Taarifa za uhakika nilizonazo Manara ndiye anaihujumu Simba SC kila ikicheza na Yanga SC atimuliwe

Taarifa za uhakika nilizonazo Manara ndiye anaihujumu Simba SC kila ikicheza na Yanga SC atimuliwe

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Msemaji wa Simba SC Haji Manara binafsi nakuheshimu mno na nisiwe pia Mchoyo wa Kukusifia na Kukupongeza kuwa ndani ya Klabu ya Simba nawe umeweka Alama yako ya Mchango wako mkubwa wa Kuitangaza vyema Simba SC na kuwa Brand hivi ilivyo sasa.

Hata hivyo Msemaji wa Simba SC Haji Manara leo nitaomba Unisamehe kwa Kuyasema haya Kwako ambayo najua hutoamini Krav Maga Mimi nimeyajuaje ila nikuambie tu nimeyapata kutoka kwa Watu wako wa karibu kutoka Mikocheni unakoishi, Kwenu Ilala na Maskani yako ya Buguruni na kwa Mru Mmoja muhimu ndani ya Klabu ya Simba.

Msemaji wa Simba SC Haji Manara mara nyingi Simba SC ikicheza na Yanga SC kwa Mapenzi makubwa uliyonayo kwa Baba yako Mzazi huwa unapenyeza Taarifa Nyeti za Kambi ya Simba SC hasa zile za Kamati za Ufundi/ Utamaduni kwa Yanga SC.

Msemaji wa Simba SC Haji Manara imenibidi leo tena nirejee Moja ya Interviews zako ulizofanya na EFM Radio ambapo kwa Kinywa chako ulishawahi Kukiri kuwa kamwe Simba SC haiwezi Kukufanya ukaacha kuwa na ukaribu na uliowaita Matajiri na Marafiki zako Wakubwa akina Gharib Said Mohammed (GSM), Injinia Hersi Said na wengineo ndani ya Yanga SC.

Msemaji wa Simba SC Haji Manara najua kwa Siku nyingi sana umekuwa ukikalia Kuti Kavu ndani ya Simba SC kwa tabia zako zilizochokwa japo unavumiliwa na Kukingiwa Kifua na Mshkaji wako Mwekezaji na Tajiri Mo Dewji na kwamba Jeuri ya Kukubalika na Watu wa Azam mpaka kuwa Balozi wa Products zao na Ahadi ya GSM kukupa Mkataba mnono kumekufanya ujawe na Kiburi huku ukitafuta Makosa kwa Makusudi ili utimuliwe Klabuni Simba.

Msemaji wa Simba SC Haji Manara hata ile Press Conferences yako ya juzi tu ambayo uliiharibu kwa Upuuzi wako dhidi ya Mwandishi wa Kike wa Habari za Michezo wa Clouds FM Prisca Kishamba ulidhamiria ulichokifanya ili tu Klabu ya Simba ikufukuze uende huko ambako unahitajika Kibishara ila nasikitika Uongozi wa Simba SC haujalijua hili na bado tu wanaendelea Kukukumbatia huku ukiihujumu katika Mechi zake na Yanga SC.

Msemaji wa Simba SC Haji Manara hakuna Kitu kilichoniuma na kunipandisha Hasira zangu Krav Maga leo kama Kitendo chako cha Kupenyeza Taarifa Nyeti ya Jambo la Kiufundi / Kiutamaduni ambalo Simba SC ililifanya pale Uwanjani kwa Mkapa mpaka Yanga SC kupitia Wachezaji wake wakakikwepa na kupitia Mlango mwingine kabisa hivyo Kutuharibia Mipango yetu yote.

Msemaji wa Simba SC Haji Manara binafsi ningeshangaa sana kwa Fadhila ambazo GSM wanakupa tokea Siku yako ile ya Harusi na Mkeo ambaye ni mwana Yanga SC lia lia kama alivyo Baba yako Mzazi kama nawe leo hii usingewapa Ushirikiano wako wa Kuisaliti Simba SC kwa kuwapa Taarifa / Siri za Kambi.

Uongozi wa Simba SC tafadhalini achaneni upesi sana na Msemaji Haji Manara vinginevyo Matokeo mabaya dhidi ya Yanga SC mtaendelea kuyapata kwani huyu Msemaji wenu / wetu ndiyo Mvujishaji Mkuu wa Taarifa zetu nyingi za Siri ya Kambi kwa Yanga SC ili amfurahishe Baba yake Mzazi na Mkewe na mkiudharau huu Ushauri wangu ipo Siku tu mtakuja Kunikumbuka Krav Maga hapa Mtandaoni JamiiForums.

