Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AISEEChisano embu kunywa chai Kwanza
Sio kweli!
Kulalamika kunasaidia nini sasa!? Ndio hizo gharama za maisha zitashuka!? Kama gharama za maisha zimepanda Tanzania, si uhamie huko ambako hazijapanda!? Hapa Tanzania na popote pale duniani hakuna atakayebadilisha/Rekebisha mambo/Hali yakufaidishe eti kwa sababu tu umelalamika.Dunia ikiwa na watu wa aina yako basi haitakalika kwa Sababu watu watauishi kama wanyama Mana itakua inaongozwa bila sheria, .Kulalamika ni kawaida Kwa mfano Sasa hivi Tanzania gharama za maisha zimepanda hivo basi lazima watu walalamike ili hiyo hali ilekebishwe.Tatizo unaujuaju mwingi kufikili Kila kitu unakijua na unaweza kukitolea ushauri kitu ambacho sio sahahi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tumia akili yako vizuri usijibu kwa kukulupuka , Kulalamika sio vibaya kwa Sababu ni kutokana na Kulalamika ndipo mambo hubadilishwa na serikali ,hata Jana Jaji Warioba alalamika kuhusu mambo ya uchaguzi wa 2020 vipi na yeye ni Lofa?Acheni ujuaji wa kijinga kujifanya mnajua Kila kituKulalamika kunasaidia nini sasa!? Ndio hizo gharama za maisha zitashuka!? Kama gharama za maisha zimepanda Tanzania, si uhamie huko ambako hazijapanda!? Hapa Tanzania na popote pale duniani hakuna atakayebadilisha/Rekebisha mambo/Hali yakufaidishe eti kwa sababu tu umelalamika.
Umeamua/Ukiamua kuishi kibinaadamu tambua kuna walioamua kuishi kinyama. Usishangae wala kulalamika pale wewe umewafanyia ubinaadamu wao wakakulipa unyama. Ndivyo ulivyochagua.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
1. Unaandika hovyoTumia akili yako vizuri usijibu kwa kukulupuka , Kulalamika sio vibaya kwa Sababu ni kutokana na Kulalamika ndipo mambo hubadilishwa na serikali ,hata Jana Jaji Warioba alalamika kuhusu mambo ya uchaguzi wa 2020 vipi na yeye ni Lofa?Acheni ujuaji wa kijinga kujifanya mnajua Kila kitu
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu. Watu tunapenda Sana kulalamika.Ukiumizwa tafuta namna ya kujitetea,
Akuumizaye muumize, kanuni rahisi itakayosaidia sio wewe tuu Bali hata kizazi chako, jamii na taifa.
Kulalamika hakujawahi kumsaidia Yeyote, hata wazazi wetu walikuwa ni watu wa kulalamika wakatuleta Sisi kuna lolote la maana
Watu wenye mitazamo Kama yako ndo wazuri kwa kuchukulia vitu kirahisi endeleeni hivyo hivyo....Kulalamika kunasaidia nini sasa!? Ndio hizo gharama za maisha zitashuka!? Kama gharama za maisha zimepanda Tanzania, si uhamie huko ambako hazijapanda!? Hapa Tanzania na popote pale duniani hakuna atakayebadilisha/Rekebisha mambo/Hali yakufaidishe eti kwa sababu tu umelalamika.
Umeamua/Ukiamua kuishi kibinaadamu tambua kuna walioamua kuishi kinyama. Usishangae wala kulalamika pale wewe umewafanyia ubinaadamu wao wakakulipa unyama. Ndivyo ulivyochagua.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Ndo maana ukiambiwa wewe kiazi unalalamika!!!
