Taarifa ya awali kuhusu hukumu ya Mahakama Kuu masjala kuu Dar es Salaam, kuhusu Wanachama 19 waliofukuzwa CHADEMA

Taarifa ya awali kuhusu hukumu ya Mahakama Kuu masjala kuu Dar es Salaam, kuhusu Wanachama 19 waliofukuzwa CHADEMA

Ruzuku na viti maalum wapi na wapi?Usipende kuropoka
Unakataa nini? Kwamba hampokei ruzuku kwa mgongo wa wabunge wenu?

Msiwakatae wabunge wenu waliowapatia Ruzuku.

Kwenye kuropoka, wewe unawashwaje kwa pilipili ninayoitafuna?
 
Tumepokea hukumu iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2023, uamuzi wa Mheshimiwa Jaji Cyprian Phocas Mkeha;

1. Kwamba uamuzi wa kuwafukuza uanachama waliokuwa wanachama wetu 19 uliofanywa na Kamati Kuu ya Chama, umeendelea kusimama (Upo pale pale) na Mahakama imekubaliana kuwa taratibu zote za Katiba ya Chadema na Sheria za nchi zilifuatwa kikamilifu na Kamati Kuu katika kuchukua uamuzi huo.

2. Kwamba, maamuzi ya Baraza Kuu kuhusu Rufaa yamefutwa na hivyo Baraza Kuu linapaswa kukaa upya kusikiliza Rufaa; lakini Kamati Kuu ilishawafukuza Uanachama na uamuzi wake Judge kasema wazi upo sahihi.

Hivyo basi, kwa hatua ya sasa Chama kitawasiliana na Mawakili wake ili kutafakari hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kumkumbusha Spika wa Bunge kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa Kamati kuu ya Chama wa tarehe 27 Novemba, 2020 kwani Mahakama imethibitisha kuwa walishafukuzwa uanachama kihalali na taratibu zote zilifuatwa .

Tunawataka wanachama wetu watulie wakati huu chama kinapotafakari hatua za ziada.

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2023.

John Mrema
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya nje.View attachment 2842642
View attachment 2842645
Huyu binamu yake mzee mbowe mbona anataka kupotosha? swala la rufaa kupitia baraza kuu ilikuwaje ?
 
Hii taarifa ya kukurupuka sana haieleweki. TUIPUUZE. Sultani Mbowe ingependeza kama angeachia ngazi kwa sababu ni aibu kwa chama kilichojaa wanasheria kugaragazwa mahakamani na kina mama shupavu 19. Mtake msitake kina Halima na wenzake ni wanachama halali wa CHADEMA. Hamuwezi kuwafukuza kihuni.
Hivi mzee Mbowe na genge lake anajisikiaje kwa UZEMBE?
 
Ni maamuzi ambayo yalitarajiwa kufanyaw na hawa majaji uchwara. Majaji wanaopokea maagizo toka juu. Pathetic!
Kwa hiyo majaji ndio walimwambie mzee Mbowe awe mwenyeketi dhid ya rufaa ambao ilitokana na maamuzi yeye akiwa mwenyekiti?
 
CHADEMA nashauri muachane na hao wanawake.. chukueni ushauri wa Bwege " mi nilijua, hii kesi hatutoboi" kwa sababu serikali ipo pamoja na upande wa pili . wana backup wale...

rejea mifano ya kesi hizi, serikali ya chama cha kijani ilipo husika, na jinsi maamuzi ya kushangaza yaliyotolewa

1. Seif vs Lipumba
2. Mbowe vs jamuhuri ugaidi
3. kesi ya askari aliyemuua akwilina
4. kesi ya walio muua mwangosi
5. kesi ya uamsho vs serikali
6. Kesi ya ditopile, mramba
7. Kesi ya mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile
8. Kesi ya Sugu
9
.
Hapana wakomae nao tuone ubovu wa hizi mahakama za CCM
 
Heri ujinga kuliko upumbavu!Maamuzi na maelekezo ya mahakama yako wazi sana!lakini.....mh!hizo comment zingine duh!hakika tutafika tuendako tukiwa tumechoka sana!Ni heri enzi zile za chuo kikuu kimoja!
 
Busara itawale CHADEMA,kaeni na wabunge wenu muombane msamaha mambo yaendeleee acha kufukuzana,jifunze Kwa CCM
Chadema ijifunze kulogana, kufanyiana fitna au zengwe au kutoa maagizo kwa Watendaji wa Mihimili mikuu mitatu???
 
Tumepokea hukumu iliyotolewa leo Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2023, uamuzi wa Mheshimiwa Jaji Cyprian Phocas Mkeha;

1. Kwamba uamuzi wa kuwafukuza uanachama waliokuwa wanachama wetu 19 uliofanywa na Kamati Kuu ya Chama, umeendelea kusimama (Upo pale pale) na Mahakama imekubaliana kuwa taratibu zote za Katiba ya Chadema na Sheria za nchi zilifuatwa kikamilifu na Kamati Kuu katika kuchukua uamuzi huo.

2. Kwamba, maamuzi ya Baraza Kuu kuhusu Rufaa yamefutwa na hivyo Baraza Kuu linapaswa kukaa upya kusikiliza Rufaa; lakini Kamati Kuu ilishawafukuza Uanachama na uamuzi wake Judge kasema wazi upo sahihi.

Hivyo basi, kwa hatua ya sasa Chama kitawasiliana na Mawakili wake ili kutafakari hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kumkumbusha Spika wa Bunge kuhusu utekelezaji wa uamuzi wa Kamati kuu ya Chama wa tarehe 27 Novemba, 2020 kwani Mahakama imethibitisha kuwa walishafukuzwa uanachama kihalali na taratibu zote zilifuatwa .

Tunawataka wanachama wetu watulie wakati huu chama kinapotafakari hatua za ziada.

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2023.

John Mrema
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya nje.View attachment 2842642
View attachment 2842645
Nahisi kama hii ni "Taarifa Rasmi ya Chadema" basi ietolewa ikiwa haijapitiwa na kuhakikiwa na wanasheria wake.
 
Covid 19 ilikua ni michezo ya mbowe na jiwe kuhadaa watu,nani alikuambia jiwe na mbowe walikuwa maadui?
 
Lakini bado jaji kafanya masmuzi kama kawaida yao. Kapelekewa asome.
Kwanini hakuangalia kura zilizo pigwa atoe hapo kura za wajumbe wa kamati kuu kuona kama zilizo baki zina tosha kutoa maamuzi?
Kuna ujinga mahakama una fanya ambayo haiinei huruma pesa wanazo lipwa hawa covid19.
Hivi maamuzi ya Chadema kuwafukuza hawa wezi na jinai serikali inayo fanya kuiba pesa za umma ni ipi kubwa???
 
Mbowe alifikiri chama ni cha mkwewe, akaona anaweza kuwaburuza watu apendavyo
Huyu dikteta idd amini mbowe amekomeshwa
Mbowe sio basha lako wewe nenda chato Kia mzoga wenu ukapate kiburudisho chako mbowe hata mamayenu anamjua vizuri
 
Back
Top Bottom