Taarifa za Ikulu kwa lugha ya Kiingereza za nini wakati sisi ni Waswahili asilia?

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeibuka na mfumo mpya wa kujulisha umma Serikali inayoyafanya kwa njia ya Kiingereza. Hii imeminya umma usiojua Kiingereza kutojua yanayoendelea nchini

Tabia kama hii naona ni bora Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Zuhura Yunus atambue kuwa kwa sasa hayupo Uingereza ni muhimu sana taarifa aziandike kwa Kiswahili kwani itasaidia umma wote kufahamu yanayoendelea nchini.

Zuhura tunaomba ufahamu sisi ni Watanzania na lugha yetu ni Kiswahili ; lugha unayotumia kutupasha habari za Ikulu ni mwiba kwa walio wengi hapa nchini

Tunaomba ubadilike na kama unaona ni muhimu kuandika lugha hiyo basi tuandikie na lugha yetu ya kiswahili.

View attachment 2120348
Kwani anatoa taarifa moja tu?
 
Itoshe kusema Wewe ni zuzu.Samahani kama ntakuwa nimekukwaza
Hizo press release za ikulu ni for public consumption. “Public” si watanzania tu bali inahusisha hata wasio watz wakiwemo mabalozi ambao wanaweza kuwa hawajui kiswahili. Sasa ndg Rwandes kama wewe umepata press release ya kiswahili, inakuuma nini ikitolewa pia ya kiingereza? Kumbuka pia kwamba Kiingereza ni lugha rasmi (official language) ya jamhuri ya Tanzania.
 
Kama umeweza kuigundua hiyo taarifa ni ya Kiingereza, basi, unaifahamu Lugha ya Kiingereza na umeelewa.

Usituchoshe! Umejuaje taarifa imeandikwa kwa Kiingereza kama hujui Lugha ya Kiingereza???
 
Yaani kuna watu kwa kulalamika hawajambo, kufanya kazi au kuwahudumia watu wa namna hiyo inabidi uwe na moyo wa chuma.

Wao kukiwa na baridi watalalamika, hiyo watalalamika, mvua watalamika, ukame watalaumu, wakidhulumiwa watalalamika, wakitendewa haki watalaumu, wakipewa watauliza kwa nini, wakinyimwa watalaani......

Kifupi wao wana shida na kila solution inayopatikana
Chadema imeharibu sana akili za vijana
 
Hizo press release za ikulu ni for public consumption. “Public” si watanzania tu bali inahusisha hata wasio watz wakiwemo mabalozi ambao wanaweza kuwa hawajui kiswahili. Sasa ndg Rwandes kama wewe umepata press release ya kiswahili, inakuuma nini ikitolewa pia ya kiingereza? Kumbuka pia kwamba Kiingereza ni lugha rasmi (official language) ya jamhuri ya Tanzania.

Point yako nini hasa kwangu…Mjibu hivyo huyo mtoa mada
 
Yaani kuna watu kwa kulalamika hawajambo, kufanya kazi au kuwahudumia watu wa namna hiyo inabidi uwe na moyo wa chuma.

Wao kukiwa na baridi watalalamika, hiyo watalalamika, mvua watalamika, ukame watalaumu, wakidhulumiwa watalalamika, wakitendewa haki watalaumu, wakipewa watauliza kwa nini, wakinyimwa watalaani......

Kifupi wao wana shida na kila solution inayopatikana
Sijaona kosa lake, Kahoji, na endapo hakuna toleo la Kiswahili ni halali yake kulalamika.
 
Yaani kuna watu kwa kulalamika hawajambo, kufanya kazi au kuwahudumia watu wa namna hiyo inabidi uwe na moyo wa chuma.

Wao kukiwa na baridi watalalamika, hiyo watalalamika, mvua watalamika, ukame watalaumu, wakidhulumiwa watalalamika, wakitendewa haki watalaumu, wakipewa watauliza kwa nini, wakinyimwa watalaani......

