Wapendwa wana chit chat ni dhahiri kwamba wote tumekuwa mashuhuda wa kilichokuwa kikiendelea katika iliyokuwa ndoa ya loya
Ruttashobolwa na
Madame B huku kwa upande mwingine ikimuhusisha
Chimbuvu. Kama ilivyo lengo kuu la tume ya Mahusiano na Ndoa hapa chit chat ni kuhakikisha kuwa members wanaendelea vizuri na kufurahia mahusiano yao, tume ilijitahidi kufanya jitihada za kutatua mgogoro ili ndoa iendelee kudumu lakini sote tumeshuhudia
Madame B kushindwa kutoa ushirikiano.
Nawashukuru wadau wa kamati mbalimbali na members kwa ujumla ambao walifanya jitihada za kuikoa ndoa hiyo.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwatangazia wana chit chat kuwa baada ya jitihada za muda mrefu kuokoa uhusiano wake na
Madame B ,Ndugu
Ruttashobolwa ameniletea taarifa za kumpa talaka RASMI
Madame B leo hii tar.01/12/2012 (siku ya kujitafakari TUKO WANGAPI).
Nikiwa kama mwenyekiti wa tume ya kuratibu mahusiano na ndoa, natangaza rasmi kuwa
Madame B sio mke wa
Ruttashobolwa tena.
Aidha ni vema nikawasilisha MASIKITIKO yangu juu ya kitendo cha ndugu
Chimbuvu kuanzisha uzi kwa lengo la kunivunjia heshima na kwa kunituhumu kuwa namtaka
Madame B huku akijua kuwa ni uzushi na kafanya hivyo kwa makusudi kabisa.ningependa kumshauri kuwa siku nyingine awe makini kabla hajafanya jambo.
Aidha ninapenda kutoa WITO kwa wana chit chat wote kufuata taratibu zilizowekwa kama tulivyokubaliana.
cc. KAMATI YA SCREENING
cc.KAMATI YA SHERIA
cc.KAMATI YA MAADILI
cc
Madame B
Wenu
Baba V
MWENYEKITI WA TUME YA KURATIBU MAHUSIANO CHIT CHAT 2012