Tabia ya kuomba hela halafu ukishatumiwa husemi imefika au kutoa shukrani sio nzuri

Tabia ya kuomba hela halafu ukishatumiwa husemi imefika au kutoa shukrani sio nzuri

Issue ni kwamba unakuta tumeomba kwa watu zaidi ya mmoja na MPESA inasoma jina la wakala au siyo lako, inabidi usubiri nani huyu katuma.

Ile sms umepata, ndy unasema asante love nimepata. La sivyo unaweza kutoa asante kwa mtu mwingine. Mpango ukaharibika

Chilling.......................
Hapo unakuwa umebeti mkeka wako siyo Aidanna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo linaanzia utotoni, kuja kumrekebisha ukubwani ni tabu!!

Wengi sana wana tabia hiyo, unatuma hela wala hasemi chochote, mpaka umuulize!
 
Sijakataa , ama sio kama sioni umuhimu wa kushukuru hapana sina maana hiyo.
Lakini unavyopiga inakua kama unafosi niseme ahsante ndio kitu nachukizwa nacho
Unachukizwaje,wakati uliomba pesa Kwa masikitiko.Yaani mtu ameacha Kula vizuri,kununua nguo nzuri,kununua cement then amekutumia 50k halafu unasema amekuchosha.Mimi kama aurespond usirudie tena kunipiga mizinga,ukatafute huko wanakotoa kienyeji enyeji.Halafu watu WA namna hii hata madeni ni wagumu kulipa.
 
Wengi wenu ndio inakuwaga ntolee, shida zako zishaisha huna habari na mtumaji hela. Dawa yenu ni kuliwa buyu tu kwan shida zina mwisho sasa?Siku ukija tena jibu ni moja "SINA"

Mkuu , point yangu sio kwamba sitampa mrejesho ila sipendi kuulizwa sababu ,Nahisi mtu anasababisha nijihisi sina shukran kitu ambacho hakipo hivyo
Vizuri kusubiri mimi nikupigie
 
Tatizo linaanzia utotoni, kuja kumrekebisha ukubwani ni tabu!!

Wengi sana wana tabia hiyo, unatuma hela wala hasemi chochote, mpaka umuulize!
Nakumbuka kipindi nakuwa kama kuna neno ambalo nilikaririshwa mara nyingi ni kusema asante napopewa kitu chochote tu.

Mtu akikupa kitu sema Asante hata kiwe kidogo kiasi gani. Ni jambo la hekima sana kusema asante. Mtu ambaye hajafunzwa katika misingi ya hekima ndio ambaye atachukulia poa poa tu.
 
Kuna mtu alikuwa na tabia hii, Tena wa karibu. Nilimuweka benchi bila kumtumia kwa miaka 4' kila akiniomba namwambia sina.
 
Hizo tabia asilimia kubwa wanazo dada zetu na inakera mnoo
Unakuta anakuomba vocha ukimrushia hana habari tena na wewe ukimpigia umulize kama imefika no iko busy

Sent using Jamii Forums mobile app
Haha haya mambo haya hata hayahitaji hasira, yani unamtumia beibe vocha afu anakua busy na boya mwingine kwa vocha hiyo hiyo anashindwa hata kukuacknowledge mtumaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka kipindi nakuwa kama kuna neno ambalo nilikaririshwa mara nyingi ni kusema asante napopewa kitu chochote tu.

Mtu akikupa kitu sema Asante hata kiwe kidogo kiasi gani. Ni jambo la hekima sana kusema asante. Mtu ambaye hajafunzwa katika misingi ya hekima ndio ambaye atachukulia poa poa tu.
Hakika jamani! Haya yanaanza utotoni kabisaa, wazazi na walezi ndo tunajukumu kubwa la kuhakikisha watoto wanakuwa wanashukuru kwa kile wanachopata bila kujali ukubwa wake!

Kwa mazingira ya kawaida kabisaa, huwezi kutumiwa hela ama vocha, ukapokea na usiseme Asante nimepata!! Yaaniii malezi yanachangia kwa kisasi kikubwa!
 
Issue ni kwamba unakuta tumeomba kwa watu zaidi ya mmoja na MPESA inasoma jina la wakala au siyo lako, inabidi usubiri nani huyu katuma.

Ile sms umepata, ndy unasema asante love nimepata. La sivyo unaweza kutoa asante kwa mtu mwingine. Mpango ukaharibika

Chilling.......................
Kuna dogo mmoja alikuwa na hii tabia..
Ameomba hela sehemu tano,ikaingia miamala miwili..hajui yupi ni yupi.
Njaa hizi dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakikisha mkono wa kulia ukitoa, hata wa kushoto usijue.
Hakikisha umwambie muhusika ajue kuwa amekukwaza, sababu inawezekana sio member humu
 
Back
Top Bottom