Tabia ya CCM kutaka kuua upinza wa vyama vingi ndiyo itakuwa kifo chake

Tabia ya CCM kutaka kuua upinza wa vyama vingi ndiyo itakuwa kifo chake

Ti Go

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
1,062
Reaction score
1,088
Tuliwambia siku nyingi kuwa tabia ya CCM kutaka kuua upinzani ndiyo itakuwa chanzo cha kifo chake. Duniani mpaka mbinguni upinzani ni muhimu. Ndiyo maana hata Mungu alimuacha shetani aendelee kuwapo kama mpinzani wake. Kwa nguvu tunayoamini anayo Mungu alikuwa na uwezo wa kumaliza shetani.

Haiwezekani nchi yenye watu milioni 60, wote tukawa na mawazo yanayofanana. Lazima tuwe na mawazo mbadala na tuyavumilie. Lazima tutoe uhuru wa kila mtu kutoa mawazo yake na tuyavumilie.

Msingi wa kukubali vyama vingi ilikuwa kuwa na mawazo/utawala mbadala.

CCM tuliwambia acheni vyama vya upinzani vifanye siasa. Kama hoja zao zitapendwa na watu, basi tukae pembeni tujipange. Tukubali kushindwa. Tusiporuhisu upinzani wa nje, tutapambana na upinzani wa ndani. Upinzani wa ndani ni mbaya kuliko wa nje.

Mpinzani wa nje ni rahisi kupambana naye. Ni vigumu kupambana na mpinzani wa ndani. Kwa sababu anakujua kila Kona, anakujua ndani na nje.

Tukiangalia kinachofanywa na Polepole ni upinzani wa ndani. Na bado tutasikia mengi.

Tuvumilie kwa sababu tuliyataka wenyewe.
 
Back
Top Bottom