chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Sherehe za Uhuru na Sasa mapinduzi, zinaadhimishwa kwa kupanda miti/kufanya usafi. Nadhani uadhimishaji wa sherehe hizi uwe na mlengo wa kiuchumi. Yawepo mawasilisho ya kiuchumi kwa lengo la kusogeza nchi mbele. Maazimisho ya magwaride yanaweza kuwepo, lakini test ya kiuchumi ni muhimu.
Nilidhani ni kipindi ambacho tungekuwa na mijadala ya kisomi kuhusu malengo ya nchi wakati tunapata Uhuru, njia tuliyopita, usahihi wake, tulipo na tunakoenda.
Mijadala hii husaidia jamii kuelewa masuala yanmuhimu, na Serikali pia kuwa na fursa ya kuwaeleza jamii nini hasa inafanya, imefanya, tunaelekea wapi, sera za nchi katika masuala mbalimbali.
Sidhani kama tunazitendea haki sherehe hizi kwa kufagia, kufagia au kufanya usafi ni jambo tunalofanya Kila siku, na halitupi tafakari, hata kupanda miti.
Kama tunakuwa hatuna hafla rasmi, basi tuangalie namna ingine ya kufanya.
Ni kipindi ambacho tungejadili mikakati ya Uhuru wa kiuchumi, kwa kuwa wazee wetu walishaleta Uhuru wa bendera. Sasa haiwezekani tukajadili Uhuru wa kiuchumi kwa kufagia na kupanda miti.
Mawaziri wapo, wangekuja na mada zao, wasomi, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wakutane mahala pamoja, wajadili, na wafanyie kazi waliyojadili baada ya kuazimia, na wawe na time line.
Kizazi (generation) ya wasomi wa enzi ya Shivji nadhani imekwisha, na si rahisi kuipata tena
Kila mtu amekaa kimtego akisibiri uteuzi