa mahakamani na kina mama shupavu 19. Mtake msitake kina Halima na wenzake ni wanachama halali wa CHADEMA. Hamuwezi kuwafukuza kihuni.
Shida ni ccm kujaza wasimbe sugu ambao akili hawana kazi kupiga kelele tu
 
Hii taarifa ya kukurupuka sana haieleweki. TUIPUUZE. Sultani Mbowe ingependeza kama angeachia ngazi kwa sababu ni aibu kwa chama kilichojaa wanasheria kugaragazwa mahakamani na kina mama shupavu 19. Mtake msitake kina Halima na wenzake ni wanachama halali wa CHADEMA. Hamuwezi kuwafukuza kihuni.

Wewe ndio shabiki. Nani kagaragazwa?. Akina Halima Mdee sio wanachama wa CHADEMA mpaka muda huu kwani maamuzi ya kamati kuu hayajabatilishwa. Ila imetoa muongozo kwamba Baraza kuu like Tena bila kuhusisha wale viongozi wa kamati kuu. Sasa hapo nani kashinda?
 
Busara itawale CHADEMA,kaeni na wabunge wenu muombane msamaha mambo yaendeleee acha kufukuzana,jifunze Kwa CCM

Msamaha anaomba nani?. Hapo ni CHADEMA kuitisha mkutano wa baraza kuu.
 
Ingekuwa busara kama CHADEMA mngejikita kwenye kuandaa uchaguzi mkuu ndani ya chama.
 
Mhe halima mdee hatimaye kampiga mkoloni mboweeh🤣🤣🤣

Kumbe mdee alifungua kesi dhidi ya Mbowe?. Halafu umesoma hukumu? Akina Halima Mdee sio wanachama wa CHADEMA, kilichoangaliwa ni rufaa yao baraza kuu. Hivyo CHADEMA inabidi isikilize ruffaa yao upya.
 
Muda wa bunge umekwisha, hii yote ilikua ni danadana kupoteza wakati.
 
Wewe ndio shabiki. Nani kagaragazwa?. Akina Halima Mdee sio wanachama wa CHADEMA mpaka muda huu kwani maamuzi ya kamati kuu hayajabatilishwa. Ila imetoa muongozo kwamba Baraza kuu like Tena bila kuhusisha wale viongozi wa kamati kuu. Sasa hapo nani kashinda?
Kwa hiyo baraza kuu lililowavua uanachama lilifanya maamuzi ya kipuuzi hadi mahakama imeamua mrudie tena? CHADEMA ina wanasheria wanaojitambua kweli?
 
Majinga chadema yamegaragazwa

Ruzuku inayotokana na kina Mdee wanaendelea kuchukua toka DJ alambe asali
Wjng kabisa,Acha sisi tuendele gawa
Rasilimali za nchi ,sisi ndiyo tuna akili
Chadema hamna kitu

Ova
 
Mbowe alifikiri chama ni cha mkwewe, akaona anaweza kuwaburuza watu apendavyo
Huyu dikteta idd amini mbowe amekomeshwa
Pambana na Hali yako,hasira za nini Kwa mambo yasiokuhusu mwafrika ni laana
 
Pambana na Hali yako,hasira za nini Kwa mambo yasiokuhusu mwafrika ni laana
Binafsi mimi si mwnachama cha siasa cho chote lakini hii taarifa ya Chadema ni mfano mzuri wa utawala bora wa kutoa tamko haraka badala ya kuacha wanachama wake kupiga ramli. Nawapeni hongera. Kuna kiongozi mmoja aliwahi kusema Chadema ina human resource ya kutosha naanza kuamini sasa.
 
Tumepokea hukumu iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2023, uamuzi wa Mheshimiwa Jaji Cyprian Phocas Mkeha;

1. Kwamba uamuzi wa kuwafukuza uanachama waliokuwa wanachama wetu 19 uliofanywa na Kamati Kuu ya Chama, umeendelea kusimama (Upo pale pale) na Mahakama imekubaliana kuwa taratibu zote za Katiba ya Chadema na Sheria za nchi zilifuatwa kikamilifu na Kamati Kuu katika kuchukua uamuzi huo.

2. Kwamba, maamuzi ya Baraza Kuu kuhusu Rufaa yamefutwa na hivyo Baraza Kuu linapaswa kukaa upya kusikiliza Rufaa; lakini Kamati Kuu ilishawafukuza Uanachama na uamuzi wake Judge kasema wazi upo sahihi.

Hivyo basi, kwa hatua ya sasa Chama kitawasiliana na Mawakili wake ili kutafakari hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kumkumbusha Spika wa Bunge kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa Kamati kuu ya Chama wa tarehe 27 Novemba, 2020 kwani Mahakama imethibitisha kuwa walishafukuzwa uanachama kihalali na taratibu zote zilifuatwa .

Tunawataka wanachama wetu watulie wakati huu chama kinapotafakari hatua za ziada.

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2023.

John Mrema
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya nje.View attachment 2842642
View attachment 2842645
Kama nilivyojieleza mwanzoni mimi si mwanachama wa chama cho chote cha siasa ila ni raia Mtanzania. Napenda kuwauliza wenzetu mliosoma constitutional law na nadharia ya sheria mnaweza kuorodhesha masuala katika jamii ambayo ni ultra vires kwa mahakama kujihusisha? Kwa mfano, Kamati Kuu ya CCM inapopendekeza majina matatu ya wagombea Urais kwenye mkutano Mkuu wa Chama, je Mahakama inaweza kuwa moved iwakataze Kamati Kuu isishiriki katika kuwapigia kura hao waliopendekezwa kwa sababu walihusika kwenye kikao cha awali cha kuwapendekeza ?
 
Back
Top Bottom