Tabia ya Watanzania ya kuzaa hovyo ndiyo chanzo cha umaskini. Bodaboda ana watoto sita! Hata Serikali inashindwa kupanga mipango

Tabia ya Watanzania ya kuzaa hovyo ndiyo chanzo cha umaskini. Bodaboda ana watoto sita! Hata Serikali inashindwa kupanga mipango

''Sweden's area is approximately 410,340 km2 (158,433 sq mi), while the area of Tanzania is approximately 885,800 km2 (342,009 sq mi). This means Tanzania is 2.16 times bigger than Sweden''
chanzo: embassies.net

Watu ndio taifa, bila watu hakuna taifa; vitani wanatakiwa watu + teknolojia

Mbona mnaendelea kuwa na uelewa wenye makosa kuhusu watu na maenedleo ya nchi? Ndiyo Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji watu. Lakini mimi nawaambieni leo, siyo kila mtu ni rasilimali kwa nchi. Wengine ni mzigo. Hili hatutaki kuliongelea tukidhani kwamba ni kuwa na dharau na kuto wajali wengine. Ni ukweli kwamba nchi za Afrika zina idadi kubwa sana ya watu wasiojielewa.
 
Kwa hiyo unataka tufikie hatua hiyo ya kulamba kila kitu ndo tusituke.
Shida tuliyonayo kama taifa, asilimia kubwa ya watanzania ni wajinga. Wanakosa hata elimu ya msingi ya kujisimamia katika maisha, kutia ndani kuzaa bila mpangilio. Mtu anajikuta ana watoto 6. Hata ukimuuliza kama alikuwa na mpango wa kuwa na watoto 6. Atakujibu hajui na kumsingizia Mungu kwamba ni mipango yake.
Wewe eliakeem una mawazo kama yangu. Yafaa tuunde kikosi kazi tuzunguke nchi nzima kuwatukana watanzania ili wafunguke akili.
 
Nenda kamuombe mungu radhi!

Hakuna kiumbe wa Mungu aliezaliwa hovyo hovyo kama unavyodhani na elimu hii ya kizungu ilivyokupotosha sana!

Kila kiumbe unachokiona chini ya jua Mungu alipanga kiwepo kabla misingi ya ulimwengu kuwepo!

Tupo katika zama ambazo janga moja tu linaua mamilioni ya watu popote pale Duniani,uwepo was uzao mwingi ni maandalizi ya nature muelekeo wa ku balance ecosystem!

Endeleeni kumsingizia Mungu mambo ya uongo. Wee unajua umepanga chumba kimoja na sebule. Unaanza kuzaa watoto kama una shule ya chekechea. Halafu wakifa kwa utapiamlo, unaanza kusema ni mipango ya Mungu. Wakati Mungu alikupa utashi na akili ya kupangilia na kudhibiti mambo.
 
Hayo Madawa ya kulevya si baadhi ya hao viongozi Wana wakumbatia waingizaji madawa nchini. Na Mtaani tuna wajua kwa nini wasikamatwe. Kama Chiko, Mzee mtamamchungu wote wapo mtaa mmoja pale magomeni kwa bibinyau.

Hiyo yote inatokana na ujinga wa wananchi. Kama nchi ina watu wanaojielewa, hakuna kiongozi atakayefanya ujinga. Sasa aina ya raia waliopo hawaelewi mambo yalivyo, basi wajinga ndivyo waliwao.
 
Tena watu wa hivi Tanzania wapo wengi waliosoma na ambao hawajasoma,hawaelewi ni kwa namna gani kutofatilia mambo basic katika nchi yanavyogharimu nchi.tuna population kubwa iliyojaa wajinga.
Yani ni kazi sijui ni nini kifanyike kwa kweli.
Hawana hata vitendea kazi na mazingira bora ya kufuatilia masuala ya nchi. TV iko moja, sebuleni mko 15+, vitoto vingine vinaumwa, vingine vinalilia katuni , mke anahangaika na mkaa hapo hapo. Baba inabidi akimbilie baa akapate utulivu huko. Kufika huko Nako anakutana na makelele ya baa. Inabidi ajizime data kwa kulewa.

Kwahiyo, unakuta nyumbani ni full vurugu kwasabb ya population density kubwa.
 
We hauna watoto nini, mbona unakasirika wenzako wakizaa? Walikuomba hela ya nepi? Kinachokuumiza ni nini hasa!! Bora ungeongea kikawaida sasa we unakuja umefura kweli eti kisa wenzako wana zaa watoto wengi. Na wewe Kazae kumi ili mihemko yako itulie.

Mkuu, duniani kote asilimia kubwa ya chimbuko la wahalifu ni kule kwenye makazi duni. Ambako watu wanazaana kama panya.
 
