#COVID19 Taarifa ya tume ya Corona sio yetu watuambie walikoitoa

Nawasalimu kwajina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndugu zangu mheshimiwa Rais wetu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliunda tume ya Corona.

Taarifa ya tume imepokelewa Jana na wengi wanaendelea kutupa mrejesho ya kile kilichopo kwenye tume.

Naomba niseme taarifa ile sio yakwetu. Taarifa hii ni ya nchi iliyokumbwa na Corona na yenye hari tata sana. Taarifa hii nahisi ilikua ya Kenya sisi tumecopy na sehemu iliyoandikwa Kenya Tumeandika Tanzania. Tena Kenya yenyewe sio yaleo ni ile Kenya iliyoweka lockdown county 5, lakini yasasa haina huo mfumo unaopendekezwa na tume.

Wote tunajua nchi hii kila pembe hakuna taarifa za hilo janga hata toka kwenye mitandao ya kijamii hatuoni wala kusikia. Sehemu nyingi nchini toka 29 June 2020 serikali iliporuhusu shule kufunguliwa raia tuliachana na tahadhari za Corona. Masuala ya sanitizers, barakoa, maji tiririka na kutokukusanyika yalipotea.

Watu wanakula bata, misibani tunashiriki, viwanjani tunajaa, maeneo yote yamikusanyiko yanajaa mpaka basi lakini vifo wala wagonjwa wa Corona hakuna.

Mama yetu hajawahi kuchukua tahadhari ya Corona wakati wote alikua free ameanza kuvaa barakoa wiki mbili kabla ya ripot ya tume.

Leo Dunia inaanza kutengemaa, ulaya viwanjani wameanza kuruhusu mashabiki, vifo vinapungua, lockdown zimeondolewa eti tume inapendekeza lockdown Tanzania seriously!

Niombe wananchi tuchukue tahadhari lakini hii tume ituambie walikokusanyia data.
Wameshakula per diem! imeisha hiyo
 
Ndugu yangu...inasikitisha sana tena sana...na utasikia ving'ora via ma ambulance kila kona kutupa taharuki. Mwenye akili na ajue cha kufanya
 
Tume haijapendekeza lockdown angalia vizuri redio yako ina mende wengi pengine.
 
Njoo Kariakoo hapa uone msongamano.

Hakuna hata mmoja anayeugua mafua.

Halafu uwaambie wakajifungie vyumbani!! Hahahaaa.

Kuna ujinga mwingine hata kuusikiliza ni kichefuchefu!
Wakati wa maombolezk ya rais Magufuli watanzania walibanana bila tahadhari yoyote! Mabeberu walitazamia baada ya wiki 2 kutakuwa na mlipuko wa corona na watanzania watakufa sana!! Sasa ni miezi 2 imepita hakuna corona wala mtoto wake na corona!! Mabeberu wanashangaa!!
Sasa mabeberu wanataka kutuvika barakoa na kutupa chanjo halafu waseme tumeokolewa na barakoa na chanjo! Kinacholengwa ni kupora utukufu wa Mungu!
Watanzania tuwe macho, tumpe Mungu utukufu!!
 
Hi nchi siku za hivi karibuni toka watuambie tutoke maeneo ya PWANI ili tudikumbwe na kimbunga Jobo, nilianza kupata mashaka Sana na watu tunaowaita wasomi na wataalamu wetu, na hicho kikosi kazi kilicholeta ripoti ya CORONA ndo kimeniacha hoi kabisa.[emoji849][emoji849]
 
Tume haijapendekeza lockdown angalia vizuri redio yako ina mende wengi pengine.
Process ya lockdown itaanza na kupima, kama waliopimwa wakawa zaidi ya 5% maana yake maambukizi yanaelekea kuzidi toralable level. Na hapo ndio lockdown inabidi iwe introduced.
 
Corona ni matatizo yanayokuja na kuondoka. Ni ya msimu, tatizo ni ile hatari inayokuwepo ndani ya jamii wakati watu wanapoanza kuuguza na kuzika ndugu zao.

Sasa hivi tunaweza tusiwe na matatizo hayo lakini hatuwezi kuukwepa ukweli kwamba muda wowote unaweza kuibuka mlipuko.

Tuchukue tahadhari binafsi na zile za kifamilia hata kama masuala kama chanjo tunaona ni ya kibiashara zaidi.
Kwahiyo hakuna tofauti kati ya anayejikinga na corona na asiyejikinga kama sie? yani kwamba sisi na wengine wote ni sawa tu kwamba kutofuata social distance wala kuvaa barakoa haina athari zozote kwetu ukilinganisha na wenzetu wanaozingatia hivyo vitu?
 
Process ya lockdown itaanza na kupima, kama waliopimwa wakawa zaidi ya 5% maana yake maambukizi yanaelekea kuzidi toralable level. Na hapo ndio lockdown inabidi iwe introduced.
Sio lazima, tume imependekeza tuchukue hatua based on local conditions na sio kuiga wengine.
 
nadhani janga la corona liliandaliwa ili kumtoa Trump madarakani....ni mtazamowangu tu lakini
 
Kwahiyo hakuna tofauti kati ya anayejikinga na corona na asiyejikinga kama sie? yani kwamba sisi na wengine wote ni sawa tu kwamba kutofuata social distance wala kuvaa barakoa haina athari zozote kwetu ukilinganisha na wenzetu wanaozingatia hivyo vitu?
Tetea afya yako na ya wanaokuhusu hayo ya wengine waachie wao.
 
Mpumbavu wewe!!
Wewe una corona?

