Tabia ya wasajili laini kutumia vitambulisho vya watu bila wenyewe kujua kusajilia watu wengine zaidi ni hatari

Dawa yake anamaliza tu hapo hapo unaangalia na kuifunga
 
Hahaaa wale wanachokifanya wanakuambia mtandao unasumbua ,alafu anachukua laini ingine anafanya kama anajaribu jaribu ,utashangaa kafungua laini ya tatu ndo imekubali ,hapo ujue ushapigwa baaadhi yao ni wahuni sana,afadhali wale wanaotumia vitambulisho vyao
 
Serika ina mambo mengi jamani !

wewe unatakiwa uhakiki namba zilizosajiliwa kwa kutumia kitambulisho chako ukiona ambazo huzitambui ukazifute mara moja.

yaani Wabongo kila kitu serikali wakati vitu vingine viko ndani ya uwezo wao wenyewe ila lawama ni kwa serikali.

badilikeni…
 
Kuna kitu kinaitwa Authentication, Mitandao ya Simu inatakiwa iende mbali zaidi kufanya authentication zaidi ya Vidole tu, namba ya nida pekee Bila Fingerprint Haiwezi kusajili
 
kidole si anaweka yoyote tu mkuu kwani inaishu gani
Kumbe hata unacholalamikia hukijui[emoji23][emoji23][emoji23]
Alama za vidole zinatofutiana mkuu, kila mtu na yake... Huyo siyo mwanamke/,mwanaume kwamba utatumia na wengine hata kama yuko ndani ya ndoa.[emoji23]
 
Kuna siku walinletea ujinga huo...et kasajli afu akajifanya line imeharibika akaitupa pemben akachukua nyingnr akanisajilia....alivomalza nijamuulza hyo line nyngne imekataa akasema ishaharibika ni ya kutupa...nikamwambia ilete nisepe nayo akasema hapana mpk nimpe buku...nikampa nikasepa na line zote mbili
 
Mkuu. Punguza hasira
 
Unaangaliaje na kuifunga, nimesahau code #
*106#
Bonyeza 3 weka namba ya NIDA bila kuweka space au alama yoyote kama -. Utaletwa namba zote ulizosajili ya mitandao yote
Njia salama ya kusajili laini ni kwa maduka ya mtandao km ni vodashop, tigoshop n.k tofauti na hapo utakuta laini zingine zimesajiliwa. Mimi niliyafuta, nilienda vodashop.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…