Unadhani kuzaa wengi ndio kutakuepusha na ushoga? Hakuna kizazi kitabaki salama kwa kipindi hiki, wameshakuwa exposed
Hujanielewa mkuu, kwa vile hao mashoga hawawezi kazalishana.tena bora sisi wenye uwezo tupige kazi maradufu kuziba gepu la hao ambao wameleft.
 
Nenda kamuombe mungu radhi!

Hakuna kiumbe wa Mungu aliezaliwa hovyo hovyo kama unavyodhani na elimu hii ya kizungu ilivyokupotosha sana!

Kila kiumbe unachokiona chini ya jua Mungu alipanga kiwepo kabla misingi ya ulimwengu kuwepo!

Tupo katika zama ambazo janga moja tu linaua mamilioni ya watu popote pale Duniani,uwepo was uzao mwingi ni maandalizi ya nature muelekeo wa ku balance ecosystem!
Unamtaka Mungu kama vile unamjua sana kuzidi waliokuletea hiyo dini. Halafu hao hao waliokuletea dini, ndiyo wanakushauri usizae sana utafubaa na kuwa maskini, unawabishia, lkn dini yake unaikubali. What a contradiction!
 
Kwa mwendo huu hakuna rais atakayeweza kuumaliza umaskini wa nchi hii.

Ili twende sawa nitoe tafsiri ya umaskini kwa mujibu wa IMF:- umaskini ni hali ya kukosa huduma za afya/maji, chakula, elimu na mahala pazuri pa malazi (nyumba bora).

Kwa tafsiri hii, na kwa uzazi holela wa hapa nchini, ni lini kila mtanzania atakuwa na uwezo wa kuwa na nyumba bora, uwezo wa kupata huduma za afya aitakayo kwa bima ama fedha yake, uwezo wa kupata milo 3 bila shida yoyote??

Unakuta bodaboda ana watoto 6?? Mama ntilie, machinga na barmaid eti nao wana familia kubwa? Nchi hii tunaenda wapi? Watu waelimishwe kuwa, siyo kila mtu lazima azae. Watoto siyo asset kwamba utakopea mkopo.

Serikali ikijenga shule ama zahanati, miaka 2 tu zimezidiwa na idadi ya watu. Hata madawati yanakuwa tatizo kila mwaka kwasbb watanzania wanafyatua watoto mno. Hakuna kitu kinawezekana bila family planning.

Dr. Slaa alipokuwa balozi Sweden alisema "Tanzania na Sweden zilikuwa na idadi sawa ya watu mwaka 1961 (milioni 9 kila moja). Hivi sasa Sweden ina watu 15M, wakati Tanzania ina watu 60+M". Hii ni hatari.

Kwa ujinga huu wa kuzaa hovyo umaskini hautatuachia. Watu milioni 60, walipa Kodi 2M !!!

Itungwe sheria, mtu akitaka kuzaa aweke milioni 10M benki kama dhamana ya malezi bora ya mtoto. Vinginevyo, shika, peleka akafungwe.
Sweden ni nchi ndogo kwa Tanzania.Na kama idadi ya watu ndiyo chanzo cha umaskini basi Brazil,China na India ndiyo nchi ambazo zingekuwa maskini kuliko zote duniani.Na Afrika Nigeria,Misri,Kenya na Ethiopia ndiyo zingekuwa nchi maskini.
 

Attachments

  • Screenshot_2024-06-14-16-45-36-870_com.google.android.googlequicksearchbox.jpg
    Screenshot_2024-06-14-16-45-36-870_com.google.android.googlequicksearchbox.jpg
    1.3 MB · Views: 3
Mkuu mleta Mada inaelekea umetoka kwenye kikao kujadili population ya Tanzania,

Ni Tanzania kuna watu wengi Sana. Hawana faida Kwa uchumi wa Nchi.

Angalia kipindi cha campaign CCM ikiwasomba watu rundo kwenye Malori, kwenda viwanjani.

CCM iko madarakani Kwa Sababu ya watu wengi wasiokuwa na faida nchini.

Angalia waalimu wanaisaidia CCM kushinda Kwa wizi wa kura Kwa malipo ya laki na nusu Tu 😂.
 
Unaweza ukazaa mtoto mmoja na akajakuwa mwizi au kibaka. Na unaweza ukazaa watoto saba na wote wakapata mafanikio na kushiriki kujenga uchumi wa nchi, wao binafsi na wa watu wao wa karibu. Life is not a black and white thing, kuna gray n.k.
Anyway kila mtu ana mawazo yake na circumstances zake alizo/anazopita katika maisha.

Mkuu hayo ndo mawazo yaliyotufikisha hapa tulipo. Kuishi kwa bahati nasibu. Bro maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua.
 
Back
Top Bottom