KERO Tabia ya Shule kuchangisha pesa za mitihani kila wiki inakithiri, Walimu wameifanya kuwa mtaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Haya
Subiri tamko la serikali
Endelea kupuuza ubunifu wa walimu kuwapa watoto wako majaribio kila wiki waone hao walimu ndo maadui

Serikali itakuridhisha Kwa kupiga marufuku michango na majaribio, wakijua wazi watoto wao hawasomi hizo shule
Ni bora kulipa Ada kuliko kufanya utapeli
 
Shule nyingi za Msingi na hata Sekondari zimejitengenezea utaratibu wa kuwafanyisha mitihani wanafunzi hasa walio katika mwaka wa mitihani ya Taifa kama Darasa la Nne, Saba, kidato cha pili na nne. Shule hizi hulazimisha wanafunzi kuchangia mitihani hiyo ambayo huifanya kila Jumamosi. Wanafunzi wasiochangia mitihani hiyo huadhibiwa au kujengewa uadui mkubwa na walimu

Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kigamboni ni moja ya shule zenye hii tabia ya wanafunzi kuchangishwa pesa za mitihani. Yaani wao kila wiki ni mitihani, halafu Walimu hawasahihishi mitihani ila inasahihishwa na hao hao wanafunzi wanaofanya mitihani. Walimu wao wanaangalia pesa tu.

Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahisha ni wanafunzi wenzetu.

Naombeni na hili mlifikishe mtandaoni na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
kwanza shukuru wewe mitihani unaiona. kun shule zingine hata mitihani yenyewe hairudi. mwisho kabisa kama lawama mtu pekee wa kupewa ni wizara ya elimu tu
 
Baadae mtalalamika watoto wa viongozi kuja kuwa viongozi? Watoto wa maskini wataendelea kuwa maskini kutokana na wazazi wao kuendelea kuwa na tabia za kimaskini. Viongozi wanalipa mamilioni watoto wao wapate elimu bora huku wapiga kura wengi kwa upuuzi wao hawataki kuchangia hata weekly tests kwa ajili ya watoto wao.
 
Pesa unamchangia mwanao Bado unalia
Kwani ulimzaa na nani?
Kama unaona unaibiwa si mwanao aache shule ubaki na pesa yako

Hakuna elimu Bure, usidanganyike na siasa
Hata hao wanasiasa wanalipia yote hayo na watoto wao wapo private schools
Pole mwalimu umeongea kwa hisia sana ila nakusihi muache huo upumbavu darasa la nne kika week unamfanyisha mitihani ya nini?
 
Shule nyingi za Msingi na hata Sekondari zimejitengenezea utaratibu wa kuwafanyisha mitihani wanafunzi hasa walio katika mwaka wa mitihani ya Taifa kama Darasa la Nne, Saba, kidato cha pili na nne. Shule hizi hulazimisha wanafunzi kuchangia mitihani hiyo ambayo huifanya kila Jumamosi. Wanafunzi wasiochangia mitihani hiyo huadhibiwa au kujengewa uadui mkubwa na walimu

Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kigamboni ni moja ya shule zenye hii tabia ya wanafunzi kuchangishwa pesa za mitihani. Yaani wao kila wiki ni mitihani, halafu Walimu hawasahihishi mitihani ila inasahihishwa na hao hao wanafunzi wanaofanya mitihani. Walimu wao wanaangalia pesa tu.

Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahisha ni wanafunzi wenzetu.

Naombeni na hili mlifikishe mtandaoni na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
Mnachanga shilingi ngapi?
Ukute ni 2000/- kwa wiki.

Wazazi wenyewe ndiyo hupendekeza madarasa ya mitihani yawe na mazoezi ya ziada kupitia tests za hivyo.

Shule haiwalipi walimu kwa hiyo kazi ya ziada. Je unataka walimu watumie fedha zao kuprint papers? Na hiyo kazi ya ziada ni ya kujitolea? Ili mje JF kuwakebehi maticha na umasikini wao?
 
Siasa zinawaongopea, watoleeni watoto hizo jero jero wapige pepa, zinawajenga, ukizingatia primary hakunaga mambo ya kujisomea somea, hivyo hizo pepa ni sehemu ya mafunzo
 
Poleni sana, mzazi. Je, huwa mnachanga kiasi gani ambacho kinatosha kuwa mtaji wa biashara gani kwa hao walimu?
 
