Tatizo mnakera mno ,unakuta mtu namba yako anaifahamu , majina yako unayotumia anayajua yote
Bado akituma hata dk kadhaa hazijapita anauliza umepata? Agrrr mnakera
Utetezi wa kitoto sana huu.
Kwa mantiki hii unaweza kupoteza fedha nyingi sana kwa uzembe, nakusimulia kisa kimoja utajifunza umuhimu wa kumjulisha mtumaji kwamba pesa imefika.
Siku moja nikiwa nafanya transaction ya laki 3 kwenda kwa jamaa yangu aninunulie kitu flani hapo kwa Makonda, tulisha chat WhatsApp tukakubaliana fresh, sasa wakati nataka kutuma nikampigia simu, yeye tayari yuko K/Koo anasubiri pesa iingie atoe, nikamuuliza nitume namba ipi maana ana namba nyingi na zote zimesajiliwa akanitajia.
Nikatuma, kumbe kwa bahati mbaya ile namba ilikua imepotea ina mwezi mzima na hajairudisha sasa alisahau kuniambia, nimetuma pesa nimekaa nusu saa nikampigia kujua kama ameshanunua mzigo anasema bado hajapata muamala, nikascreenshot ile msg nikatuma WhatsApp lakini kwake haijafika, sasa tumelumbana sana baada ya muda akabaini namba niliyotuma pesa ilishapotea.
Kwahiyo nikaenda Tigo pesa kushughulikia pesa irudi sikutaka kusubiri yale masaa 24 kutokana na kubanwa na shida niliyokuwa nayo.
Sasa kwa mfano ningekaa kimya je huyo jamaa angeendelea kusubiri kwa muda gani? Pamoja na kwamba jina lilitoka jina lake.
Muungwana ukitumiwa pesa toa mrejesho, maana mtu anaweza kutuma kupitia wakala sasa yuko dukani anasubiri umjibu we unakausha, na kuna wakati mwingine miamala huwa inafeli sasa kutoa mrejesho ni muhimu. Hicho ni kitendo cha uungwana tu
Sent using
Jamii Forums mobile app