Tabia ya wasajili laini kutumia vitambulisho vya watu bila wenyewe kujua kusajilia watu wengine zaidi ni hatari

Tabia ya wasajili laini kutumia vitambulisho vya watu bila wenyewe kujua kusajilia watu wengine zaidi ni hatari

Dawa yake anamaliza tu hapo hapo unaangalia na kuifunga
 
Hahaaa wale wanachokifanya wanakuambia mtandao unasumbua ,alafu anachukua laini ingine anafanya kama anajaribu jaribu ,utashangaa kafungua laini ya tatu ndo imekubali ,hapo ujue ushapigwa baaadhi yao ni wahuni sana,afadhali wale wanaotumia vitambulisho vyao
 
Serika ina mambo mengi jamani !

wewe unatakiwa uhakiki namba zilizosajiliwa kwa kutumia kitambulisho chako ukiona ambazo huzitambui ukazifute mara moja.

yaani Wabongo kila kitu serikali wakati vitu vingine viko ndani ya uwezo wao wenyewe ila lawama ni kwa serikali.

badilikeni…
 
Kuna kitu kinaitwa Authentication, Mitandao ya Simu inatakiwa iende mbali zaidi kufanya authentication zaidi ya Vidole tu, namba ya nida pekee Bila Fingerprint Haiwezi kusajili
 
kidole si anaweka yoyote tu mkuu kwani inaishu gani
Kumbe hata unacholalamikia hukijui[emoji23][emoji23][emoji23]
Alama za vidole zinatofutiana mkuu, kila mtu na yake... Huyo siyo mwanamke/,mwanaume kwamba utatumia na wengine hata kama yuko ndani ya ndoa.[emoji23]
 
Kuna siku walinletea ujinga huo...et kasajli afu akajifanya line imeharibika akaitupa pemben akachukua nyingnr akanisajilia....alivomalza nijamuulza hyo line nyngne imekataa akasema ishaharibika ni ya kutupa...nikamwambia ilete nisepe nayo akasema hapana mpk nimpe buku...nikampa nikasepa na line zote mbili
 
Habari wakuu natumaini mko poa wote,

Iko hivi kuna kipindi nilipoteza simu yangu ya smart pamoja na laini yani niliibiwa sasa nikakaa kama mwezi maana simu nilikuwa naona sehemu ilipo nikaamini nitaipata baadae nikaja nikakata tamaa nikaona isiwe kesi ngoja nirudishe laini zangu.

Siku nimekaa nikamuona mtu anasajili line za tigo na airtel kwa bei nzuri nikaamua kusajili upya line zangu zote zilizo potea na simu sasa hichi ndo kisa nimeamka nacho asubuhi.

Leo nikaamua kuangalia namba ambazo zimesajiliwa na kitambulisho changu cha nida namba nilizoziona mpaka nika shangaa nimekuta line ya tigo ina number 4 wakati tigo niko na line mbili. Airtell nina line moja nimekuta nina line 2 haloteli sina nimekuta nina line ya halotel kasoro voda tu ndo nimekuta iko salama.

SWALI: hawa watu huo mchezo wanao ufanya umenikera sana kumbe unawapa number ya nida akija mtu mwingine na wao wana sajili kwa kitambulisho chako.

Tena kitu ambacho sio sahihi na hili swala limeongelewa sana kuhusu kumsajilia mtu line kwa kitambulisho cha mtu kuwa ni kosa. Ningekuwa na uwezo wa kuwa shtaki sikufichi leo ninge anza process zote na nijue huyo msajili line kwanini alifanya hivyo.

N:B Penda kuangalia kama mimi yaweza kuwa una number zaidi ya 7 bila kujijua na nimepanga naenda kuzifungia line zote bila huruma kama kuna mtu alikuwa anatumia line yangu atajua hajuii.

Nawasilisha.
Mkuu. Punguza hasira
 
Unaangaliaje na kuifunga, nimesahau code #
*106#
Bonyeza 3 weka namba ya NIDA bila kuweka space au alama yoyote kama -. Utaletwa namba zote ulizosajili ya mitandao yote
Njia salama ya kusajili laini ni kwa maduka ya mtandao km ni vodashop, tigoshop n.k tofauti na hapo utakuta laini zingine zimesajiliwa. Mimi niliyafuta, nilienda vodashop.
 
Back
Top Bottom