Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,566
- 4,013
Taasisi ya Mo Ibrahim imetoa kauli kali dhidi ya hatua za serikali ya Tanzania kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji kufuatia uchaguzi wa Oktoba 2025, ikionya kuwa nchi hiyo inarejea katika mwenendo wa kiimla.
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, taasisi hiyo ilieleza “wasiwasi na masikitiko makubwa” kuhusu taarifa za mauaji na kuzimwa kwa huduma za intaneti, ikieleza kuwa matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji “hayakubaliki kabisa.”
“Mheshimiwa Rais, hili halikubaliki,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo. “Baada ya utawala wa kiimla wa mtangulizi wako, Rais Magufuli, sote tulikukaribisha kama kiongozi wa mageuzi aliyesimamia demokrasia, utawala wa sheria na nafasi ya asasi za kiraia.”
Taasisi hiyo ilisema imesikitishwa na uamuzi wa serikali kupiga marufuku vyama vya upinzani kushiriki katika uchaguzi, kufunga intaneti na kutumia risasi dhidi ya waandamanaji, wengi wao wakiwa vijana. “Uchaguzi unaowatenga wapinzani si wa haki wala halali,” taarifa hiyo iliendelea, ikiongeza kuwa hasira za wananchi mitaani “zinaeleweka na zilitarajiwa.”
Ikikumbusha mkutano wake wa mwaka uliofanyika Marrakech mwezi Juni, taasisi hiyo ilirejelea onyo lake kuhusu kuongezeka kwa ukatili wa kisiasa nchini Tanzania na Uganda; nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali. Ilisisitiza kuwa amani, usalama na utawala wa sheria ni misingi muhimu kwa uwekezaji na maendeleo barani Afrika.
“Kanda hii tayari inashuhudia ukatili mkubwa na maafa ya kibinadamu nchini Sudan,” taarifa hiyo ilihitimisha. “Taifa moja lililoshindwa linatosha.”
Kauli ya taasisi hii inakuja baada ya mtetezi mkubwa wa demokrasia barani Afrika na bilionea, Dkt. Mo Ibrahim, kulaani taarifa za ukatili, ikiwemo mauaji na upigaji risasi dhidi ya raia, utekaji na kukamatwa kiholela kabla na wakati wa uchaguzi.
“Kwa nini kuua watu au kuwapiga risasi vijana? Hilo si jambo sahihi. Kama kweli unapendwa na wananchi wako, kwa nini kuchafua mchakato mzima kwa damu? Ni jambo la kusikitisha sana,” alisema Dkt. Mo.
Pia Soma: Mo Ibrahim akosoa Uchaguzi wa Tanzania: Kwanini uue, kuteka na kufunga Watu kama unapendwa kiasi cha kupata 98% ya kura