Ng'wanamalundi
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,203
- 1,422
Kama ushindi ni nchi kuchakazwa kama Gaza ilivyofanywa, basi ni heri kushindwa kuliko kusema umeshinda ukiwa hali hiyo. Hebu turudi nyuma mpaka vita vya Mwaka 1967.Sote tukae mkao wa kusubiri halwa ya sinia za harusini iliyopikwa ikapikika na Gidemi. Wengi wakazi wa jiji la Dar, wa zamani wenzangu, nikiitaja halwa ya Gidemi ya sinia wanaielewa utamu wake.
Kwanza ilikuwa ikifika masinia yale wakati wa kugawanywa, kila mmoja anakodoa macho isije ikawahiwa na wajanja na kuisha kabla ya kufika kwako. Maana kuna watu wanajuwa kukomba halwa hao, si mchezo.
Kwenye tovuti za YouTube nimekuwa nikizifatilia sana habari za kijasusi za kutoka vyanzo vitatu, nilikuwa nazileta JF kiaina fulani, lakini kwa bahati nzuri au mbaya, wengi walikuwa hawazioni umuhimu wake. Hata uzi wa kwanza kabisa kabla ya kutangazwa kutakuwa na kusitisha mapigano niliuleta hapa JF kutokea moja ya vyanzo hivyo.
Kama kawaida, wengi ya wana JF mapoyoyo hawakuitilia maanani habari hiyo, baadhi waliitilia maanani na kuanza kuuliza maswali ya hapa na pale, mpaka siku mbili tatu baadae ilipotangazwa kweli kusitisha mapigano na kubadilishana wafungwa ndiyo wachache wenye uelewa wakaanza kuzifatia post zangu kwa kina.
Ya leo haya ni makubwa zaidi. Someni kwa kina na sikioizeni video clips nilizobandika humu, asiyeelewa aulize swali, sijaweza kuleta habari yote post itakuwa ndefu sana, isipokuwa nimechukuwa kidogo kidogo kutokea huko, kulikounguwa shoka mpini ukabakia:
Tafsiri kwa msaada wa "google translate".
55 Mpango wa Mossad, CIA, Misri na Qatar Kutana kwa ajili ya mvutano wa Israel na Gaza waendelea
Maafisa wa juu wa ujasusi wa kutoka Amerika, Israeli, Misri na Qatar wanakutana Qatar kujadili suala la uwezekano wa kusitisha mapigano moja kwa moja na kubwa zaidi ni jinsi ya kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Hamas.
Kwa nini wanakutana hivi sasa? Kama unaweza kufahamu kuwa kumekuwa na kipindi cha Makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano ambayo yameongezwa muda zaidi Wakati Mkataba wa awali wa kusitisha mapigano waliokubaliana wote.
Hamas na Israel walikubaliana kuhusu idadi ya watu ambao watakuwa wanaachiwa na Israel na Hamas. Kimsingi, majina ya ya wanaoachiwa hayatochapishwa chapisha kwa sababu za kibinadam. Hata hivyo walikubaliana kuwa watakuwa wengi wanawake na watoto na iliendelea hivyo kama tulivyokuwa tunashuhudia.
Makubaliano pia yalikuwa ile iwe hali ya awali huku kila upande ukiangalia njia bora zaidi ya kufanyika. Liliendelea zoezo hilo mpaka muda ukawa umeongezwa
Ikaonekana kuwa kwa mpango huuunoendelea sasa ni watu 300 tu kutolewa Israel na 100 tu kutokea Israel watakaoachiwa. kuna uwezekano pande zote zikapoteza wafungwa wale wakubwa ambao kila mmoja wao aliwania watolewe, hususan mazayuni ambao walishikiwa majenerali wao na wakuu mbali mbali wa kijeshi katika siku 48 za mapigano. Wakaona Duh hapa tutapoteza watu.
Na Mazayuni walipopata habari za Kiintelijensia kutoka kwa wafungwa waliowachiwa, wakaona hapa imekula kwetu. Ikumbukwe kuwa mateka wote wa Kiyahudi walioshikiliwa na Hamas waliozidi miaka 18 ni wanajeshi kamili na wale wazee wote ni wanajeshi na majasusi wastaafu, ndiyo hao wanaowekwa kwenye vijiji vya mpakani (Kibutz) na hawawekwi tu huko watu kiuholela.
Ikabidi kupitia Wakuu wa ujasusi, imeonekana hawa wanaongea lugha moja kuliko wanasiasa, itumike fursa na nafasi ya msingi hii ili kimsingi kujaribu na kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano bilqkupoteza Mfungwa yeyote mkubwa kwa pande zote. Hamas waakaelewa kuwa wao ndiyo wameshikiia turufu.
Tafadhali mengine yasikilize kwenye hii video clip, pia mnaweaa kuuliza chochote kwa ufafanuzi zaidi, kwani habari ni ndefu kidogo.
