KERO Taasisi ya Elimu ya watu wazima haijalipa wawezeshaji wa mradi wa SEQUIP kwa miezi miwili mfululizo bila taarifa yoyote

KERO Taasisi ya Elimu ya watu wazima haijalipa wawezeshaji wa mradi wa SEQUIP kwa miezi miwili mfululizo bila taarifa yoyote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mradi wa SEQUIP - AEP unafadhiliwa na Benki ya Dunia na unatekelezwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI. Mradi huu unalenga kuwarudisha watoto wa kike waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kupitia elimu mbadala (Alternative Education Pathway).

Mpaka sasa umepita muda wa miezi miwili mfululizo wawezeshaji (walimu) katika mradi huu hawajalipwa stahiki zao bila taarifa yoyote. Malipo yamelipwa kwa mara ya mwisho mwezi Agosti, 2024.

Hata hivyo, tangu kuanzishwa kwa mradi huu malipo yamekuwa yakisuasua kwa malipo ya mwezi husika (yaani malipo ya mwezi wa kwanza yamekuwa yakilpwa mwezi wa pili mwishoni au wa tatu mwanzoni) hali inayopelekea walimu kufanya kazi kwa manung'uniko.

Tunaomba mamlaka husika itoe ufafanuzi juu ya malipo kwa watumishi hao kwani mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ile.
 
Back
Top Bottom