Tabia hizi za jamii kwa mtoto mdogo(mchanga) zinaleta sintofahamu

Tabia hizi za jamii kwa mtoto mdogo(mchanga) zinaleta sintofahamu

Adolph Jr

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
5,950
Reaction score
9,511
Wasalaam...!

Ni muda mwingine tena natoka kwenye majukumu yangu ya siku na kuingia nyumbani ila mwanamke ananipokea na kunitaarifu kuwa kuna mgeni, rafiki yangu wa zamani kapita kunijulia hali,basi napitia sebuleni...

ile kufika sebuleni namuona rafiki yangu kambeba mtoto wangu na kaingiza mdomo wake kwenye shingo ya mtoto na anakua kama anaitekenya kwa mdomo basi mtoto anachekelea....😅😅

Basi bwana nikampatia hi! Rafiki tukaanza stories za muda mrefu huko nyuma, na kusimliana matukio ya huko nyuma tulipokuwa tunazisaka....

Wakati tukiendelea na story mara amshike mtoto na kumrusha juu sana na kumdaka,mtoto anakuwa kama vile anakakamaa kwa kuwa na hofu ya kudondoka 😟😟😟....

Basi yeye anacheka na kusema "Huyu mtoto wako ni mwoga sana"......mimi najibu kwa tabasamu tu na kuendelea na story.....

Haipiti muda anambeba na kumuelekea yaani uso wake unaangaliana na mtoto huku akiwa amegusanisha paji lake la uso na paji la uso la mtoto huku akisema "Aji.jiji.jiji..iiii......!....Iyoooooooooh...mambo toto..? Anamaliza anampiga busu kwenye paji la uso.....

Daaaah...!..kwa kweli mimi nabaki natabasamu tu ila sikupendezwa na matukio hayo maana mpaka anaondoka mtoto amelowa mate yake (ni watu wanaoongea kwa nguvu kubwa na mate yanaruka).

Sijapendezwa na hii tabia sijui kwa wenzangu labda ni wivu wangu tu...

Hebu tushauriane kuhusu hizi tabia

inaendelea......
download-4.jpg
 
...Tabia hizi pia huwa zinanitatiza..

1: Wakati umembeba mtoto wa rafiki yako kumpatia vidole vyako anyonye...
2:Kumbusu shingoni wakati unauadui na mswaki
images-5.jpg
 
Siyo kwamba kumbeba mtoto wa rafiki yako ni vibaya, au kumbusu kichwani,

Kuna busu zingine siyo hatarishi na wala mtoto hatokuwa kwenye hatari ya kupata vimelea vya magonjwa (hasa kipindi hiki cha magonjwa ya maambukizo ya mfumo wa hewa mfano mafua na kikohozi na homa ya mapafu) au kudhurika mfano hii (niwazavyo)
images-6.jpg
 
mimi mtu akija kuniona kama ana mafua siwezi mpa mtoto amshike na hua namwambia utaniambukizia mtoto bana ngoja upone uje ucheze naye sio siri mafua kwa mtoto yanatesa

kingine ni kumbusu mtoto mdomoni yan mnagusanisha midomo ya mtu mzima namtoto kumpa tu bakteria sipendi hili
 
mimi mtu akija kuniona kama ana mafua siwezi mpa mtoto amshike na hua namwambia utaniambukizia mtoto bana ngoja upone uje ucheze naye sio siri mafua kwa mtoto yanatesa

kingine ni kumbusu mtoto mdomoni yan mnagusanisha midomo ya mtu mzima namtoto kumpa tu bakteria sipendi hili
Daah mimi inanipatia ugumu nahisi ataniona namfukuza hivyo huwa namezea tu...

Ila imeisha nigharimu kuna kipindi rafiki mmoja alikuja na mafua yake haikupita muda mtoto kaugua mafua makali hadi kushindwa kupumua anapumulia mdomo tu yaani nilikasirika hatari ila hakujua....nimeamua kumuambia mwanamke awe anakaa na mtoto muda wote


Ila wageni walivyo vin'gan'ganizi utasikia "totoooo njoo nikubebe".....aiseee
 
Daah mimi inanipatia ugumu nahisi ataniona namfukuza hivyo huwa namezea tu
mkuu mtoto akiumwa mafua anateseka yan kama ananyonya hanyonyi vizuri kabisa unaweza kukesha pia sasa niteseke nimezee kisa jitu limekuja na mafua au kajipulizia mipafyum kama yote ya nn kunitesea mtoto
 
mkuu mtoto akiumwa mafua anateseka yan kama ananyonya hanyonyi vizuri kabisa unaweza kukesha pia sasa niteseke nimezee kisa jitu limekuja na mafua au kajipulizia mipafyum kama yote ya nn kunitesea mtoto
Yaani hadi mke wangu akawa anafanya kuyavuta kwa mdomo pia kukanda pua kwa maji vuguvugu yaliyotiwa viksi hebu fikiria aisee
 
utafanyeje ndio waswahili wa ccm tulivyo
 
Nimesoma nikisubiria.. useme labda ndio baba yake.. nikakuta hujayaandika..

Napita..
 
Back
Top Bottom