Majitu yamejifungia huko yanatoka na ma report ya kijinga unaunga mkono?

Hizi tume ndo zile za wizi kama zile za awamu ya nne. Na ukishaona serikali inaunda tume kwa kitu ambacho ni world wide ujiulize sana!!!

Kwani hajui nchii hii corona haikuwahi kuisha?
Nani hajui kuwa corono haina tiba?
Nani hajui hatua za kujikinga?
Aliyeunda tume amehamia nchii hii akitokea ww

Yaani ni ujinga ujinga tu.

Mtu atashauri watu wachanjwe...halafu anasisitiza watumisi wa umma na wa vyombo vya ulinzi na usalama......hufikirii tu kuna nini hapo?

Nani kwaambia hilo ndo kundi linaloshambukiwa na corona kuliko wengine.

Anyways, iko siku tutajielewa.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Heshimu Mawazo ya watu.
 
Nawasalimu kwajina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndugu zangu mheshimiwa Rais wetu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliunda tume ya Corona.

Taarifa ya tume imepokelewa Jana na wengi wanaendelea kutupa mrejesho ya kile kilichopo kwenye tume.

Naomba niseme taarifa ile sio yakwetu. Taarifa hii ni ya nchi iliyokumbwa na Corona na yenye hari tata sana. Taarifa hii nahisi ilikua ya Kenya sisi tumecopy na sehemu iliyoandikwa Kenya Tumeandika Tanzania. Tena Kenya yenyewe sio yaleo ni ile Kenya iliyoweka lockdown county 5, lakini yasasa haina huo mfumo unaopendekezwa na tume.

Wote tunajua nchi hii kila pembe hakuna taarifa za hilo janga hata toka kwenye mitandao ya kijamii hatuoni wala kusikia. Sehemu nyingi nchini toka 29 June 2020 serikali iliporuhusu shule kufunguliwa raia tuliachana na tahadhari za Corona. Masuala ya sanitizers, barakoa, maji tiririka na kutokukusanyika yalipotea.

Watu wanakula bata, misibani tunashiriki, viwanjani tunajaa, maeneo yote yamikusanyiko yanajaa mpaka basi lakini vifo wala wagonjwa wa Corona hakuna.

Mama yetu hajawahi kuchukua tahadhari ya Corona wakati wote alikua free ameanza kuvaa barakoa wiki mbili kabla ya ripot ya tume.

Leo Dunia inaanza kutengemaa, ulaya viwanjani wameanza kuruhusu mashabiki, vifo vinapungua. Makundi yaliyopendekezwa na tume kuchanjwa yanatakiwa kuangaliwa upya.

Niombe wananchi tuchukue tahadhari lakini hii tume ituambie walikokusanyia data.
Huna jipya zaidi ya kubeza juhudi za amkusudi kukabiliana na Covid.
Ninyi ndo mnataka watu wafe bila sayanzi kutumika .
Mbona mkupata malaria mnakimbilia kupima
Mbona mipata UKIMWI mnakimbilia kupimwa
Mbona mkihara mnakimbilia kupima

Na ninyi mliozoea kwenda kwa waganga wa kienyeji, hamjui kuwa KUPIMA kunaendana na STATISTICS ambazo nazo zinatumika ku analyse Afya ya Jamii.

Sasa nyie mmkekazana na Dorithy wenu kujifukiza, mnaua watu kwa kukosa hekima ya maarifa.
 
Tangu kuzuka kwa Corona nchini China mwaka 2019, mataifa mengi duniani yaliamua kuja na mbinu za kupambana na Corona kwa kufungia watu ndani(lockdown) kuvaa barakoa, social distance na mengine mengi ikiwemo Chanjo.

Tanzania tuliamua kuishi na Corona kwa kukataa kujifungia (lockdown) na shughuli ziliendelea kama kawaida na watu wakisafiri huku na huko, hata watalii kipindi cha Corona walikuwa wengi sana Tanzania.

Baada ya miaka miwili kupita tangu Corona izuke mataifa yaliyoongoza kwa vifo ni Marekani, China, India Brazil etc hayo mataifa ni tajiri yana mitungi ya oxygen mingi ,wana barakoa, na walijifungia.

Tanzania chini ya hayati rais Magufuli tuliamua kutumia njia za asili kama kunywa juice ya Tangawizi na malimao, kupiga nyungu na kumtanguliza Mungu mbele etc na matokeo yake impact ya Corona ni ndogo sana na tuliweza kuingia uchumi wa kati.

Cha kusikitisha baada ya miaka 2 ya Corona kupita, tume iloyoundwa na rais Samia Suluhu licha ya hiyo kamati kujaa maprofesa wa afya inataka kutuaminisha kwamba watanzania si lolote si chochote na tunatakiwa tujifunze kwa waliofanya lockdown huko nchi za nje!

Lakini ukweli ni kwamba ukipima impact ya Corona Tanzania inaonyesha tumefanikiwa sana na tulitakiwa tujivunie haya mafanikio hadharani na kuitaka dunia ije ijifunze Tanzania mbinu tulizotumia.

Hivi sisi watanzania nani aliyeturoga? Pamoja na ushahidi wote uliotuzunguka ukionyesha tumefaulu vita ya Corona bado maprofesa wetu wanataka tufanye kama walivyofanya India, Marekani, Rwanda?

Na Chadema nao wanashqngilia?
Point nzur but utasikia nyumbu
#wafrica tumelaaniwa#
#Mungu wabariki wazungu🤔🤔 sometimes huwaga nahis ss n nyan Kwel coZ hatujipendi hasa Bawacha na bavicha
 
Back
Top Bottom