🤣🤣🤣🤣Msimuudhi mleta mada hapendi malalamiko
Lazima utuone malofa maana hujui hata petrol tunanunua buku 3 we si unalala kwa shemeji sebleni Kama baiskel
ila siku shemej yako akikunyima msosi aanze kukulisha mlo mmoja Kama mbwa usiende kijijin kulalamika kuwa anaroho mbaya
Petrol elfu tatu unalia Lia Nini wakati gari ulinunua million 5 una akili wewe,Lazima utuone malofa maana hujui hata petrol tunanunua buku 3 we si unalala kwa shemeji sebleni Kama baiskel
ila siku shemej yako akikunyima msosi aanze kukulisha mlo mmoja Kama mbwa usiende kijijin kulalamika kuwa anaroho mbaya
Ni jinsi gani huna akili? Ni nan kakwambia Mimi Nina gari? Kwahiyo wewe ukiskia mfumuko wa bei ya bidhaa ya mafuta kwakua wewe unaendesha baiskel mkangafu unafikiri athari haiwezi kukupata?Petrol elfu tatu unalia Lia Nini wakati gari ulinunua million 5 una akili wewe,
Acha kulia Lia kama Vipi uza gari upande daladala,
Umaskini Mbaya Mtu mwenye V8 lake hawezi lalamika kuuziwa mafuta Bei Hiyo ila wenye Passo na ISt Ndio mnaongoza kulia Lia,
Anyway
Sina nyumba Wala gari ila hua sipendi kulia lia kinyonge!
Shabhash!
Usipanic mangi tafuta Hela Acha kulia Lia haitakusaidia bidhaa zikipanda bei Wewe pandisha mizuka ya kusaka Pesa upate kwenda na beat,Ni jinsi gani huna akili? Ni nan kakwambia Mimi Nina gari? Kwahiyo wewe ukiskia mfumuko wa bei ya bidhaa ya mafuta kwakua wewe unaendesha baiskel mkangafu unafikiri athari haiwezi kukupata?
Unaonekana kichwan umejaza uji wa pilipili manga tu hamna kitu
mhn! kwa kadri ya kicwa cha habari ni kweli lakini pamoja sikuweza kuisoma yote kwa mistari michache niliyosoma na mada kuwa ndefu kiasi hiki ni kwamba na wewe ni mlalamishi tu!Heshima kwenu Wakuu!
Hakuna tabia inakera Kama mtu kulalamika, sasa unalalamika nini, yaani upuuzi tuu!
Kulalamika ni tabia walizonazo wazembe na malofa, kila kitu kulalamika, kila kitu kunung'unika, upuuzi mtupu!
Oooh! Wanasiasa wanapiga Sana hela, Kwa nini nawe usijiingize Huko kwenye siasa? Nani kakukataza?
Nani alikuambia kuna mtu hapa Duniani yupo kwaajili yako kama sio akili yako ya kilofa unayoiendekeza!
Ooh! Wafanyabiashara wanaiba, sijui wanaloga, mara sijui wanahujumu uchumi, Nani kakukataza kuwa mfanyabiashara? Kuwa nawe mfanyabiashara ili uwe na maisha Kama mfanyabiashara. Unalalama Kama Mpumbavu Mpumbavu tuu! Alafu unafikiri utaonewa huruma! Hakuna mtu mwenye akili atakayekuonea huruma Kwa ulofa wako.
Oooh! Nalipwa Mshahara kidunchu, sijui wananinyonya, pumbavu! Ulilazimishwa? Nani kakulazimisha, Acha kazi, ili ufanye vile utakavyo na sio kupangia watu na ulofa wako.
Watu wanaolalamika wanapenda Sana kupangia watu wengine chakufanya, upuuzi tuu!
Oooh! Wanawake wanapenda pesa! Sijui blah! Blah! Sasa si utafute pesa kama unawapenda HAO wanawake, Kama huwezi kutafuta pesa temana nao, fanya mambo mengine, sio kulalamika hapa Kama mpuuzi!
Ulifikiri ukiwalalamikia wanawake watakuona huruma, hakuna Duniani na mbinguni ama mahali popote wanapoonea huruma malofa.
Oooh! Sijui Utawala huu haufai, blah! Blah! Kama haufai si muuondoe? Andamaneni, sio kulia Lia Kama watoto wapumbavu! Watu wenye akili zao, mataifa yaliyoendelea yakigundua Utawala uliopo haueleweki wanautoa madarakani kivyovyote, iwe Kwa Amani au kwa vurugu. Na sio kulalamika Kama malofa au wazembe Fulani.
