KERO Tabia ya Shule kuchangisha pesa za mitihani kila wiki inakithiri, Walimu wameifanya kuwa mtaji

KERO Tabia ya Shule kuchangisha pesa za mitihani kila wiki inakithiri, Walimu wameifanya kuwa mtaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Usingekuwa na njaa usingeita mtihani wa 200 ni utapeli.
Ndiyo maana nikakuuliza hizo fedha zinatosha kuwa mtaji wa biashara gani?
Uulizwe wewe unayekusanya 200 kwa kila mwanafunzi .

Unafaidika na nn?
 
Uulizwe wewe unayekusanya 200 kwa kila mwanafunzi .

Unafaidika na nn?
Wanasaidia watoto wenu
Mnawaita matapeli
Uhalisia hauko hivo, serikali haiwezi kuwasaidia kwenye elimu
Washukru walimu Kwa mkakati wa kufaulisha
Elimu ni Pana, Elimu ni gharama.

We unaamka unamtuka mtoto shule, hana vitabu vya ziada, shule haina maktaba, vitabu havitoshi, walimu hawatoshi, madawati hayatoshi, watoto wengi, shuleni watoto hawapati hata uji

Mwalimu anawambia wazazi mchangie 200
Watoto wafanye majaribio, nje ya ratiba ya serikali ambayo haitekelezeki

Unakuja mtandaoni kushtaki na kulalamika mitandaoni

Sasa wakiacha hayo majaribio, unadhani mwalimu atapoteza kazi yake

Watanganyika ni watu wapumbavu sana
 
Uulizwe wewe unayekusanya 200 kwa kila mwanafunzi .

Unafaidika na nn?
Sifaidiki na chochote bali nawasaidia wanafunzi.
Ningekuwa nataka faida, watoto wa masikini kama wewe wasingemudu gharama.
 
Pesa unamchangia mwanao Bado unalia
Kwani ulimzaa na nani?
Kama unaona unaibiwa si mwanao aache shule ubaki na pesa yako

Hakuna elimu Bure, usidanganyike na siasa
Hata hao wanasiasa wanalipia yote hayo na watoto wao wapo private schools
Acha kujibu kipumbavu.
 
Wanasaidia watoto wenu
Mnawaita matapeli
Uhalisia hauko hivo, serikali haiwezi kuwasaidia kwenye elimu
Washukru walimu Kwa mkakati wa kufaulisha
Elimu ni Pana, Elimu ni gharama.

We unaamka unamtuka mtoto shule, hana vitabu vya ziada, shule haina maktaba, vitabu havitoshi, walimu hawatoshi, madawati hayatoshi, watoto wengi, shuleni watoto hawapati hata uji

Mwalimu anawambia wazazi mchangie 200
Watoto wafanye majaribio, nje ya ratiba ya serikali ambayo haitekelezeki

Unakuja mtandaoni kushtaki na kulalamika mitandaoni

Sasa wakiacha hayo majaribio, unadhani mwalimu atapoteza kazi yake

Watanganyika ni watu wapumbavu sana
Hivi kuna mtihani wa kila siku asubuhi?
Inaingia akilini?200×6 days =1200 shilings kwa week.
1200×4 weeks =4800 sh. × 400 wanafunzi =1920000/..kwa mwezi.

Baadhi ya shule wanatoa 500 sh kila siku ya mtihani..
500× 6 days =3000 shilings × 4 weeks 12000 shilings kwa mwezi.
12000 ×400 wanafunzi =4800,,000/ kwa mwezi..
Huu ni mradi wa watu unasemaje walimu wanasaidia wanafunzi?

Kama ni mtihani kwann wasifanye kila week end?
Why kila siku asubuhi.?
Na kama msaada kwani wao wana kazi gani pale shuleni?

Hata mimi nimesoma kayumba lakini haikuwa kama wafanyavyo walimu wa sasa..
 
Mtoto wa maskini atabaki kuwa wa maskini tu huwezi kukuta mzazi anaemsomesha mwanae english medium akaja kulalamikia mitihani ya wiki ni sisi kajamba nani ndio tunalalamika.
Sasa tatizo hawaweki wazi, wanasema Elimu buree, wazazi wanabweteka, baadae wanaanza kudaiwa hela, unadhani inakuaje hapoo?
Lol
 
Usingekuwa na njaa usingeita mtihani wa 200 ni utapeli.
Ndiyo maana nikakuuliza hizo fedha zinatosha kuwa mtaji wa biashara gani?
Kwni msingi wako wa genge ni shilings ngapi?
Usijifanye KANJUNJU aisee.
 
Watanzania kwa kupenda miteremko...
Hawa wanaoitwa maskini sijawahi ona wakilalamikia bei za vijora inayopanda kila mwaka wa fedha wa kiserikali...
Huyu anayeitwa maskini yuko radhi kutoa 20,000/- ili ale keki ya "basdei" ya shogake lakini atapiga kelele na nduru kuhusu 200/- ya mtihani wa mtoto wake...
 
Shule nyingi za Msingi na hata Sekondari zimejitengenezea utaratibu wa kuwafanyisha mitihani wanafunzi hasa walio katika mwaka wa mitihani ya Taifa kama Darasa la Nne, Saba, kidato cha pili na nne. Shule hizi hulazimisha wanafunzi kuchangia mitihani hiyo ambayo huifanya kila Jumamosi. Wanafunzi wasiochangia mitihani hiyo huadhibiwa au kujengewa uadui mkubwa na walimu

Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kigamboni ni moja ya shule zenye hii tabia ya wanafunzi kuchangishwa pesa za mitihani. Yaani wao kila wiki ni mitihani, halafu Walimu hawasahihishi mitihani ila inasahihishwa na hao hao wanafunzi wanaofanya mitihani. Walimu wao wanaangalia pesa tu.

Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahisha ni wanafunzi wenzetu.

Naombeni na hili mlifikishe mtandaoni na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
Walimu ni wapigaji tu,shule ya sekondari kawe walimnyima mdogo wangu matokeo ya mtihani eti kisa hajalipia ela ya walimu wakujitolea,upuuzi kabisa
 
Ni 4000 kwa mwezi,unakula sh ngapi?
Au umezaa Kijiji?
Iyo elfu nne anatoa peke yake, unakuta darasa la nne madarasa matatu jumla wapo 200, aya piga hesabu sh. Ngapi jumla inakuwa? Laki nane iyo, na wanacheza mchezo kila wiki anachukua mwalimu mmoja,
Yaani mishahara mnalipwa halafu mnataka wazazi wawatajirishe wapuuzi nyie
 
Pigia wanao,siyo watoto wa wenzio mkuu🤣🤣🤣🤣
 
Halafu kuna kigenge cha wahuni chenye maslahi binafsi,
Kinachojiita uongozi wa wazazi wa wanafunzi hapo shuleni.

Hawa ndy wanashirikiana na walimu kutoa maamuzi ya shinikizo..
Ni kama kauli ya uongozi wa wazazi ndy kauli ya wazazi wote hapo shuleni.
Hata kama hawajashirikishwa wazazi wote.
 
Imeandikwa kila mtu atakula kazini kwake
 
Back
Top Bottom