Taarifa ya ikulu kuhusu rais kikwete kufanya mazungumzo na diamond

Taarifa ya ikulu kuhusu rais kikwete kufanya mazungumzo na diamond

heaven on desert

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
1,025
Reaction score
393
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo, Jumatatu, Februari 4, 2013, alikutana kwa muda mfupi na kundi la wasaniii wa muziki la Diamond Group wakiongozwa na kiongozi wa bendi hiyo Nasib Abdu maarufu kwa jina la Diamond.

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ikulu Ndogo ya mjini Kigoma, wasanii hao walimshukuru Rais Kikwete kwa msimamo wake
usioyumba wa kuunga mkono wasanii wa Tanzania na kuhakikisha kuwa wanafaidika na kazi zao.

Rais Kikwete alikuwa mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambako jana, Jumapili, Februari 3, 2013, alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma na ambako Diamond na kundi lake walitumbuiza.

Mwanamuziki huyo alimshukuru Rais Kikwete kwa juhudi zake nyingi na za wakati wote kuunga mkono wasanii wa Tanzania na hasa
kuunga mkono mapambano ya jitihada za wasanii hao kunufaika na kazi zao.

Shukurani kubwa za Diamond zilihusu hatua ya Rais Kikwete kumlipa mtaalamu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam aliyefanya utafiti
wa namna ya kuwasaidia wasanii, hatua iliyopelekea Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) kuanzisha mfumo wa kusaidia kuthibiti kazi za
wasanii mwaka huu. Mtaalamu huyo alilipwa Sh. milioni 20 kwa kazi hiyo.

Diamond amemwomba Rais Kikwete kuangalia jinsi gani Serikali inavyoweza kuwasaidia wasanii kupata malipo ya haki kutokana na
nyimbo zao zinazotumika kama milio ya simu.

Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
4 Februari, 2013
 
Vipi hajamshukuru kwa kufumbia macho ujangiri, ni punguwani tu atakayepongeza upuuzi huo tra wanakusanya mapato nyie mnasema mnafaidika wajinga kweli. badala ya kupigania hakimiliki nyie mnapongeza upuuzi. kwendazenu huko.
Jiulize unatoa wimbo vieo na audio unauweka kwenye blog dakika tu ushasambaa nchi nzima bure hizo ni akili kweli ? hovyo kabisa
 
Waende Uganda wakajifunze jinsi wasanii wanavyonufaika na kazi zao
 
yapo mambo ya msingi sana kwa sasa yanayosumbua nchi, kuonana na wasanii sio priority labda wawe walikuwa na mambo yao mengine.
 
hao walienda kumshukuru kwa kuwapa ulaji kwa kuwaakuka kuimba ujinga wao maadhimisho ya ccm.
 
Wasanii wenyewe ni akina nani yaani hawa wanaoimba matusi na kurap hovyohovyo kama mtu anatapika ndo wasanii hao
 
Hiyo inahitaji taarifa ya Ikulu? Aisee inaelekea mambo sasa yapo tambarare hapa Bongo!
 
Z
Z
Z
ra

????????????????????????????????????????????????????
 
Kama fastjet kafikia kutoa press release ya namna hii. ni muda muafaka hii wizara ya habari, michezo ... ya wakina Mukangara na Makala ifutwe tu. Wanakula mishahara bure wakati kazi zao zinafanya na fastjet
 
Wasanii wenyewe ni akina nani yaani hawa wanaoimba matusi na kurap hovyohovyo kama mtu anatapika ndo wasanii hao

unajifanya unadis akati computer yako na cm imejaa mamziki acha basi kuckiliza ka wanaimba matusi
 
Chinekeeee,,, Wonders shall never endo...

Rais anakutana na kijana wa Bongo fleva halafu anatoa ''press release''!!!!

Mi nahisi hii pR imetoka katika Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ya HUMU JF. Tunajua kuwa Salva Rweyemamu anaishi mjini kwa kujikomba, lakini sidhani kama amefikia kiasi hiki.

Rais angenikuna sana kama angekutana na Said SalimBakhresa aliyeajiri zaidi ya watanzania 6000 na sio mwanamuziki wa bongofleva ambaye hajawapa hata mikataba ya ajira waimbaji na wanenguaji wake na hivyo hasomeki kama ameajiri. For that matter kila anachokifanya ni kwa faida yake binafsi, kitu ambacho rais wa nchi akiamua kukutana na watu wote wenye mafanikio katika shuguli zao binafsi Ikulu hakutakalika. Tusubiri siku akikutana na Ruge, hah haa haaa, au ni kweli Rais anafanya ile biashara ambayo watu huwa wanaisema, I'm trying to connect dots here,,, why this PR, why?? Must be something fishy going on...
 
Ikulu wanatakiwa kujua ni mambo gani ya kutangaza na wakati gani wafanye hivyo.

Taarifa kama hizi na hasa timing yake zinaweza kumbomoa rais kuliko kumjenga kwa sababu zinaacha maswali juu ya pririty ya taasis hii. Mfano, rais ana muda wa kukafanya mazungumzo na Diamond - mwanamzuki - lakini hakuwa na nafasi ya kwenda Mtwara kuongea na wananchi kuhusu mustakabali wa huo ukanda na gesi!
 
mbona Jay z na Beyonce walipokutana na Obama ikulu ilitangazwa,obama alishutumiwa na nan kwa kitendo hicho?Matanzania bana
 
siwezi kushangaa msanii kuongea na msanii mwenzake,ila aibu ni pale chama cha siasa kumchukua jamaa akaimbe mara nimpende nani....mapenzi na siasa wapi na wapi????Kwani ROMA MKATOLIKI mwenye nyimbo za kisiasa mlimkosa???huyo ndiye alitakiwe akapige shughuri huko kigoma na si diamond eti nataka kulewa...kulewa na siasa wapi na wapi???
 
Back
Top Bottom