Simba kuifunga Yanga inabidi itumie nguvu za ziada hasa kama Yanga wanautaka ushindi.
Kumbukeni Yanga ilianza kuundwa kabla ya Simba.
Hivyo wananchi wengi hasa wenye madaraka ni wapenzi wa Yanga FC
Viongozi wa CCM wengi ni Yanga.
Maana yake vigogo wa serikali wengi ni Yanga.
Wafanya biashara wengi ni Yanga kwasababu wanataka kuwaridhisha vigogo wa CCM na wa Serikalini maana wao cha msingi kwao ni kupendwa na Vigogo ili wafanye biashara zao vizuri.
Simba tuna MO Dewji peke yake na mnakumbuka misukosuko aliyoipitia na anayoipitia toka atake Hisa za Simba.
Kama angekuwa na moyo mdogo MO ungeisha jiondoa Simba.
MO anatukanwa kupita wafadhiri wa Yanga na watu wanaona kawaida tu.
Sijaona wafadhiri wa Yanga wakidhihakiwa kama MO.
Simba tuna MO peke yake,
Wenzetu wana
Rostam
Manji
GSM
Kikwete
UVCCM wengi akina Joketi Mwegelo
Wachawi nguli kama Mzee Mpili
Meneja wa Uwanja wa Taifa
Na wengine wengi tu.
Yanga ni kama mtoto wa nyumbani na Simba ni mtoto wa kufikia.
Ndio maana wanadeka na wanasikilizwa.
Marefa waniogopa Yanga kwa sababu ya hii hali.
Hata beki akidaka mpira sio jambo rahisi kutoa penati dhidi ya Yanga. Kwa Simba ile ya jana ingetolewa penati haraka tu.
Hivyo Yanga wanauwezo mkubwa kuifunga Simba nje ya Uwanja.
Wana Sapoti kubwa sana, kuliko Simba.
Tafadharini Simba kama hamlijui hili na kujifanya mnaujua mpira, mtafungwa mechi zote tatu tutakazo kutana na Yanga mwaka huu.
Yaani mechi ya
F.A.
Ngao ya Jamii
Ligi ya Vodacom.
Na tutaendelea kufungwa mechi za mbeleni.
Wachezaji wa Simba, Benchi la Ufundi, Viongozi wa Simba kuweni makini sana na hali hii.
La Simba tutaendelea kufesheheshwa kila kukichwa kwa kufungwa na timu tunayoizidi Ubora kwa viwango vya CAF.
Wenzetu wana support kubwa sana.