Taarifa ya JWTZ kwa Umma

Taarifa ya JWTZ kwa Umma

Status
Not open for further replies.
hivi kweli JWTZ inaacha kulinda mipaka ya nchi inahangaika na JF??
Kwanza watatuchukulia hatua gani?? kivipi?? na je hawaoni ni kupoteza muda kuhangaikia ma-blog badala ya kuhangaikia amani na usalama wa mipaka ya nchi??
 
Wambieni warudi wakaisome katiba ya nchi vizuri ndio warudi hapa na hoja ya msingi wanataka watu wasipeani habari JF imesaidia sana kuhabarisha watu kuna habari nyingi watu wamagazeti wanazitoa kwenye JF ni free website na ina kanuni zake na watu wanalipa kuendesha hii website Mods wanafanya kazi nzuri habari kama haina evidence mara nyingi wana delete kwahiyo ushauri kwahao mabwana fanyeni kazi zenu kwamujibu wa sheria za nchi kazi zenu ni ulinzi na usalama wa nchi mambo ya cyber crime ni polisi wapo pale kamata sio nyinyi kama mnaona kuna kosa limefanyika basi fungueni case msitupie mpira JF mkataka mtandao ufungwe ujue hii dunia ya utandawazi watu wengi wamekwenda shule labda muwaburuze wa bunge wetu pale mjengoni elimu yao ndogo na vyeti fake humu JF mwenye elimu ndogo labda ritz lakin most of them ni Phd
 
Watawachukulia hatua jf? Nijuavyo mimi jf=Watanzania, hii ina maana kua habari zinazopatikana jf huandikwa na wanachama wa jf ambao wengi wao ni Watanzania. Sidhani kama wasimamizi wa jf huwatuma watu kuandika habari yeyote, wao kazi yao ni kuchuja habari kama ni za ukweli ama za uzushi na kuzifuta.
Kwa mtazamo huu jwtz wanataka kupambana na Watanzania, sawa tusubiri ila wakati wanafanya hivyo wasisahau kusoma "disclaimer" ya jf waone inasemaje ndipo waje na mikakati yao.
 
Jamaa wapo in a combat mood , operesheni sechi and inkapasiteti JF sava.
 
Dah! Sikujua kwamba JF inafuatiliwa na watu wengi kiasi hicho na taarifa za humu zinachukuliwa kwa uzito mkubwa kiasi hicho.Hili kusema kweli limenistua kidogo lakini kwa upande mwengine limenipa moyo. Apongezwe sana mwanzilishi wa Jukwaa hii, Wapongezwe sana Ma mods kwa sababu hii ni ishara kuwa kazi yao waliyoifanya na wanayoifanya ni muhimu na inakubalika mno.Kadhalika ni jambo linalohitaji pongezi na la kutia moyo kwa wahabarishaji wanaotupa taarifa na kuchangia mijadala kwenye jukwaa hili. Ni wajibu wao tu kuongeza umakini ili kuhakikisha wanatupa kitu cha ukweli na uhakika.Kuhusu hiyo taatifa ya JWTZ; kama ilikuwa si sahihi; mleta mada anaweza kulaumiwa tu ikiwa hakuwa na vielelezo, ila kama alikuwa na vielelezo; cha kulaumiwa na chanzo cha habari yake.
 
JWTZ wasianze siasa za kiCCM CCM, JF iko nje ya uwezo wao. Bora watulie na kuhangaikia mambo mengine ya msingi kwao!
:majani7:sheria zipo zinazoruhusu jeshi kuingia mitaani.peruzi vitabu vya sheria
 
Watachukua hatua gani sasa...

Huu ni ulimwengu mwingine kabisa tofauti na magazeti....

Wacha kuji jambia wewe I'd yako fake mtu wenyewe unaishi sehemu hata gprs haisomi hakuna hata mnara wasimu ukitaka kusikiliza simu lazima upande juu ya mti sasa unaogopa nini?wata kushitaki kwa kosa gani na sheria zipi?
 
Another none in our Millitary sense.Hebu mtafuteni huyo Kanali wenu mliyempa kitengo nyeti bila kujua kuwa ni adui halafu baadaye akawatorokeni.Tumewangeni mkono kipindi chote shida mlivyokuwa mkituhitaji na sasa mnapanga kusimama kujipima dhidi JF? JF ni sisi, hivyo mmechagua kusimama dhidi yetu na yenu wenyewe. Habari ni za uhakika sijui shida yenu nini, au jamaa wameona ndiyo muda muafaka wa kuzorotesha JFkabla ya uchaguzi mkuu?JF siyo Mtwara, wala siyo M23.

Jamani jamani jamani Jf waooneeni huruma jeiwii, mkiwapiga ishu tatu tu za nguvu watasambaratishana wenyewe kwa wenyewe, please msiwape za uso mtauwa. Maana JF ni zaidi ya JW!
 
QHapa juzikati wana jf tulionyesha uzalendo wa hali ya juu,kutoa moral support kwa jwtz dhidi ya m23.leo jwtz hao hao wanakuja na
vitisho dhidi yetu.
 
Kwani tunataka kupigana na nani? Yaani kutoelewana kidogo na majirani tayari sie tushakunja ndita kiasi hiki?
 
Hata kama habari ni za kweli mnadhani watakiri hao...
 
Nadhani ni busara zaidi kama tukitaja chanzo huku tukibainisha tarehe/toleo la gazeti.......na hata ukurasa ikiwezekana......ili kuepusha *sintofahamu* hapa jukwaani.........ni mawazo yangu binafsi tu...........
 
Mwanzo habari za JF zilipo fika bungeni ndiyo ilikuwa mara ya jwanzavnaisikia jf na nikajiunga.hivyo ndivyo ninavyoamini pia kwa sasa kuwa jwtz ndiyo wanaitangaza jf.hivyo kufuta awatoweza ila wataleta members wapya.na pia itasaidia kuchangamka badala ya kina Ritz na buku7 kuwa na akaunti tanotano alafu tukajiona wengi
 
JW bana.... mie nilidhani siasa ziliondoka na mwanasiasa Shimbo.

Tatizo la jeiwii wanaifananisha JF na FB, Huku hatulingishiani mavakesheni huku pa kusemea, moderator mwenyewe anatukoma, zinapigwa za uso humu mpaka anadiliti posti chezea JF wewe!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom