Tabia ya Sekretarieti ya Ajira kupanga usaili Jumamosi ni kama ubaguzi kwa Wasabato

Binafsi nahisi wanapanga ratiba za mitihani siku za mapumziko (weekend) kwa sababu huwa wanatumia venues(kumbi) za vyuo (mfano kumbi za chuo kikuu cha Dodoma UDOM) kama sehemu ya kufanyia mitihani na siku za weekend venue(kumbi) nyingi huwa hazitumiki hivyo wanatumia kama fursa ya kukamilisha hili jambo.

M.
 
Na waislam wakisema ijumaa wapumzike ingekuwaje yaani katika vitu ambavyo tumeingia mazima mazima waafrika ni dini mpaka wao wenyewe waliozileta wana tuona mbumbu kwa hlo.
 
Wewe kama unaona haifai usiende, mbona jumapili pia kuna usaili unafanyika. Kweli nimeamini ukiwasikiliza wasabato hakuna Jambo utafanya.
 
Tambua kuwa dini zilikuja kwa meli, Kazi ni msitakabali wa Maisha yako tofauti na hapo kuwa mchungaji
 
Nakumbuka mwaka 2013 Interview ilifanyika Mwalimu Nyerere pale Kigamboni...ilikuwa siku ya jumamosi kuna wasabato walifanya na wapo kazini mpaka Leo wapo kazini.
Serikali haina Dini sio lazima kufanya kazi ya Serikali.
Muslim wasemaje...Ijumaa ni siku ya kazi full watu wanapiga kazi.
Umewaza akija mwingine akisema jumatatu ni siku yake ya kuabudu itakuaje? Mwingine Jumatano.... Sio lazima kufanya interview za Serikali kama ilivyo kuwa sio lazima kufanya kazi kwenye viwanda vya bia.
 
Na suala la space pia.Duce/ udom/UD/ mipango siku za kazi halls zinatumiwa na wanafunzi.
 
Watu wa jumapili na ijumaa.hawanaga shida kabisaa...huwez sikia wanalalamika na interview hua zinapangwa pia siku hzoo
 
Watu wa jumapili na ijumaa.hawanaga shida kabisaa...huwez sikia wanalalamika na interview hua zinapangwa pia siku hzoo
Understanding yako iko chini sana siwezi hata ku argue na wewe tena! just think out side the box, hivi muislam safi anaweza kula nguruwe eti kwasababu wakatoliki na waluteli wanakula? usitoe majibu mepesi hivyo wakati kuna watu wengine wanaumia let us be realistic tuache chuki na majibu ya dharau kwa imani za watu tukijidai wataalamu sana wa hoja nyepesi
 
Mleta mada nchi hii ina uhuru wa kuandika na kuamua.
Hivyo ww amua kile upendacho na cha muhimu kwako.
Wasalimie wapare wote wa SDA hapo Hedaru,Makanya,Same na kwingineko.
Dah! hapa binafsi hata sijui umeandika hoja gani
 
Wewe kama unaona haifai usiende, mbona jumapili pia kuna usaili unafanyika. Kweli nimeamini ukiwasikiliza wasabato hakuna Jambo utafanya.
wenzako wanawasikiliza wala hawajapungukiwa kitu
 
Wasabato waliofanya interview sawa ni kama waislamu si wapo wanakula kitimoto au hujui lakini je hiyo ni imani yao? waza nnje ya box
 
Mi naona usahili unafanyia j.mosi ili wasahili wapige pesa ya over time. Maana ki uhalisia usahili ni sehemu ya kazi kwa nini usifanyike siku za kazi?
 
Mimi nakushauri iwe wewe ushauri hizo interview zifanyike siku ya ijumaa, kwa maana hawa Waislamu hawalalamiki kwa nini ijumaa ni siku ya majumuhisho ya ibada zao za wiki nzima lakini na ni siku ya kazi pia ...?

Lakini pia hilo wazo wewe sio mtu wa kwanza, nakumbuka Magufuli alibadilisha siku ya uchaguzi kutoka siku ya jumapili ambayo ulikuwa unafanyika kila mwaka wa uchaguzi kabla ya yeye kuwa Rais, mwaka 2020 akasema uchaguzi ufanyike siku ya jumatano ili jumapili wakristo waende kanisani.

Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, BW Mkapa hata Dr. Kikwete hili hawakuliona, na watu walikaa kimya na kumpongeza Dr. Magufuli kwa alichokifanya cha kubadili siku ya uchaguzi, ila wasiwasi jambo kama lile lingefanywa na mtu kama Kikwete la kwasema siku ya ijumaa ni siku kuu ya ibada kwa Waislamu, watu waende makazini hadi saa 11 : 45 am kisha waende misikitini na saa 01 : 15 pm warudi maofisini ingekuwa ajenda kubwa sana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…