Tabia ya ovyo watu wazima kutoitikia salamu ipasavyo za wanaowazidi umri

Ila hii tabia haijaanza leo, ni ya kitambo sana, nakumbuka kipindi nipo primary kuna mzee ana mvi kabisa zimejaa kichwani ila anaonekana ni wazee wa mjini kwa mambo yake...

Kila siku nilikua napita hapo kwake kuelekea shule ilikua nikimsalimia shikamoo anajibu salama mjukuu wangu, hajawahi kuitikia marahaba hadi nikaachaga kumsalimia, nikimkuta nje kwake nampita maana nilianza kumtilia shaka.
 
Wazungu hawana Shikamoo ,wana Good morning ,After noon and Good Evening.

Shikamoo ni Utumwa -Ilitumiwa na waarabu enzi za biashara ya Utumwa.

Wewe ukikutana nao sema tu Hi au Hello au How you doin'? au Morning basiii hayo mambo ya shikamoo peleka UAE(Uarabuni).
 
Kuna mama mmoja alikuwa mtu mzima sema ana mambo ya ujana sana ... Watoto wakimsalimia anakausha na kwa upanda wa vijana kabla hujamsalimia anakuwahi kwa kuanza kukusalimia.

Mungu si mchoyo binti yake akabeba ujauzito na sasa ana mtoto anaitwa Bibi .. Yale madoido yote kapuni na sasa analea mjukuu baada ya mtoto kumtelekeza mtoto.

Salamu na heshima haiombwa wala kulazimishwa bali ni kipimo cha utu.
 
mimi nasemaga 'shkaoo' ya chapu chapu ukijisumbua kuitika shauri yako nishafika mita 100 mbele
 
Unataka kusema nini mkuu si unyooshe maelezo

Kwahiyo usipoitikia salamu mtoto wako atazalishwa nje ya ndoa?

Kama akili yako ndo hiyo CCM watashindwa kweli kukurubuni?
 
Hatutaki, msitulazimishe kufanya vitu ambavyo hatupendi......
 
= mnafikiria

Hivi hizo shule mlienda kusomea jinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…