MAANA YA UTAFITI
Utafiti ni njia ya kupata utatuzi wa suala fulani katika jamii na mazingira ya binadamu kwa njia ya uchunguzi unaotumia nadharia za kitaaluma na kisayansi.
Aidha utafiti ni njia maalum inayofuatwa ili kufikia ujuzi au taarifa muhimu inayokusudia kuchangia katika usomi wa kina na uchunguzi wenye mweleko wa kimaantiki. Utafiti wowote ule hauwezi kufanyika wala haukamiliki pasi kuongozwa na nadharia kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Kuna utafiti wa taasisi ya SSRC imekuja na utafiti wa kura za maoni kuwa mgombea wap wa Uraisi atashinda kwa 85% maoni hayo ni kama yaliishaminishwa huko nyuma na Katibu Mkuu wa CCM kuwa mgombea wao ataweka historia ya kushinda kwa 84% hivyo utaona hiyo taasisi haijaenda kufanya utafiti kwa kukusanya maoni kwa wapiga kura isipokuwa imechukua maoni ya katibu mkuu ya kutaka kulazimisha ushindi huo wa kushindo bila kuzingatia matakwa ya wapiga kura.
Nini dhana ya utafiti, Utafiti umeelezwa kwa njia mbalimbali.
Ufafanuzi mpana wa utafiti unatolewa na Godwin Colibao "Katika maana pana zaidi ya neno, ufafanuzi wa utafiti unahusisha kukusanya mambo yoyote ya data, habari na ukweli kwa ajili ya kuendeleza ujuzi.
Ufafanuzi mwingine wa utafiti unatolewa na John W. Creshwell ambaye anasema "ni mchakato wa hatua za kukusanya na kuchambua habari ili kuongeza uelewa wetu wa mada au suala". Inajumuisha hatua tatu ili kuuliza swali, kukusanya data ili kujibu swali, na kutoa jibu la swali.
Uongo wa Utafiti wa CCM
haulezwi umechukuliwa sehemu gani mkoa gani? Haulezwi ni idadi gani ya watu wangapi na makundi gani, umri na elimu zao, jinsi zao?
Haulezi ni vigezo wametumia kufanya utafiti aina ya maswali kama ni ya wazi au lah (wasije wakawa wanauliza unaonaje MAGUFULI atashinda Urais) halafu wanauliza makada wa CCM.
Ukweli ni kuwa kabla ya utafiti kulikuwa na ramli chonganishi huo unaoitwa utafiti wa Polepole ni ramli chonganishi.
Kwa vyovyote vile uwanja ukiwa huru hakuna mgombea atakayevuka 57% ya ushindi. Ushindani wa mwaka huu ni mkubwa.
Moja Rais aliyeko madarakani huwa anachokwa hivyo lazima asilimia zishuke tena kwa Meko zitashuka sana tu. Kinachomtofautisha Meko na maraisi wengine wastaafu ni ukatili wake wa kufingia vyombo vya habari, kutoguswa na majanga makubwa ya kitaifa kama vile tetemeko la Bukoba, Watoto 32 waliofariki pale Arusha, Polisi wetu 10 waliofariki pale Kibiti, watu kupotea, kutekwa na kuteswa na upendeleo wa waziwazi kwa CHAMA chake, kabila lake na rafiki/jamaa zake wa karibu nina imani CHADEMA wangetoa tafiti NBS leo wangekifungia hicho chombo kilichofanya utafiti.
Week end njema kwa Wote.
Jumamosi njema kwa wote.