Tabia ya Watanzania ya kuzaa hovyo ndiyo chanzo cha umaskini. Bodaboda ana watoto sita! Hata Serikali inashindwa kupanga mipango


Mbona mnaendelea kuwa na uelewa wenye makosa kuhusu watu na maenedleo ya nchi? Ndiyo Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji watu. Lakini mimi nawaambieni leo, siyo kila mtu ni rasilimali kwa nchi. Wengine ni mzigo. Hili hatutaki kuliongelea tukidhani kwamba ni kuwa na dharau na kuto wajali wengine. Ni ukweli kwamba nchi za Afrika zina idadi kubwa sana ya watu wasiojielewa.
 
Wewe eliakeem una mawazo kama yangu. Yafaa tuunde kikosi kazi tuzunguke nchi nzima kuwatukana watanzania ili wafunguke akili.
 

Endeleeni kumsingizia Mungu mambo ya uongo. Wee unajua umepanga chumba kimoja na sebule. Unaanza kuzaa watoto kama una shule ya chekechea. Halafu wakifa kwa utapiamlo, unaanza kusema ni mipango ya Mungu. Wakati Mungu alikupa utashi na akili ya kupangilia na kudhibiti mambo.
 
Hayo Madawa ya kulevya si baadhi ya hao viongozi Wana wakumbatia waingizaji madawa nchini. Na Mtaani tuna wajua kwa nini wasikamatwe. Kama Chiko, Mzee mtamamchungu wote wapo mtaa mmoja pale magomeni kwa bibinyau.

Hiyo yote inatokana na ujinga wa wananchi. Kama nchi ina watu wanaojielewa, hakuna kiongozi atakayefanya ujinga. Sasa aina ya raia waliopo hawaelewi mambo yalivyo, basi wajinga ndivyo waliwao.
 
Tena watu wa hivi Tanzania wapo wengi waliosoma na ambao hawajasoma,hawaelewi ni kwa namna gani kutofatilia mambo basic katika nchi yanavyogharimu nchi.tuna population kubwa iliyojaa wajinga.
Yani ni kazi sijui ni nini kifanyike kwa kweli.
Hawana hata vitendea kazi na mazingira bora ya kufuatilia masuala ya nchi. TV iko moja, sebuleni mko 15+, vitoto vingine vinaumwa, vingine vinalilia katuni , mke anahangaika na mkaa hapo hapo. Baba inabidi akimbilie baa akapate utulivu huko. Kufika huko Nako anakutana na makelele ya baa. Inabidi ajizime data kwa kulewa.

Kwahiyo, unakuta nyumbani ni full vurugu kwasabb ya population density kubwa.
 
We hauna watoto nini, mbona unakasirika wenzako wakizaa? Walikuomba hela ya nepi? Kinachokuumiza ni nini hasa!! Bora ungeongea kikawaida sasa we unakuja umefura kweli eti kisa wenzako wana zaa watoto wengi. Na wewe Kazae kumi ili mihemko yako itulie.

Mkuu, duniani kote asilimia kubwa ya chimbuko la wahalifu ni kule kwenye makazi duni. Ambako watu wanazaana kama panya.
 
Unadhani kuzaa wengi ndio kutakuepusha na ushoga? Hakuna kizazi kitabaki salama kwa kipindi hiki, wameshakuwa exposed
Hujanielewa mkuu, kwa vile hao mashoga hawawezi kazalishana.tena bora sisi wenye uwezo tupige kazi maradufu kuziba gepu la hao ambao wameleft.
 
Unamtaka Mungu kama vile unamjua sana kuzidi waliokuletea hiyo dini. Halafu hao hao waliokuletea dini, ndiyo wanakushauri usizae sana utafubaa na kuwa maskini, unawabishia, lkn dini yake unaikubali. What a contradiction!
 
Sweden ni nchi ndogo kwa Tanzania.Na kama idadi ya watu ndiyo chanzo cha umaskini basi Brazil,China na India ndiyo nchi ambazo zingekuwa maskini kuliko zote duniani.Na Afrika Nigeria,Misri,Kenya na Ethiopia ndiyo zingekuwa nchi maskini.
 
Mkuu mleta Mada inaelekea umetoka kwenye kikao kujadili population ya Tanzania,

Ni Tanzania kuna watu wengi Sana. Hawana faida Kwa uchumi wa Nchi.

Angalia kipindi cha campaign CCM ikiwasomba watu rundo kwenye Malori, kwenda viwanjani.

CCM iko madarakani Kwa Sababu ya watu wengi wasiokuwa na faida nchini.

Angalia waalimu wanaisaidia CCM kushinda Kwa wizi wa kura Kwa malipo ya laki na nusu Tu 😂.
 

Mkuu hayo ndo mawazo yaliyotufikisha hapa tulipo. Kuishi kwa bahati nasibu. Bro maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…