Tabia ya ovyo watu wazima kutoitikia salamu ipasavyo za wanaowazidi umri

Naomba niulize swali kwa watu wazima hasa wanawake. Hivi huwa mnafikilia nini unaposalimiwa na mtu unayemzidi umri mpaka mnashindwa kuitikia?

Unakuta mama mzima analingana na mama yako au zaidi ukimwamkia shikamoo anakujibu Safi kama vile mnalingana. Ni nini hasa kinachopelekea msikubali kusalimiwa na wadogo zenu na watoto wenu? Nawasilisha
mtoto wa 2004 embu Pambana na shule achana na mijimama
 
Shikamoo sio salamu

Tafuta salamu inayoendana na MTU mfano

MTU unayemuheshimu sana mwambie "habari ya uzima"

Aliuekuzidi umri mwambie -Unaendleaje na hali

Babu au bibi mzee sana 60+ yrs mwambie shikamoo.

Shikamoo sio salamu in inayojitosheleza
 
Ila hii tabia haijaanza leo, ni ya kitambo sana, nakumbuka kipindi nipo primary kuna mzee ana mvi kabisa zimejaa kichwani ila anaonekana ni wazee wa mjini kwa mambo yake...

Kila siku nilikua napita hapo kwake kuelekea shule ilikua nikimsalimia shikamoo anajibu salama mjukuu wangu, hajawahi kuitikia marahaba hadi nikaachaga kumsalimia, nikimkuta nje kwake nampita maana nilianza kumtilia shaka.
Hakutuma maombi?
 
Naomba niulize swali kwa watu wazima hasa wanawake. Hivi huwa mnafikilia nini unaposalimiwa na mtu unayemzidi umri mpaka mnashindwa kuitikia?

Unakuta mama mzima analingana na mama yako au zaidi ukimwamkia shikamoo anakujibu Safi kama vile mnalingana. Ni nini hasa kinachopelekea msikubali kusalimiwa na wadogo zenu na watoto wenu? Nawasilisha
Shikamoo ni salamu ya kitumwa.

Ndiyo maana Wazanzibari walioujua utumwa wanasalimiana "Cheichei" na anayeitikia anaitikia " Cheichei".
 
Mimi nilishaacha kusalimia shikamoo hata kama amenizidi miaka 20.wa mama wengi wa dar wanapenda kujifanya kuwa ni wasichana wakati yamezeeka.
 
Naomba niulize swali kwa watu wazima hasa wanawake. Hivi huwa mnafikilia nini unaposalimiwa na mtu unayemzidi umri mpaka mnashindwa kuitikia?

Unakuta mama mzima analingana na mama yako au zaidi ukimwamkia shikamoo anakujibu Safi kama vile mnalingana. Ni nini hasa kinachopelekea msikubali kusalimiwa na wadogo zenu na watoto wenu? Nawasilisha
Kwa uelewa wangu mie wanawake wengi hawanaga shida kupewa shikamoo na wadogo zao,inawezekana wewe unawaamkia watu wa umri wako/rika lako.
 
Back
Top Bottom