Taarifa za uhakika nilizonazo Manara ndiye anaihujumu Simba SC kila ikicheza na Yanga SC atimuliwe

Simba kuifunga Yanga inabidi itumie nguvu za ziada hasa kama Yanga wanautaka ushindi.

Kumbukeni Yanga ilianza kuundwa kabla ya Simba.
Hivyo wananchi wengi hasa wenye madaraka ni wapenzi wa Yanga FC

Viongozi wa CCM wengi ni Yanga.
Maana yake vigogo wa serikali wengi ni Yanga.

Wafanya biashara wengi ni Yanga kwasababu wanataka kuwaridhisha vigogo wa CCM na wa Serikalini maana wao cha msingi kwao ni kupendwa na Vigogo ili wafanye biashara zao vizuri.

Simba tuna MO Dewji peke yake na mnakumbuka misukosuko aliyoipitia na anayoipitia toka atake Hisa za Simba.
Kama angekuwa na moyo mdogo MO ungeisha jiondoa Simba.
MO anatukanwa kupita wafadhiri wa Yanga na watu wanaona kawaida tu.
Sijaona wafadhiri wa Yanga wakidhihakiwa kama MO.

Simba tuna MO peke yake,
Wenzetu wana
Rostam
Manji
GSM
Kikwete
UVCCM wengi akina Joketi Mwegelo
Wachawi nguli kama Mzee Mpili
Meneja wa Uwanja wa Taifa
Na wengine wengi tu.

Yanga ni kama mtoto wa nyumbani na Simba ni mtoto wa kufikia.
Ndio maana wanadeka na wanasikilizwa.

Marefa waniogopa Yanga kwa sababu ya hii hali.
Hata beki akidaka mpira sio jambo rahisi kutoa penati dhidi ya Yanga. Kwa Simba ile ya jana ingetolewa penati haraka tu.

Hivyo Yanga wanauwezo mkubwa kuifunga Simba nje ya Uwanja.
Wana Sapoti kubwa sana, kuliko Simba.

Tafadharini Simba kama hamlijui hili na kujifanya mnaujua mpira, mtafungwa mechi zote tatu tutakazo kutana na Yanga mwaka huu.
Yaani mechi ya
F.A.
Ngao ya Jamii
Ligi ya Vodacom.
Na tutaendelea kufungwa mechi za mbeleni.

Wachezaji wa Simba, Benchi la Ufundi, Viongozi wa Simba kuweni makini sana na hali hii.
La Simba tutaendelea kufesheheshwa kila kukichwa kwa kufungwa na timu tunayoizidi Ubora kwa viwango vya CAF.

Wenzetu wana support kubwa sana.
 
Lile tukio la utopolo kupita mlango usio rasmi, lilinishangaza kwamba ni lazima wamepewa nyepesi tu!
Lile goli la utopolo ni la kichawi kabisa, jinsi wachezaji wa simba walivyokuwa wamejipanga wakati ule mpira unapigwa ni kama walipumbazwa!
Uko sahihi 100% Ndugu kwani kuna Mtu ndani ya Simba SC na inasemekana ni Haji Manara ( Msemaji Wetu ) ndiyo amevujisha Siri hiyo kwa Baba yake Mzazi na Mkewe ambao ni wana Yanga SC watupu.
 
Nasikitika ni kwanini andiko lako hili zuri na lenye ukweli mtupu Watu hawajakupongeza na kukupa Likes nyingi tu Ndugu. Umeandika sahihi na nakuunga mkono 100% kabisa na umenena hasa nimekuelewa.
 
Mhh,,hapana Haji huyu aliyetaka kumvesha baba yake jezi ya Simba mbele ya umma hawezi kuihujumu Simba!
 
Simba haina watu smart apa uongozini wote makopo tupu
 
Lile tukio la utopolo kupita mlango usio rasmi, lilinishangaza kwamba ni lazima wamepewa nyepesi tu!
Lile goli la utopolo ni la kichawi kabisa, jinsi wachezaji wa simba walivyokuwa wamejipanga wakati ule mpira unapigwa ni kama walipumbazwa!
Kwa mawazo haya mpira wetu una safari ndefu sana!!
 
Nasikitika ni kwanini andiko lako hili zuri na lenye ukweli mtupu Watu hawajakupongeza na kukupa Likes nyingi tu Ndugu. Umeandika sahihi na nakuunga mkono 100% kabisa na umenena hasa nimekuelewa.
Mara nyingi mtu anayesema jambo la ukweli huwa haonekani kama ana hoja muhimu.
Sababu moja wapo ni kuwa watu wengi hawana weledi wa kutosha wa kutafakari mambo ya msingi.
Pili watu wengi wanapenda kusikiliza na kuamini habari za uwongouwongo kama za Manara.
Nashukuru wewe sio mmoja wao.
Inatosha sana.
 
Mhh,,hapana Haji huyu aliyetaka kumvesha baba yake jezi ya Simba mbele ya umma hawezi kuihujumu Simba!
Tegemea Breaking News ya Simba SC kumuhusu Yeye Ndugu sawa? Ukiona nimekuja na taarifa hapa jua nimeipata kutoka Jikoni na ndiyo maana hata Signature yangu tu inasema 'Gifted Intellectually, Knowledgeable, Challenger and Well Informed' Ndugu.
 
Kwani wao WAMELALAJE πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ mji kimya, msipende kwenda uwanjani na maneno ya Manara kichwani huku mkiwa na matokeo yenu mifukoni,mtadondoka mfe kwa presha.
 
Ahsante na Shukran Ndugu kwa Kunielewa Krav Maga. Ipo Siku hiki nilichokileta hapa Kitajithibitisha na Kujidhihiri.

Hapa nimeamua Kuwapa ukweli mtupu wana Simba SC hasa hasa Uongozi. Wamuondoe upesi sana Msemaji wa Simba SC Haji Manara kwani ndiyo Mpigaji Shoti Mkuu kila pale Simba SC ikicheza na Yanga SC kwa kutoa Siri za Klabu kwa Baba yake Mzazi na kwa Marafiki zake wakubwa wa Yanga SC Gharib ( GSM Mwenyewe ) na Injinia Hersi Said.
 
Umeandika takataka tu hapa, kama unaongelea uchawi kwa hiyo Simba wao hawakuwa na huo uchawi.

Sasa kama ni swala la uchawi kwa nini Simba watumie mamilioni ya fedha kwenda kununua wachezaji wa kigeni na kuwalipa pesa nyingi kila mwezi kwa nini wasiwatumie tu wachezaji wa hapa halafu waongezee na huo uchawi na mambo yaende?

Madai hayo uliyotoa dhidi ya Manara ni ya kijinga sana na hayana mahusiano yoyote na uchezaji wa timu ya Simba na hayahusiani na matokeo ya mechi labda kama Manara alikuwa anachezea Simba.

Elewa kwamba, football is a game of chance, hivyo sio lazima kwamba Simba ashinde muda wote anapocheza kwani hachezi na vipofu.
 
Hawa watu akina GSM, Manji, Kikwete, Rostam, ni wenye uwezo mkubwa sana.
Kama kuna mtu yupo karibu nao, na ni Kiongozi wa Simba, ni lazima atiliwe shaka.
Pesa ni pasua kichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…