Tabia ya kutembeza wageni kwenye nyumba mpya!

Umefundishwa jinsi ya kuwa na personal hygiene. Inaonesha wewe ni mchafu, chumba hudeki, kitanda hutandiki, miswaki unaacha bafuni😂
 
Mpaka hapo mshamba ni wewe uliyeacha chumba chako shagarabagara!
 
Hii ilinikuta kipindi napambania maisha nikiwa gheto kwa jaamaa, aisee nimekumbuka mbali miaka 10 sasa
 
Hiyo tabia wengi wanayo, Kuna jamaa yangu alijenga nyumba nzuri tu akanikaribisha, nilipofika alikua ananitembeza kila chumba na maelezo juu hadi nikawa naona aibu, nilimuona miyeyusho sana Ila kumwambia sikuweza
Wanazingua sana Kuna ndugu yangu alikuwa na hiyo tabia ya kuwatembeza rafiki zake kwenye nyumba yake mpya, mama yake akamkataza ikawa mwisho kufanya hivyo
 
Mimi nilishaweka utratibu kitambo nikisafiri nalala loji, ndugu nitawatembelea na kuondoka.

Mambo za kwenda kubanana majumbani kwa watu sitaki kusikia.
 
Jenga yako na wewe ufanye unavyotaka, au fikia hoteli.

Ukifikia kwa mtu, usimpangie cha kufanya kwenye nyumba yake.

Hapo wewe ndiye umemuingilia mtu kwenye nyumba yake, halafu unalalamika tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…