Oooh! Wanaume wanatutelekezea watoto, sijui hawalei watoto wala kutoa matunzo ya watoto, pumbavu! Si ulee mwenyewe! Hakuna aliyekutuma kuzaa na Masikini ukijua wazi Hana kazi, au kipato chake hakiridhishi, mtu yeyote anayelalamika ubaya ulianzia kwake.
Unalalamika nini sasa ikiwa Kama sio wewe mambo yote yasingetokea.
Mkiambiwa msubiri ndoa hamtaki, mnajifanya nanyi mnatamaa Kama wanaume, mbaya zaidi mnashindwa hata kuchagua mwanaume wa ku-date naye. KAZI kuchagua mashalobaro na Handsome boy, wale wachapakazi wenye Sura ngumu mnawatenga, alafu mkishapata madhara mnalalamika.
Oooh! Ananichukulia mke au mume wangu, ukilalamika haitasaidia kitu. Hii dunia inatumia kanuni ya jino Kwa jino. Apandacho mtu ndicho umpe mavuno yake.
Usijitie mnyonge, usipende kujiona lofalofa, dhaifu wa kuonewa huruma, Duniani hakuna kuoneana huruma. Dunia ni fight for fittest, akichukua mke, nawe chukua wake na Watoto, au nenda mbali zaidi.
Sheria Kwa sheria
Nguvu Kwa nguvu
Pesa Kwa pesa
Uchawi Kwa Uchawi
Mungu Kwa Mungu
Moto Kwa moto
Maji Kwa maji
Hakuna kurembana.
Malofa na wazembe wanaweza wasinielewe, Hilo sitajali, najua ni kawaida yao, wengine wameumbwa kuwa swala na Digidigi mbugani.
Acha kulalamika! Fuata ukitakacho, usisubiri mwingine akuletee kitu kitakachokunufaisha wewe, hakuna Jambo Hilo Duniani na peponi.
Yaani Kwa ulofa wako unakaa kabisa ati unafikiri Jambo linalokunufaisha wewe ati mwingine akuletee! Embu tumia hata akili ya kuku tuu! Hilo haliwezekaniki kamwe.
Ukiona mtu Anakuletea Jambo linalokunufaisha ujue yeye ananufaika mara Mia zaidi yako. Ukiona hanufaiki ujue huo ni mtego kwako. Au ujue tayari wewe ni marehemu wanakupeleka kukuzika, maana maiti ndio hutendewa hivyo. Tena wengine mpaka kwenye maiti hutafuta faida.
Oooh! Mungu nakuomba unipe Baraka! Mpuuzi wewe! Mungu akupe mara ngapi, kuzaliwa tuu ni baraka inayokutosha, unataka baraka gani Kama sio kumchosha Mungu na kukuona lofa.
Watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa!
Oooh! Madaktari, sijui mainjinia wanalipwa pesa nyingi, Nani alikukataza kuwa Dokta? Nani alikukataza kuwa Injinia? Nani huyo!
Unalalamika unafikiri itasaidia kitu.
Oooh! Wazungu wanatubagua, sijui waarabu na wahindi wanabagua na kututesa, na wewe watese, Nani kakuzuia! Unajua wanaolalamika wanaakili za kijinga Sana. Mtu anakubagua nawe si umbague, au ndio kutokujielewa kwako ndio kunakufanya uteswe! Acha uteseke ili utie akili!
Taikon nataka kusema nini?
Tambua nafasi yako, usipende kuwamilikisha watu wengine nafasi yako. Alafu uje kulalamika lalamika hapa.
Hata aje kuongoza Mungu hapa Duniani malofa hawataacha kulalamika,
Akizingua mtu mzingue
Akikuheshimu Mheshimu!
Akikupenda mtu mpende!
Hiyo ndio haki na kamwe hautakuwa mtu wa kulalamika lalamika Kama mjinga mjinga!
Taikon nimemaliza!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
mhn! kwa kadri ya kicwa cha habari ni kweli lakini pamoja sikuweza kuisoma yote kwa mistari michache niliyosoma na mada kuwa ndefu kiasi hiki ni kwamba na wewe ni mlalamishi tu!