Tabia ya kuomba hela halafu ukishatumiwa husemi imefika au kutoa shukrani sio nzuri

Tabia ya kuomba hela halafu ukishatumiwa husemi imefika au kutoa shukrani sio nzuri

[emoji16][emoji3][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]hana vocha ya kupiga kutoa shukran ?? [emoji16][emoji16][emoji16] ila vocha ya kuomba pesa atumiw anayo [emoji16][emoji3][emoji16][emoji16]
Binafsi naelewa wew ulieyemtumia ndo unatakiwa kupiga simu kuulizia kama muamala umemfikia sababu unaweza kujaa povu kumbe text haijamfikia au hana hata hiyo vocha ya kukupigia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo mnakera mno ,unakuta mtu namba yako anaifahamu , majina yako unayotumia anayajua yote
Bado akituma hata dk kadhaa hazijapita anauliza umepata? Agrrr mnakera
Aliongea mpoki kwamba wanaume waache kuuliza uliza Kama hela imefika,
Kwani hawaoni msg ya muamala?
Eti wanauliza maswali mengi kuliko hata hela yenyewe waliyotuma[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utetezi wa kitoto sana huu.

Kwa mantiki hii unaweza kupoteza fedha nyingi sana kwa uzembe, nakusimulia kisa kimoja utajifunza umuhimu wa kumjulisha mtumaji kwamba pesa imefika.

Siku moja nikiwa nafanya transaction ya laki 3 kwenda kwa jamaa yangu aninunulie kitu flani hapo kwa Makonda, tulisha chat WhatsApp tukakubaliana fresh, sasa wakati nataka kutuma nikampigia simu, yeye tayari yuko K/Koo anasubiri pesa iingie atoe, nikamuuliza nitume namba ipi maana ana namba nyingi na zote zimesajiliwa akanitajia.
Nikatuma, kumbe kwa bahati mbaya ile namba ilikua imepotea ina mwezi mzima na hajairudisha sasa alisahau kuniambia, nimetuma pesa nimekaa nusu saa nikampigia kujua kama ameshanunua mzigo anasema bado hajapata muamala, nikascreenshot ile msg nikatuma WhatsApp lakini kwake haijafika, sasa tumelumbana sana baada ya muda akabaini namba niliyotuma pesa ilishapotea.

Kwahiyo nikaenda Tigo pesa kushughulikia pesa irudi sikutaka kusubiri yale masaa 24 kutokana na kubanwa na shida niliyokuwa nayo.
Sasa kwa mfano ningekaa kimya je huyo jamaa angeendelea kusubiri kwa muda gani? Pamoja na kwamba jina lilitoka jina lake.

Muungwana ukitumiwa pesa toa mrejesho, maana mtu anaweza kutuma kupitia wakala sasa yuko dukani anasubiri umjibu we unakausha, na kuna wakati mwingine miamala huwa inafeli sasa kutoa mrejesho ni muhimu. Hicho ni kitendo cha uungwana tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hujanielewa ama sijaeleweka vzr nilichomaanisha wewe ukishatuma huna haja yakunipigia wajibu wa kupiga na kushukuru unapaki kwangu
Na ndio maana nikasema subiri lwa dk kadhaa mimi nikupe mrejesho
Yaani mtu anikinipigia kuuliza jambo hilo nahisi kama sitambui wajibu wangu
 
Usijiweke kwenye kundi la kutumiwa tu

Wewe fikiria umemtumia mtu pesa anyamaze asitoe taarfa utajisikiaje?
Mkuu mimi nikimtumia mtu na nikiwa na uhakika wa muamala , sishughuliki nae tena
Kwa sababu najua kwa muda wake akiiona atanijulisha
 
Tatizo mnakera mno ,unakuta mtu namba yako anaifahamu , majina yako unayotumia anayajua yote
Bado akituma hata dk kadhaa hazijapita anauliza umepata? Agrrr mnakera
Unakula pozi kutuma ka message kwamba umepata?
Wakati unaomba, inatuma mimeseji hadi kero. Mara salamu, mara umekula na upuuzi wote wa Dunia hii. Ukishapata unakula pozi kwanza.
 
Kausha wala usiulize.

Next time akiomba tena muulize kama zile za mwanzo zilifika.

Kutosema kunaweza kumaanisha mambo kadhaa. Hana mpango na wewe Ila hela yako. Wewe ni ATM tu.

Labda kuna sehemu naye anatuma kwanza.

Labda kaona umetuma kiasi kidogo ingawa yeye hana hata nauli ya daladala.
 
Mkuu mimi nikimtumia mtu na nikiwa na uhakika wa muamala , sishughuliki nae tena
Kwa sababu najua kwa muda wake akiiona atanijulisha
Mimi hata nikituma hela kupitia kwa wakala,nitaangalia message palepale kwa wakala Kama imefika.
Wala sijipi kazi kuanza kumuuliza niliyemtumia Kama amepata au hajapata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unakula pozi kutuma ka message kwamba umepata?
Wakati unaomba, inatuma mimeseji hadi kero. Mara salamu, mara umekula na upuuzi wote wa Dunia hii. Ukishapata unakula pozi kwanza.
Pole sana mkuu, halafu sio kila pesa inaombwa wengine hutuma kama wajibu
 
Mimi hata nikituma hela kupitia kwa wakala,nitaangalia message palepale kwa wakala Kama imefika.
Wala sijipi kazi kuanza kumuuliza niliyemtumia Kama amepata au hajapata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida hawaelewi kwamba ukishatuma basi kazi yako imeisha. Kuuliza ni kama kufosi vitu .
Mimi kwangu sijipi presha hiyo ya kuuliza
 
Back
Top Bottom