Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 966
- 6,019
Wasaalam.
4 Juni, 2024, Dodoma.
________________
Athuman Kapuya Foundation ni shirika lililosajiliwa mwaka 2021 ambapo, kwa kipindi chote limetekeleza matakwa ya kisheria ya uwasilishaji wa taarifa na kulipa ada.
Kwa mujibu wa usajili wao malengo waliyotekeleza na kupelekea hatua kuchukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Paul Chacha ni kinyume na Katiba waliyosajili na kinyume na Sheria ya Usajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (Non-Government Organizations) (NGOs) ambayo imeweka bayana utekelezaji wa NGOs unatakiwa kuendana na mila na desturi za Taifa la Tanzania na sio vinginevyo.
Kutokana na upungufu huo, Ofisi ya Msajili kupitia Bodi ya uratibu wa Mashirika hayo tayari imesimamisha utendaji kazi wa shirika hilo kote nchini kupisha uchunguzi na hatua zaidi. Baada ya uchunguzi kukamilika wahusika watachukuliwa hatua zote stahiki kwa mujibu wa sheria.
Nachukua nafasi hii kumpongeza Mhe. Paul Chacha, Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa uratibu mzuri wa Mashirika yanayofanya kazi katika mkoa wake na kwa hatua alizochukua kama mamlaka kamili ya usimamizi wa shughuli za serikali ikiwemo wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu kupitia sera ya ugatuaji madaraka kwenda Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Uratibu huu makini ndiyo umepelekea kuibuliwa kwa madhaifu ya shirika hilo.
Hivyo, natoa wito kwa mamlaka zote za tawala za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kuimarisha uratibu na ufuatiliaji na kuchukua hatua stahiki kwenye maeneo yao kwa mujibu wa sheria pale wanapoona kuna kukiukwa kwa sheria husika.
MWISHO.
Pia soma: Vitabu vinavyohamasisha mapenzi ya jinsia moja vyakamatwa Tabora