Kifupi wao wana shida na kila solution inayopatikana
Hao ndio Wa Tanzania bhana. Akiwa hana hela halafu ukimpa atakosoa kuwa Sio hela Mpya. Yaani hata umuambie MUNGU akubariki yeye kimoyomoyo atasema "Huyu nayeee"
 
Kama umeweza kuigundua hiyo taarifa ni ya Kiingereza, basi, unaifahamu Lugha ya Kiingereza na umeelewa.

Usituchoshe! Umejuaje taarifa imeandikwa kwa Kiingereza kama hujui Lugha ya Kiingereza???
[emoji23][emoji23][emoji23] ila humu ndani.
 
Uhuru wa kuhoji ndio huu..Unahoji hata vyenye maana. Ni haki yako.
 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeibuka na mfumo mpya wa kujulisha umma Serikali inayoyafanya kwa njia ya Kiingereza. Hii imeminya umma usiojua Kiingereza kutojua yanayoendelea nchini

Tabia kama hii naona ni bora Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Zuhura Yunus atambue kuwa kwa sasa hayupo Uingereza ni muhimu sana taarifa aziandike kwa Kiswahili kwani itasaidia umma wote kufahamu yanayoendelea nchini.

Zuhura tunaomba ufahamu sisi ni Watanzania na lugha yetu ni Kiswahili ; lugha unayotumia kutupasha habari za Ikulu ni mwiba kwa walio wengi hapa nchini

Tunaomba ubadilike na kama unaona ni muhimu kuandika lugha hiyo basi tuandikie na lugha yetu ya kiswahili.

View attachment 2120348
Huyu mswahili anataka kuonyesha kuwa ametoka Ulaya
 
Halafu cha ajabu huyo Zuhura alikuwa BBC -Kiswahili kwa nini hawakumuweka BBC- English ? Katoka huko kwa English people anakuja kutambia Waswahili nia English. Kwa nini alikuwa haongei English alipokuwa England BBC anakuja kuongelea English Tanzania kwa Waswahili ?

Lows IQ people kama Zuhura ndo maana English wamekataa kumuongezea Mkataba!
Kweli we ni Kijakazi
 
BBC program ya focus on Africa alikuwa anasoma taarifa ya kiingeleza,labda kama hujawahi kumuona,hata Salim anasoma pia.

Japo binafsi pia sioni sababu ya barua ya kiingeleza wakati target ya audience ni Waswahili karibia asilimia 99
 
Alikuwa idhaa ya Kiswahili BBC, sasa anataka kuondoa shaka kwamba labda hakusoma.

Hakuna njia ya uhakika ya kuonyesha umesoma kwa mswahili limbukeni kama kubainisha unajua Kiingereza.
kwa hiyo hadi leo watanzania bado mnafikir finyu ya kudhani kuwa kujua kuzungumza kiingereza au kuandika ndio kuelimika?!,

Yaani watanzania bado akili zetu zimetawaliwa na wazungu?!

nadhani aliye turoga kafa, sasa sijui kama tutabadilika!!

JPM alijitahidi sn kuondoa hii kasumba ya ovyo..ya kutukuza lugha ya kiingereza na kuhakikisha Lugha ya Kiswahili inapewa umuhimu....ndipo alipo pendekeza mabadiliko ya sheria za kutoa haki mahakamani kwa lugha ya kiswahili.....ambapo baada ya kuaga dunia mchakato wake umepuuzwa.
Tunamuomba sana Rais wetu asipuuze matumizi ya Lugha ya kiswahili pale inapo bidi.
 
Wewe ni jinga kabisa.Kwani hujui kwamba Lugha rasmi za kazi Tzn ni Kiswahili na kingereza?

Ofisi za umma zinatumia lugha gani? Kuwa kwako msawahili ndio tumesema uwe mbumbumbu wa kingereza?

Mwanaume mzima unakuwa na nongwa,hapo katoa taarifa kwa lugha zote je ingekuwa kingereza tuu ungefanyaje? Hovyo kabisa wewe mtoa mada.
Kama ninhivyo Mbunge mmoja atoe hoja zake kwa kimombo huko bungeni uone kama hajakatazwa au mtangazaji atangaze kipindi chake kwa kimombo uone kama hajaondolewa studio
 
Back
Top Bottom