Cha muhimu tukae mkao wa halwa tungoje mapiganoi yasitishwe kabisa na Wapalestina wakabidhiwe nchi yao kamili kama mipaka ya 1967 ilivyokuwa.
Kwa namna yoyote ile, huu ni ushindi mkubwa sana kwa Wapalestina.
Viva Hamas Viva Palestine Viva wapenda haki wote duniani.
View attachment 2829047
Baada ya upelelezi wa kijasusi wa Israel kugundua kwamba Waarabu wanapanga kuishambulia Israel, Wayahudi walianzisha vita ya kustukiza ya kujihami mnamo tarehe 5 Juni 1967. Ndege za kivita za Misri hazikuwahi hata kuruka, zikateketezwa karibu zote zikiwa ardhini. Misri ndiyo alikuwa mbabe wa Waarabu. Akafuatia Syria. Naye akachakazwa vibaya sana. Akafuata Jordan. Vivyo hivyo akapigwa vibaya tu. Ikumbukwe kwamba Nchi hizi zinaizunguka Israel. Kwa hiyo israel ilikuwa ikipigana pande zote, sawa na Tanzania ipigane wakati ule ule na Kenya na Uganda kwa Kaskazini; Malawi, Zambia na Msumbili kwa Kusini; na Rwanda na Burundi kwa Magharibi. Vita vilidumu siku sita tu mpaka tarehe 10 Juni 1967. Misri wakapoteza Sinai; Syria wakapoteza Golan Heights; na Jordan wakapoteza Gaza, West Bank, na East jerusalem.
Ndani ya hiyo wiki moja tu Waarabu wakakubali yaishe, wakiachia Israel sehemu ilizoziteka. Na hivyo ndivyo ikawa, mpaka Mwaka 1973 Waarabu wlipoivamia israel kwa kustukiza toka pande zote zinazoizunguka Israel. Uvamizi huo ulifanyika tarehe 6 Oktoba 1973, siku ya sikukuu ya Yom Kippur, ambayo ni sikukuu kubwa kwa Wayahudi, sawa na Pasaka kwa Wakristu. Huo pia ulikuwa wakati wa mfungo wa Ramadhani kwa Waislamu. Waarabu wakajua ulinzi kwa Myahudi utakuwa poa siku hiyo. Kweli ndani ya siku tatu Waarabu wakakomboa maeneo mengi yaliyokuwa yametekwa tangu Mwaka 1967. Kukawa na sherehe kubwa miji mingi ya Kiarabu. Video zilisambaa zikionyesha Waarabu wakifurahia mitaani kwa kupiga risasi hewani. Myahudi akajipanga, akaanza kujibu mapigo na mpaka tarehe 25 Oktoba akawa amefaulu kuyachukua upya maeneo yaliyokuwa yamekombolewa, na akaenda mbali zaidi kwa kujitwalia maeneo mengine mapya. Huko kukawa ndiyo mwisho wa kujigamba ushindi kwa Mwarabu.
Mwarabu akajitafakari na akauona ukweli kwamba hana ubavu wa kukomboa ardhi yake kwa mtutu wa bunduki. Hivyo Misri, mbabe wa Waarabu, akaona aingie mazungumzo na Israel. Rais Jimmy Carter wa Marekani akawakaribisha Camp David huko Marekani Rais Anwar sadat wa Misri na Waziri Mkuu Menachem Begin wa Israel. makubaliano yalitiwa sahihi tarehe 17 Septemba 1978 yakiainisha Israel iirudishie Misri Sinai na Misri iitambue Israel kuwa nchi huru inayostahili kuwepo duniani, na waanzishe uhusiano wa kibalozi. Na hivyo ndivyo ikawa. Makubaliano hayo yalipelekea Sadat na Begin kutuzwa Nobel Peace Prize ya mwaka 1978.
Makubaliano yanayofanana na hayo yalitiwa sahihi tarehe 17 Mei 1983 kati ya Israel na Lebanon, yakihusisha Israel kuondoa majeshi yake nchini Lebanon lakini Israel ibakishe ukanda wa kinga wa kilomita zipatazo 19.
Kwa ufupi, tangu mwaka 1967 hakuna ardhi ya Mwarabu iliyokombolewa kwa mtutu wa bunduki. Mwaka 1973 kulikuwa na sherehe kubwa kwa ushindi wa mpito wa Mwaarabu, zilizofuatiwa na kilio cha kupoteza hata ziada ya ardhi yao. Leo hii Mwarabu anasherehekea 'ushindi' wa Hamas wa tarehe 7 Oktoba 2023 ambao umempatia maafa makubwa na kumrudisha nyuma kimaendeleo zaidi ya pale alipokuwa kabla ya mashambulizi yake. Sasa ushindi gani huu wa mtu kufurahia?