  • Thanks
Reactions: EWM
Ni bora serikali itoe tamko kwamba elimu shule za serikali tulipe ada kuliko kufanya utapeli..
Kulipa kila siku 200 za test na kila jmosi kulipa 1000 za mtihani sio utapeli?

Mtoa post ana hoja nzr asipuuzwe
Utapeli wa Tsh. 200?

Tupate wazo zuri kutoka kwako; je, unataka walimu wasiandae mitihani ama waandae ila wanafunzi wasilipe chochote?
 
Kuna mtihani gani wa kila siku?
Sh 200×watoto 800 ni sh ngp kwa siku?
Kwa week?
Kwa mwezi?

Walimu punguzeni utapeli
 
Kuna mtihani gani wa kila siku?
Sh 200×watoto 800 ni sh ngp kwa siku?
Kwa week?
Kwa mwezi?

Walimu punguzeni utapeli
Mentality ya kimasikini ndiyo inakusumbua. Pigia hesabu mwanao, acha kupigia hesabu wanafunzi wote.

Hivi unaujua ugumu wa kusahihisha mitihani mia 8 kila wiki?
 
Kwani hawalipwi mishahara?
Zamani walikuwa wanalazimisha kukopesha ubuyu na kashata kwa lazima kwa watoto wetu.

Baada ya serikali kupiga marufuku biashara ndogo ndogo za walimu mashuleni ,,
Sasa mmeanzisha utapeli wa mtihani kila siku asubuhi na jioni tuition kwa lazima.

Walimu uchwala shame on you
 
Shule nyingi za Msingi na hata Sekondari zimejitengenezea utaratibu wa kuwafanyisha mitihani wanafunzi hasa walio katika mwaka wa mitihani ya Taifa kama Darasa la Nne, Saba, kidato cha pili na nne. Shule hizi hulazimisha wanafunzi kuchangia mitihani hiyo ambayo huifanya kila Jumamosi. Wanafunzi wasiochangia mitihani hiyo huadhibiwa au kujengewa uadui mkubwa na walimu

Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kigamboni ni moja ya shule zenye hii tabia ya wanafunzi kuchangishwa pesa za mitihani. Yaani wao kila wiki ni mitihani, halafu Walimu hawasahihishi mitihani ila inasahihishwa na hao hao wanafunzi wanaofanya mitihani. Walimu wao wanaangalia pesa tu.

Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahisha ni wanafunzi wenzetu.

Naombeni na hili mlifikishe mtandaoni na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
Mchango ni shilingi ngapi
 
Kwani hawalipwi mishahara?
Zamani walikuwa wanalazimisha kukopesha ubuyu na kashata kwa lazima kwa watoto wetu.

Baada ya serikali kupiga marufuku biashara ndogo ndogo za walimu mashuleni ,,
Sasa mmeanzisha utapeli wa mtihani kila siku asubuhi na jioni tuition kwa lazima.

Walimu uchwala shame on you
Ni uchwara siyo uchwala. Inaonesha una elimu ya kuungaunga ndiyo maana hufahamu hata unachokipinga.
 
Wewe mwenye elimu kubwa umegunduwa nn?ktk taifa hili?

Walimu punguzeni njaa,, wacheni kufanya utapeli mashuleni..
 
Usingekuwa na njaa usingeita mtihani wa 200 ni utapeli.
Ndiyo maana nikakuuliza hizo fedha zinatosha kuwa mtaji wa biashara gani?
 
Mnaomponda mleta mada na wale wenye mlengo kama wake inabidi mjitafakari.Nimegundua kwamba nyinyi ndo mna akili za kimasikini yaani mnadharau 200,na kuita ndogo,Bakharesa angekuwa kama nyinyi asingeuza maandazi ya mia mia,wanachokifanya walimu ni utapeli wa moja kwa moja sisi wote tumesoma hizo shule hatukuona hiyo mitihani ya kila siku badala tuwakemee walimu tunawashangilia kwa upumbavu wanaoufanya,Alafu kutwa humu mnaiponda Ccm,

Sasa hawa walimu na Ccm wanatofauti gani?haya mambo yapo hadi mahospitalini watoto matibabu ni bure ila mpeleke mtoto ndo utajua watanzania sisi ni mahayani.kwenye vyombo vya usafiri nauli inajulikana ni buku ila konda anapiga debe buku mbili basi ndani ya gari abilia mmoja akilipa buku kama nauli stahiki kuanzia konda na abilia wenzako watakusakama kama mwizi na maneno ya dharau juu sasa ndo kama hili la walimu hawa ni Wezi.
 
Back
Top Bottom