Kwa wale ambao labda watashangaa ni kwanini Krav Maga nazungumzia sana Fitna za Mambo ya Kiufundi ule wa Kiutamaduni ni kwamba 55% ya Mechi za Simba na Yanga huwa ni Utamaduni wa Mwafrika, 30% ni Kuhonga Wachezaji wa Timu Pinzani au Waamuzi na 15% tu ni Jitihada za Wachezaji ndani ya Uwanja.

Na wala simsemi hapa Msemaji wa Simba SC Haji Manara labda nikimaanisha kuwa Simba SC ni Timu Jabali isiyoweza Kufungwa na Yanga SC ila haingii Akilini Timu ina ball possession ya 70% hadi 75% huku Wachezaji wakikosa Magoli ya Wazi na Mipira mingine unaona imepigwa Golini na inaenda Kuingia mara ghafla mpira unabadili mwelekeo wake na kutoka nje kidogo tu ya Goli halafu usiseme kuwa kuna Mkono wa Mtu hasa Kiutamaduni.

Simba SC mtimueni Haji Manara haraka.
 
Sasa hizi hujuma ulizoongelea na mechi ilivokua hakuna uhusiano kabisa.

Cha muhimu hapa ni kujipanga kwajili ya mechi ijayo lakini ukikomaa na hizi nadharia zako hakuna kitu wala faida yoyote.

Natamani sana washabiki wa mpira bongo waache haya mawazo potofu kama uloandika hapa.
 
Umechanganyikiwa wew kunywa maji mengi walau upate kazii ya kwenda kukojoa mara kwa mara sio kujaza saver za jf kwa takataka zako.

Kiufupi wew ni kama mtu aliyetapeliwa bado unatapatapa kutafuta sababu.

2016 December man u alimfunga arsenal kwa possession ya 21% arsenal 79% tena walikua nyumbn kwa arsenal.

Sasa Simba ni nan mpka asifungwe? Alishafungwa Barca kwa possession ya 80%+ huko acha kuchafua watu.

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Huna unachokijua nakushauri Kalale tu.
Weka ushahidi hapa kama una hizi ni porojo tu kama zile za manara kwa prisca kishamba.

Hapa utaruka ruka kumlaumu manara sijui nani laumu kila mtu lakini hakuna kitu utabadilisha.
 
🤣🤸🐒
20210704_015338.jpg
 
Ninacho mlaumu Manara ni mbinu zake ovu za kuwajaza sifa wachezaji wa Simba ili kuwaondolea umakini wa kupata ushindi kukiwa na mechi na Yanga fc.

Anawasifia wachezaji hadi wanabweteka kupigana uwanjani dhidi ya Yanga. Hii ni mbinu ya kuiangusha Simba inapocheza na Yanga, kwa kuwavimbisha kichwa wachezaji. Anawalazimisha wachezaji wa Simba wawachukulie dhaifu wachezaji wa Yanga bila kusahau tumeshafungwa na Prison na Ruvushuting kwa kujiamini kupita kiasi. Hili la Baba Yanga, Mke Yanga na Mfadhiri Yanga kuna haja ya kuliangalia kwa undani.

Mwisho namwomba Kocha wa Simba Gomes, asimpange John Boko kwenye mechi za Simba na Yanga. Hakuwahi kufanya vizuri ktk mechi zote na Yanga.

Mechi nyingine anajituma sana na anafanya vizuri.
 
Msemaji wa Simba SC Haji Manara binafsi nakuheshimu mno na nisiwe pia Mchoyo wa Kukusifia na Kukupongeza kuwa ndani ya Klabu ya Simba nawe umeweka Alama yako ya Mchango wako mkubwa wa Kuitangaza vyema Simba SC na kuwa Brand hivi ilivyo sasa...
Umeamua kujifichia huku? Tunakujua hata hutumie I'd gani uandishi wako Ni ule ule. Haya endeleeni kuloga tuone mtafika wapi.
 
Msemaji wa Simba SC Haji Manara binafsi nakuheshimu mno na nisiwe pia Mchoyo wa Kukusifia na Kukupongeza kuwa ndani ya Klabu ya Simba nawe umeweka Alama yako ya Mchango wako mkubwa wa Kuitangaza vyema Simba SC na kuwa Brand hivi ilivyo sasa...
polen mnamtafta mchawi simba mtazifunga tim zote sio yanga tena uleule uwanja pendwa mnaojidah nao
 
Huyu mbona kama yule jamaa[emoji848][emoji848]
 
Uchawi wenu umewarudia hakika

Najua Sana simbwa mnatembelea nyota za watu na watu walishaanza kuzizima hakika mtakoma

Gentamicin
 
Back
Top Bottom