Taarifa za uhakika nilizonazo Manara ndiye anaihujumu Simba SC kila ikicheza na Yanga SC atimuliwe

Hawa watu akina GSM, Manji, Kikwete, Rostam, ni wenye uwezo mkubwa sana.
Kama kuna mtu yupo karibu nao, na ni Kiongozi wa Simba, ni lazima atiliwe shaka.
Pesa ni pasua kichwa.
Msemaji wa Simba SC Haji Manara anatumaliza kwa kupitia hawa hawa uliowataja hapo ambao wengi wao ndiyo walikuwa wakimuweka mjini na bado wanaendelea kumuweka mjini mpaka sasa na kwa 99% ndiyo waliiratibu Harusi yake, bata wakampa na mpaka Zawadi ya Gari wakampa na hivi sasa yupo katika Payroll ya GSM wanaoidhamini Yanga SC.
 
Tegemea Breaking News ya Simba SC kumuhusu Yeye Ndugu sawa? Ukiona nimekuja na taarifa hapa jua nimeipata kutoka Jikoni na ndiyo maana hata Signature yangu tu inasema 'Gifted Intellectually, Knowledgeable, Challenger and Well Informed' Ndugu.
Akuna cha Breaking News wewe,Manara awezi kupigwa pini pale Simba na hata kama habari unazosema zipo Simba ya sasa sio ya kukurupuka bila kufanya uchunguzi.

Manara awezi kuihujumu Simba, hata kwa kuota ndoto Simba wanafungwa hawezi kuota hiyo ndoto.
 
Simba 0-Yanga 1 Mchezo uliisha hivyo,ungeisha tofauti huu uzi usingefikirika hata kuandika. Hata sisi ni wana Simba tunakiri tumepigwa.
 
Mkuu wewe ni mwana simba pekee duniani mwenye akili timamu

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Genta katika ubora wako.
 
Kwa hiyo yanga walivyopigwa 4-1 mechi ya FA msimu uliopita hao uvccm, Gsm, Kikwete hawakuwepo? Kumbuka kombe la FA kwa yanga msimu uliopita lilikuwa muhimu sana maana ilikuwa tiketi ya kimataifa lakini walipigwa na kutolewa. Enzi za utawala wa Kikwete hao Yanga wamewahi pigwa 5-0, penati kama mbili hivi,kwa hiyo hoja yako ya marefa sio sahihi.

Kwa akili ya kawaida ni yupi anaetoa support ya maana kwa klabu kati ya Mo alie peke yake na hao uliowataja kwa yanga? Kwa misimu karibia minne yanga haina mwelekeo wowote wa maana halafu wewe unawaona wa maana hao kisa tu ushindi wa derby.Ni heri Mo abaki peke yake maana sote tunaona simba inavyocheza na kupata mafanikio hapa nyumbani na huko CAF hata kama inafungwa na yanga kuliko eti Mo apate support ya sijui uvccm , sijui Mwinyi halafu mwisho wa siku klabu inakuwa ipo ipo tu. Man u wameifunga Man city kwenye derby ya hivi karibuni lakini kamwe hawawezi kujivunia hilo kuliko kutwaa epl.
Hakuna anaefurahia kufungwa kwenye derby ila ni upuuzi kudhania umefungwa kwa sababu ya nje ya uwanja zaidi sababu ya wale kupewa support na watu maarufu. Hata wanayanga wanataka wapate Mo wao wa kuwapeleka mbele zaidi na sio kupewa support na matajiri au wanasiasa kwenye mechi tatu au nne.
 
Acha wivu wewe.Aidha leo umeamua kuweka wazi kwamba Simba mnategemea ushirikina kwa 55 %, Kuhonga marefa /wachezaji wa Timu pinzani kwa 30% Na jitihada za wachezaji wenu kwa 15% . Hovyo kabisa
 
Hatari sana, duh! kumbe kweli Manara ni kanjanja sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…