Taarifa ya kupotea kwa ndugu Fakhru Issa Abeid (maarufu Osama)

Taarifa ya kupotea kwa ndugu Fakhru Issa Abeid (maarufu Osama)

Dah..kajiunga tarehe moja, Nduguye kapotea tarehe nne... kila la kheri mkuu.

Sijasema mtu anajitafuta. Maana hata ID inahusika na ndevu kiaina...kama Osama.

Badala utoe mchango unahangaika na terehe za kujiunga, we uliyejiunga Zamani umenizidi nini labda!!!, au tangu ujiunge kila ukipost unapewa posho na Wamiliki wa JF, Kwamba posho yako ya JF ishakuwa kiwango kikubwa mi ndo naanza au !!!!?
 
Poleni Sana katika utawala huu wa JIWE ,Kashaenda Kuungana na Wenzake wale 300+ wa kibiti,Yupo Mawinguni Kwa Sasa!!

siwezi kuamini dhana zako. hakika Dhana ni mbaya , na huenda kakupelekea kupata madhambi ikiwa dhana yako sio sahihi
 
Badala utoe mchango unahangaika na terehe za kujiunga, we uliyejiunga Zamani umenizidi nini labda!!!, au tangu ujiunge kila ukipost unapewa posho na Wamiliki wa JF, Kwamba posho yako ya JF ishakuwa kiwango kikubwa mi ndo naanza au !!!!?

Sasa twende kwenye mchango wangu... nduguyo alichukuliwa muda gani? waliomchukua walikuwa wangapi? waliondoka nae kwa kutumia usafiri gani? alikuwa anaishi hapo hapo Vigwaza au Dar? ana familia(Mke na watoto)? iko wapi?..na je ana muda gani hapo kazini? mahusiano yake na wafanyakazi wake hapo kazini yalikuwaje wiki moja kabla ya kupotea kwake? alikuwa ana nafasi yoyote ya uongozi/usimamizi hapo ofisini?
 
Kunywa maji tuliza munkari sheikh..

Sasa twende kwenye mchango wangu... nduguyo alichukuliwa muda gani? waliomchukua walikuwa wangapi? waliondoka nae kwa kutumia usafiri gani? alikuwa anaishi hapo hapo Vigwaza au Dar? ana familia(Mke na watoto)? iko wapi?..na je ana muda gani hapo kazini? mahusiano yake na wafanyakazi wake hapo kazini yalikuwaje wiki moja kabla ya kupotea kwake?.. alikuwa ana nafasi yoyote ya uongozi/usimamizi hapo ofisini?

Sijapanik ndugu ,kitambo sana nimetulizana kama maji ya kisima!!, I was just challenging u. Aidha, maswali yako ulouliza ni mazur , ngawa siwezi yajibu sasa hivi. Ntayajibu kadri ntakavyopata majibu yake.
 
kwa nini nickname ya Osama na sio nickname nyingine?

Hayo majina watu huwa wanapenda kuwabandika wale wenye ndevu nyingi, siyo yeye tu (na wengine wakiona una ndevu nyingi wanakuita Alkaida mpaka linakushika na linazoeleka ikiwa utalikubali ), uitanaji wa majina ya Osama na Alkaida ulianza tangu Osama Bin Laden alipoilipua Pentagon
 
Sijapanik ndugu ,kitambo sana nimetulizana kama maji ya kisima!!, I was just challenging u. Aidha, maswali yako ulouliza ni mazur , ngawa siwezi yajibu sasa hivi. Ntayajibu kadri ntakavyopata majibu yake.

Ukipata majibu karibu tuendelee kuona namna gani tunampata huyu nduguyo.
 
Hayo majina watu huwa wanapenda kuwabandika wale wenye ndevu nyingi, siyo yeye tu (na wengine wakiona una ndevu nyingi wanakuita Alkaida mpaka linakushika na linazoeleka ikiwa utalikubali ), uitanaji wa majina ya Osama na Alkaida ulianza tangu Osama Bin Laden alipoilipua Pentagon
kwa hiyo yeye jina LA Osama alilikubali
 
hv kwa hali ya kawaida wanakuja watu kazini kwangu, siwajui hawanijui wananiambia twende tukaongee, na mimi nawafuata tu hivi hivi? Mytake wanajuana na alipopelekwa anapajua, sema tatizo linabaki kwa nyinyi ndugu na jamaa ambao hakuwashilikisha
 
Ndebile,
Dah, Watanzania sio watu wazuri kabisa, badala ya kumuombea mwenzio mema, wewe unamuombea mabaya
 
Nimeuliza kama vituo vya polisi mmeuliza sijajibiwa
 
Nimeuliza kama vituo vya polisi mmeuliza sijajibiwa.

Kama kabebwa na polisi kwa nia njema wangeshatoa taarifa, lakini kama c kwa nia njema hata ukiulza cjui kama unaweza kuambiwa kwamba wao ndo wanaye.
 
hv kwa hali ya kawaida wanakuja watu kazini kwangu, siwajui hawanijui wananiambia twende tukaongee, na mimi nawafuata tu hivi hivi? Mytake wanajuana na alipopelekwa anapajua, sema tatizo linabaki kwa nyinyi ndugu na jamaa ambao hakuwashilikisha

Pia unaweza ukaitwa na anayekufahamu na ukapotezwa bila kurud, au hujui hilo ndugu, technique ni nyingi sana.
 
T11,

Kama unamaanisha kutoa taarifa Polisi , taarifa tayari na namba ya RB hiyo hapo (ipo kwenye post pia)>>>>>>>>>> (VIG/RB/212/2020 YA 05/06/2020) .
 
Muelimishe mwengine kuwa kuwa na ndevu si Ugaidi, ugaidi unaanza kwenye moyo wa mtu, na gaidi anaweza akawa yyte yule, awe mfupi mweusi mrefu mweupe bonge mwembamba, dini yyte ata asiekua na dini Jambazi

,
images-8.jpg
 
Hiyo namba haiwezi potea, imejilipua kwenda kwa wenzake.
 
  • Thanks
Reactions: T11
Back
Top Bottom