Taarifa za Ikulu kwa lugha ya Kiingereza za nini wakati sisi ni Waswahili asilia?

Kwani anatoa taarifa moja tu?
 
Itoshe kusema Wewe ni zuzu.Samahani kama ntakuwa nimekukwaza
Hizo press release za ikulu ni for public consumption. “Public” si watanzania tu bali inahusisha hata wasio watz wakiwemo mabalozi ambao wanaweza kuwa hawajui kiswahili. Sasa ndg Rwandes kama wewe umepata press release ya kiswahili, inakuuma nini ikitolewa pia ya kiingereza? Kumbuka pia kwamba Kiingereza ni lugha rasmi (official language) ya jamhuri ya Tanzania.
 
Kama umeweza kuigundua hiyo taarifa ni ya Kiingereza, basi, unaifahamu Lugha ya Kiingereza na umeelewa.

Usituchoshe! Umejuaje taarifa imeandikwa kwa Kiingereza kama hujui Lugha ya Kiingereza???
 
Chadema imeharibu sana akili za vijana
 

Point yako nini hasa kwangu…Mjibu hivyo huyo mtoa mada
 
Sijaona kosa lake, Kahoji, na endapo hakuna toleo la Kiswahili ni halali yake kulalamika.
 
Hao ndio Wa Tanzania bhana. Akiwa hana hela halafu ukimpa atakosoa kuwa Sio hela Mpya. Yaani hata umuambie MUNGU akubariki yeye kimoyomoyo atasema "Huyu nayeee"
 
Kama umeweza kuigundua hiyo taarifa ni ya Kiingereza, basi, unaifahamu Lugha ya Kiingereza na umeelewa.

Usituchoshe! Umejuaje taarifa imeandikwa kwa Kiingereza kama hujui Lugha ya Kiingereza???
[emoji23][emoji23][emoji23] ila humu ndani.
 
Uhuru wa kuhoji ndio huu..Unahoji hata vyenye maana. Ni haki yako.
 
Huyu mswahili anataka kuonyesha kuwa ametoka Ulaya
 
Kweli we ni Kijakazi
 
BBC program ya focus on Africa alikuwa anasoma taarifa ya kiingeleza,labda kama hujawahi kumuona,hata Salim anasoma pia.

Japo binafsi pia sioni sababu ya barua ya kiingeleza wakati target ya audience ni Waswahili karibia asilimia 99
 
Alikuwa idhaa ya Kiswahili BBC, sasa anataka kuondoa shaka kwamba labda hakusoma.

Hakuna njia ya uhakika ya kuonyesha umesoma kwa mswahili limbukeni kama kubainisha unajua Kiingereza.
kwa hiyo hadi leo watanzania bado mnafikir finyu ya kudhani kuwa kujua kuzungumza kiingereza au kuandika ndio kuelimika?!,

Yaani watanzania bado akili zetu zimetawaliwa na wazungu?!

nadhani aliye turoga kafa, sasa sijui kama tutabadilika!!

JPM alijitahidi sn kuondoa hii kasumba ya ovyo..ya kutukuza lugha ya kiingereza na kuhakikisha Lugha ya Kiswahili inapewa umuhimu....ndipo alipo pendekeza mabadiliko ya sheria za kutoa haki mahakamani kwa lugha ya kiswahili.....ambapo baada ya kuaga dunia mchakato wake umepuuzwa.
Tunamuomba sana Rais wetu asipuuze matumizi ya Lugha ya kiswahili pale inapo bidi.
 
Kama ninhivyo Mbunge mmoja atoe hoja zake kwa kimombo huko bungeni uone kama hajakatazwa au mtangazaji atangaze kipindi chake kwa kimombo uone kama hajaondolewa studio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…