Taasisi za dini, zinazoomba zisitozwe kodi ni wezi, Serikali msikubali kwa hilo

😂😂😂
Ingawa mie ni Mkristo, sijawahi kukutana na scenario ya hivi, yaani hiyo fomu ya kujaza!!!
Seems hawa wapo kibiashara hasa!
Ni vzr tusitumie mienendo ya taasisi moja kuhukumu zingine zoote..
Ni dhehebu gani hili?
 
Kwani hizo huduma unazosema zinatolewa bure?
Kwa miaka hii kwenda mbele hizo huduma si kipaumbele tena kwa tumeambiwa serikali imejenga zahanati na hospitali za Wilaya za kutosha. Wanatakiwa walipe kodi
 
Uko sahihi kabisa,Yesu alifukuza wafanyabiashara hekaluni akapindua meza zao akawambia nyumba yangu itaitwa nyumba ya Sara,Leo wafanyabiashara madhabauni wamerudi Kwa kasi Sana,Wanauza mafuta ya upako,maji ya upako,keki ya upako,vitambaa vya upako,chumvi za upako,wengi ni mabilionea wakubwa hawana biashara yeyote yenye TIN no hawalipi Kodi hawana faida Kwa Taifa.
 
Zitajiendeshaje kama hazi charge garama walau ndogo ili ukijumlisha na kodi isiyolipwa ziweze kuendelea kutoa huduma

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Punguani ni wewe! Hujui kuwa mtu au taasisi yeyote ikitoza hata shillingi kwa mintarafu ya kutoa huduma zake, kutozwa Kodi hakukwepeki! Shule si wazazi wanalipa Ada? Kama wanalipa, Kodi ni halali kulipa.
Shule za seminari(za kiislamu na kikristu ) zaman zilikuwa hazitozi ada

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Nimewapata ila inatia hasira watu wanatumalizia mb kwa makusudi bila kutumia ubongo

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
Changamoto Ni kawaida mkuu hapa duniani Jambo la muhimu Ni kuchagua njia iliyobora yakukabiliana na kila aina ya changamoto inayokukabali hasa isiyo vunja utu wa mtu yoyote hio ndio njia bora👍
 
1. Sababu halisi za taasisi za kidini kutolipa kodi ni zipi?

2. Je, kwa kutotoza kodi taasisi hizo serikali imelenga kulipa fadhila au kuhakikisha huduma za kijamii zinazotolewa na taasisi hizo zinatolewa kwa gharama ambazo mwananchi wa kawaida anaweza kuzimudu?

3. Ni nini kinachopelekea ada kubwa mno kwenye shule za madhehebu ya dini kiasi kwamba asilimia kubwa ya WAMILIKI WAKE HALALI (waumini wa kawaida) hawamudu kusomwsha watoto wao huko?

4. Ni upi mchango halisi wa madhehebu haya kwa jamii inayowazunguka? Au ndio kusema mchqngo wao unaishia kuhubiri madhabahuni pekee?

5. Fanya ulinganifu kati ya shule bimafsi na shule za kidini, kwq nini shule nyingi binafsi zina ada za chini ukilinganisha na hizi za kidini zenye msamaha wa kodi na nyingine zina staff ambao sio watu wa msharaha?
 
justification yake ndo hiyo tu basi mpaka ukaruka na suluhisho la taasisi kutozwa kodi?afterall hata hako kajifomu katakuwa ni feki tu hata hakana nyama.ungeenda mbali zaidi na kutoa mifano kadha kwa kadha labda tungeona hoja yako lkn kwa hicho kijifomu tu bado sishawishiki kuunga mkono hoja yako.
 
si lazima kutoa zaka bali ni takwa la kiimani na kama wewe si mwumini na huna imanihulazimishi kutoa baki kama ulivyo.ya kaisali mwachie kaisali na ya Mungu mwachie Mungu hivyo ni juu yako kusuka au kunyoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…