Tabia ya Sekretarieti ya Ajira kupanga usaili Jumamosi ni kama ubaguzi kwa Wasabato

Hakuna siku za juma zile 7 hakuna mtu hawi kwenye ibada , labda kama unataka wakupendelee wewe , Uzi wako unatakiwa usomeke mnipendelee siku ya jumamosi, na tunaweza kukupendelea na jumamosi tukaibadilia jina ikawa ijumaa
Jibu hoja ya mto thread acha kujibu kwa short cut unaonekana una mawazo mepesi sana na uwezo mdogo wa kufikili yaani maelezo ya mtoa hoja huoni logic kabisa! Da kweli Elimu yetu iko chini sana. Pole sana kwa kuandikia ujinga
 
Mademu jumamosi mnatongoza lakini kufanya interview ni issue au sio?
Jibu la kipuuzi kweli, kuna watu humu wanapaswa kufukuzwa jamiiforums maana tuna wajinga wengi! jibu hoja acha kutoa majibu mepesi wengine hapa tunakuona kichwa chako kimejaa ujinga. jibu hoja bro tuone uwezo wako wa kuchambua mambo hatutaki majibu ya kijinga
 
Niliwahi kulianzishia uzi pia hili suala, ni jambo linaloleta ubaguzi sana na kuwaminya watu wengine fursa za ajira kwanini huo usaili usiwekwe siku za kazi iwe jumamosi tu kila siku?


Uhuru wa Kuabudu na Usaili Kufanyika Siku za Ibada
 
Mbona nimejibu hoja mkuu? Wasabato nimeishi nao sana ukiwafuatisha hakuna kitu utafanya.
 
Kwamba ukikosa ibada siku moja kwa ajili ya jambo muhimu la dharura ni kumkosea Mungu? Wewe ni msomi mkuu,acha uumini wa kishamba. Mimi nimewahi kufanya interview jumapili na Jumamosi...unafikiri hiyo itanipeleka motoni?
 
Nenda kanisani kazi na usaili achana nao
 
Jibu hoja ya mto thread acha kujibu kwa short cut unaonekana una mawazo mepesi sana na uwezo mdogo wa kufikili yaani maelezo ya mtoa hoja huoni logic kabisa! Da kweli Elimu yetu iko chini sana. Pole sana kwa kuandikia ujinga
Unajua Kuna siku ya kuabudia na serekali imeifanya ni siku ya kazi kabisa , sasa wewe unataka logic gani kwa mtoa mada siku moja tu kwa watu wachache ndio tubadili?
 
Huo usahili ni siku moja tuu na ni kwa dakika chache sana kama unajali future yako wala sio jambo baya muhimu ni kumuomba Mungu tuu akusaidie ufaulu.

Je, mifugo yako nayo huwa hauifungulii au kuilisha siku ya Jumamosi? Yule anayeiangalia/kuilisha huwa hafanyi kazi?

Hapana jitoe kwa muda mfupi tuu, kwa manufaa ya baadae.
 
MFANO UKAPATA HIYO KAZI, NA UKAAMBIWA UENDE UKA SIGN MKATABA J.MOSI UTAENDA HUENDI??

THN ILI USIKWAZIKE NA IMANI YAKO KUJIAJIRI NDIO BEST OPTION, CZ KUAJIRIWA UNAWEZA AMBIWA UENDE J.MOSI KUFANYA KAZI, LET SAY HAKUNA WANAJESHO, POLICE , DOCTORS AU MANESI WASABATO??? HAWA KAZI NI SIKU 7 ZA WEEK JE HAO SIO WASABATO SANA?
 
Siku za kazi pia ni shida maana wanaofanya interview na wanaoendesha interview wengine ni wasjiriwa Wana majukumu mengine. Binafsi wasabato hata wakipata kazi ,jumamosi kwao ni shida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…