Shujaa Nduna
JF-Expert Member
- Sep 8, 2022
- 599
- 487
Mliyo na dhamana ya kusimamia vitengo serikali kwanini mnalea uzembe,uwizi wa watumizi wenzenu?Mara nyingi unakuta mtumishi anafika oficini anasaini halafu anafanya kazi kidogo anaenda mtaani kuzurula au kwenye mishe binafsi ndiyo mana nasema uzembe,uwizi mana analipwa na mshahara ambao mi mkulima nimekamuliwa kodi wakati hamalizi muda wa kuwa ofisini,kuna mtendaji hapa mtaani anafanya kazi kijiji jirani lakini sasa wiki ya pili hajaenda ofisini alikoajiriwa wala hayupo likizo huyu mtu ni mtendaji wa mtaa ni mwajiriwa,yani kila siku yupo kwenye ofisi yake ya kushona.Tabia hii hujirudia mara kwa mara na mshahara anapata.Mtu huyu na wengine wa aina yake wezi,wazembe.Natowa wito wawajibishe wazembe kama hawa.Sheria ya ajira iwekwe msisitizo kuwa mtumishi ukikaa home siku kadha hujaenda job kazi huna tena ikibidi hakuna kubaki nyumbani hadi likizo,homa na dharula muhimu tena kwa maandishi.Tofauti na hapo kata mshahara au fukuza.Mbona sionagi mwalimu akakaa nyumbani bila kwenda kazini hata siku mbili bila sababu?