Tabia ya waumini wengi wa KKKT kuondoka kabla ya ibada kuisha, Ni ishara kanisa linahitaji mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa ibada

KKKT ni nzuri ila kuna watu wanaiharibu,kwanza sadaka zimekuwa na msisitizo kama TRA wako tayari wahubiri dak 20 ila muda wa kusisitiza maokoto uwe mrefu.Pia baadhi ya watumishi wanajitangaza kuliko kumtangaza Mungu na taasisi.Matatizo ya watumishi wanajipa kipaumbele kuliko wenye shida na umaskini na mengineyo.Sasa hao wanaotoka ibadani,unakuta mtumishi anapenda kuhubiri yeye mwenyewe kila jumapili na hana nguvu ya ufafanuzi wa neno.Akiita mhubiri tofauti anahakikisha hamzidi kiwango,watu wakiona hivyo ibadq huwa inachosha mno.
 
Hiki ndio kizazi cha nyoka. Badala ya waumini kubadilika na kufuata taratibu na miongozo ya inada. Ibada ndio inatakiwa kufuata ratiba za watu. No wonder siku hizi mdada anatoka kanisani kisha anaenda kuopolewa na walevi
 
Hahahaha Azania front ... Ukifika hapo Luther house nenda kwenye Ile cafeteria pale chini ya Mzee shayo mwambie akupe breakfast Kwa jina langu!

Usisahau kubeba TUMWABUDU Mungu
 
Wakatoliki bhana πŸ˜‚ kwahy mkiwa na mpangilio wa kanisa moja ndo mnaambiwa wote mtoke mapema? πŸ˜‚
Ishu n uongozi tuu na sio umoja huo unaoutaka mana ht familia tuu ina kiongozi.
Ratiba inapangwa na makao makuu na nilazima ifuatwe, KKKT ni kama mkusanyiko na kila kikundi kinapanga yake, mfano baadhi misa ya Jumapili inaanza saa 12 asubuhi mpaka saa tatu kisha inaingia misa ya pili, lakini wengine inaanza saa 1 asubuhi na ni misa moja tu.
 
Hahahaha Azania front ... Ukifika hapo Luther house nenda kwenye Ile cafeteria pale chini ya Mzee shayo mwambie akupe breakfast Kwa jina langu!

Usisahau kubeba TUMWABUDU Mungu
Amina Amina mtumishi...... Bwana Yesu asifiwe, unataka nioshe vyombo eeh πŸ˜‚ πŸ˜‚

Hivi makanisa ya mjini km st Joseph na Azania Front hata st Albans posta waumini wake wanaishi hapo hapo mjini ?

Maake nilishangaa kuona mtu anatoka ety africana kwenda kusali huko na ndo ratiba yake mwingine namjua naye kimara kuja kusali mjini! Huko kote sii wanaovuka makanisa?
 
Huwezi kuosha vyombo! Labda iwe si Mzee shayo anayeendelea kufanya kazi hapo!

Watu Wana madhabahu zao wanazifata mkuu πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…