Taasisi za kushughulika na bidhaa feki zinakula rushwa au haziwezi kazi? Kuna bidhaa feki nyingi Mtaani na expired zinauzwa kwa uhuru bila hofu

Taasisi za kushughulika na bidhaa feki zinakula rushwa au haziwezi kazi? Kuna bidhaa feki nyingi Mtaani na expired zinauzwa kwa uhuru bila hofu

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
1729538381621.png

1729538435054.png

1729538490972.png

Yani hakuna kash kash za kukamata wauzaji wa bidhaa feki, viwanda bubu vina operate kwa uhuru.

Taasisi za kupambana na bidhaa feki ni kama hazipo, Je ni Rushwa ? Hawawezi kazi ??

Na kuna michezo mipya imeanza bidhaa zilizoharibika zinazotupwa dampo zinarudi mtaani, mchele ulio expire na kumwagwa unapepetwa upya, samaki waliooza wanarudi mtaani, n.k.

rerences: biashara hizi zina mtandao, magodauni, faida kubwa, n.k. kama hazijatokomezwa bado zinaendelea.

Tahadhari: Samaki walioharibika waingizwa nchini kinyemela na kuuzwa soko la feri..!!

DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

DOKEZO Mpangaji wangu kageuza Nyumba yangu kuwa kiwanda bubu cha kutengeneza vinywaji vikali feki kama Konyagi, K Vant nk

Wawili mbaroni Iringa kwa wakidaiwa kusafirisha maboksi 56 ya vipodozi feki
 
nao wanaofumbia macho hutumia bidhaa hizo bila kujua
 
Babu subiri kwanza kwa hio na hapo uneweka Samaki inamaana hao Samaki ni feki au mimi ndio sijaelewa huku Matombo maana watu wa huku hatuelewi mada km hizi kwa hio hapo hao Samaki feki?
Yani hakuna kash kash za kukamata wauzaji wa bidhaa feki, viwanda bubu vina operate kwa uhuru.
 
Na kuna michezo mipya imeanza bidhaa zilizoharibika zinazotupwa dampo zinarudi mtaani, mchele ulio expire na kumwagwa unapepetwa upya, samaki waliooza wanarudi mtaani, n.k.
Tolea ufafanuzi hili suala kuna maripota wengi humu sio unaliongelea juu hapo kwenye Samaki ni feki au namna gani?
 
Wanakula rushwa na hivyo hawawezi kutimiza wajibu wao. Kwa upande wa usalama wa vyakula tunavyokula, hali ni mbaya sana, uzuri madhara yake ni ya taratibu. Miaka kadhaa mbele magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yanakwenda kuwa janga la kitaifa, na kwa huduma zetu duni za afya, umaskini utajikita kwelikweli. Mwamposa et al., wataendelea sana kula hela zetu
 
Na wewe hakuna unachosaidia. Kusema kuna bidhaa feki bila kuonesha bidhaa gani, ipi iko kwenye mzunguko na ime expire n.k ni bure
 
Wanakula rushwa na hivyo hawawezi kutimiza wajibu wao. Kwa upande wa usalama wa vyakula tunavyokula, hali ni mbaya sana, uzuri madhara yake ni ya taratibu. Miaka kadhaa mbele magonjwa yasiyo ya kuambukizwa yanakwenda kuwa janga la kitaifa, na kwa huduma zetu duni za afya, umaskini utajikita kwelikweli. Mwamposa et al., wataendelea sana kula hela zetu
Tuliowapa dhamana ya kuhakikisha bidhaa feki haziingii sokoni wako busy wanakula kwa urefu wa kamba zao. Ni janga la kitaifa na ndio maana kumekuwa na ongezeko kubwa kwa ugonjwa wa figo.
 
Tolea ufafanuzi hili suala kuna maripota wengi humu sio unaliongelea juu hapo kwenye Samaki ni feki au namna gani?
 
Cha kusikitisha inakuwa ngumu kujua kipi feki kipi OG. Siwezi kusemea vitu vingine ila kwenye sekta ya vipodozi, dah! Ni hatari sana
 
Ili hayo yote yaweze kukomeshwa lazima kwanza tupate katiba mpya,kwa sababu unaweza ukamfungia mtu,taasisi,kampuni au kiwanda kisha ikapigwa simu moja tu kutoka juu na ukajikuta wewe mtaaluma ndo mwenye hatia na kazi pia ukafukuzwa.Kwahiyo kwa mantiki hiyo ili kulinda ugali wao ndio maana wote wako kimya sio kwamba hawaoni bali meno yao yamewekwa sponji hayaumi.
 
Back
Top Bottom