Taasisi za elimu ya juu nazo zinasuburi mihadhara ya kisomi iruhusiwe? Sherehe muhimu Uhuru/mapinduzi ilifaa kuwa na mijadala ya kisomi.

Taasisi za elimu ya juu nazo zinasuburi mihadhara ya kisomi iruhusiwe? Sherehe muhimu Uhuru/mapinduzi ilifaa kuwa na mijadala ya kisomi.

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Sherehe za Uhuru na Sasa mapinduzi, zinaadhimishwa kwa kupanda miti/kufanya usafi. Nadhani uadhimishaji wa sherehe hizi uwe na mlengo wa kiuchumi. Yawepo mawasilisho ya kiuchumi kwa lengo la kusogeza nchi mbele. Maazimisho ya magwaride yanaweza kuwepo, lakini test ya kiuchumi ni muhimu.

Nilidhani ni kipindi ambacho tungekuwa na mijadala ya kisomi kuhusu malengo ya nchi wakati tunapata Uhuru, njia tuliyopita, usahihi wake, tulipo na tunakoenda.

Mijadala hii husaidia jamii kuelewa masuala yanmuhimu, na Serikali pia kuwa na fursa ya kuwaeleza jamii nini hasa inafanya, imefanya, tunaelekea wapi, sera za nchi katika masuala mbalimbali.

Sidhani kama tunazitendea haki sherehe hizi kwa kufagia, kufagia au kufanya usafi ni jambo tunalofanya Kila siku, na halitupi tafakari, hata kupanda miti.

Kama tunakuwa hatuna hafla rasmi, basi tuangalie namna ingine ya kufanya.

Ni kipindi ambacho tungejadili mikakati ya Uhuru wa kiuchumi, kwa kuwa wazee wetu walishaleta Uhuru wa bendera. Sasa haiwezekani tukajadili Uhuru wa kiuchumi kwa kufagia na kupanda miti.
Mawaziri wapo, wangekuja na mada zao, wasomi, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wakutane mahala pamoja, wajadili, na wafanyie kazi waliyojadili baada ya kuazimia, na wawe na time line.

Kizazi (generation) ya wasomi wa enzi ya Shivji nadhani imekwisha, na si rahisi kuipata tena

Kila mtu amekaa kimtego akisibiri uteuzi
 
Umeongea point tupu mkuu, wasomi wa siki hizi sherehe kama hizi kwa kuwa hawaendi kazini; ratiba zao zipo hivi,akiamka Leo ni kwenda kupata supu ya samaki au kuku, hapo atashushia na bia 2 baridi baada ya hapo ataenda kubeti/ mkeka na baada ya hapo kucheza pool table la kamali.

Baada ya hapo kukutana na bint Chaurembo kula mzigo na jioni ni bia mwanzo mwisho. Jumatatu kuchukua Salary advance na kufukuzia Dili za seminer.

Kizazi hiki hata kuongea anything against gov wanaogopa,wanaamini ni kosa sana. Uhuru wa Maoni umewapata wasioutaka. Tunahitaji tu rehema za Mungu. Ngoja nikapate mtori mie
 
Sherehe za Uhuru na Sasa mapinduzi, zinaadhimishwa kwa kupanda miti/kufanya usafi. Nadhani uadhimishaji wa sherehe hizi uwe na mlengo wa kiuchumi. Yawepo mawasilisho ya kiuchumi kwa lengo la kusogeza nchi mbele. Maazimisho ya magwaride yanaweza kuwepo...
UDASA hii ya Kina Dkt Clesensia Shule utegemeee fikra mpya. Wamebaki na agenda za usagaji na haki za Wanawake. Mijadala ilishaenda na watu huru kina Bashiru, Baregu, Jingu na Kitila Mkumbo
 
UDASA hii ya Kina Dkt Clesensia Shule utegemeee fikra mpya. Wamebaki na agenda za usagaji na haki za Wanawake. Mijadala ilishaenda na watu huru kina Bashiru, Baregu, Jingu na Kitila Mkumbo
Hahahaa, usagaji hahaha, kwa kweli
 
Back
Top Bottom