Taarifa za habari kutoka kwenye media zetu zinaboa sana

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Yaani miaka nenda Rudi ukitazama ITV, TBC, ZBC, clouds, wasafi
Habari ni zile zile za matatizo.
1. Video
2. Watu kutekwa
3. Mafuriko.
4 Matatizo ya maji
5. Mlipuko wa magonjwa, kipindupindu, suala
6. Upungufu wadawa
7. Ugomvi wa wakulima na wafugaji
8. Ufisadi.
9. Ubakaji
10 Njaa n.k
11. Kukatika madaraja

Yani ukiwa Tanzania huwezi kuwasha TV ukatazama habari chanya za

1. Mambo ya technology
2. Mapinduzi katika kilimo
3. Biashara za Kimataifa
4. Tafiti mbalimbali
5. Masuala ya viwanda, kukuza uchumi n.k

Sasa hapa tutatokaje hapo
Shida aliziacha Nyerere hadi Leo zipo
 
Majibu yako hapa
Your browser is not able to display this video.
 
Hapa lipo jambo la kufanya...yaani wizara iweke regulations za asilimia ya habari za mazila ya kijamii,maswala ya maendeleo ,maswala ya teknolojia ,michezo n.k.
Ukiingia BBC huwezi kusikia unyang'au wa serikali ya Uingereza.
Aliyewafundisha waandishi wetu ametuletea majanga.
Good thing kwa sasa tuna social media .
 
Kweli kabisa
Yaani huwezi kusikia habari ukajifinza jambo
Waandishi wetu hawajishughulishi kusaka habari za kufundisha
 

Nadhani Utv ambayo ni channel ya Azam Tv wanajitahidi wapo tofauti kidogo, kwenye siku 5 za wiki yaani Jumatatu hadi Ijumaa, kuna siku moja kwenye taarifa ya habari kuna segment ya makala ya kilimo, elimu, teknolojia, afya hizo zote huwa ni makala mpya kila wiki.


Kueleweka zaidi ni kwamba Jumatatu wanaweka makala ya elimu hiyo segment wao wanaita ufunguo, Jumanne wanaweka Kilimo ambapo wanaita shambani, jumatano wanaweka Teknolojia, alhamisi wanaweka Afya wanaita Siha yako, ikimbukwe kwamba hizo makala huwa zinaruka kwa kupishana siku japo naweza kua nimekosea kutaja siku ila huwa ndani ya Jumatatu hadi ijumaa.
 
U nailed it .
 
Mbona huwa wanatangaza kiongozi...? Wewe sema tu kwa nchi yeti matatizo hayo yameshamiri now..,..
 
Nitajaribu kuifatilia azam
 
Tungali maskni wa kutupwa.
 
sasa ulishawahi kuona akili iliyochoka kama inaweza kuwa na kingine kipya? kimsingi ndio mambo ambayo watanzania wanataka kusikia mambo magumu na ya maana wala hawayataki
 
Mm naona n sawa tuu mana ndio mazingira yanataka hvy, kama tuu kila rais akiwa madarakani anasema jambo fulani itakuwa historia na rais anayefuata nae anadai jambo hilo hilo litakuwa historia sasa ww unategemea kuona kipi kipya.
 
Mm naona n sawa tuu mana ndio mazingira yanataka hvy, kama tuu kila rais akiwa madarakani anasema jambo fulani itakuwa historia na rais anayefuata nae anadai jambo hilo hilo litakuwa historia sasa ww unategemea kuona kipi kipya.
Kwamba Toka nchi ipate uhuru
Bado viongozi wananunua madawati, wanajenga rami, wananua mabomba
 
Wenye wajibu wa kuripoti hizo habari chanya ni kina nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…