Taasisi zinazohitaji tujaze fomu za karatasi taarifa zetu nyeti za NIDA ni hatari, taarifa zinaweza Kutumika kwenye utapeli, wizi, kuomba mikopo, n.k.

Taasisi zinazohitaji tujaze fomu za karatasi taarifa zetu nyeti za NIDA ni hatari, taarifa zinaweza Kutumika kwenye utapeli, wizi, kuomba mikopo, n.k.

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Kuelekea mapinduzi ya Teknolojia, mambo mengi nchini yameanza kufanyika kwa kutumia NIDA.

Kwenye mifumo ya kusajili biashara, kuomba ajira, kuomba mikopo, kujisajili huduma za kiserikali mtandaoni, n.k. huwa unajaza Nida halafu baada ya hapo unaulizwa maswali matatu ya uhakiki mfano jina la mama, sehemu uliyozaliwa, shule uliyosoma, n.k.

Kuna shida imeanza ya baadhi ya taasisi kukupa karatasi ujaze taarifa zako nyeti za NIDA, hii ni hatari sana,

Mfano kuna benki flani kubwa tu, kuna baadhi ya shida ukiwa nazo wanakwambia ujaze hii fomu ya uhakiki wa utambulisho

1740656326352.png


Nilivyopewa hii fomu nilishangaa sana,

  • wakati nafungua account walishanihakiki nilipowapa nida namba na kuweka alama za vidole na kunipiga picha, kwanini nijaze taarifa nyeti za NIDA kwenye karatasi nje ya mfumo wa NIDA ?
  • Sheria gani inawapa nguvu hii ?
  • iweje nihakiki taarifa zangu za NIDA kwenye fomu badala ya kutumia alama za vidole ?
  • kuna hatua zipi za kulinda karatasi, kwamba linazagaa zagaa tu kama rough paper ?
  • kwanini fomu haina maelezo ya uwajibikaji wa taarifa ?

SIKUJAZA HATA SWALI MOJA

Baada ya kuzozana bila mafanikio nikajiapiza sijazi chochote ni bora nifungue account mpya tu ntahamishia fedha zote account mpya, nilipoenda tawi lingine nao walihitaji lakini walikuwa waelewa nikahudumiwa

Uhshauri wangu kuhakiki taarifa za NIDA vitumike vidole tu, kama kuna haja ya taarifa za ziada mteja aziiingize mwenye kwa usiri
 
Back
Top Bottom