Mallia
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 437
- 1,562
Hii tabia ya chafu ya kupeleka wenza nyumbani alafu wazazi wanamkataa mtu uliyempeleka imepelekea vijana wengi kuingia kwenye mahusiano ya ndoa na watu ambao sio machaguo yao na ndio maana ndoa za sikuhizi hazidumu, unakuta mtu ni mchaga basi kisa wazazi wake wanataka wachaga wenzao anamuacha labda binti mzuri wa kabila lingine ambae ukute wamesota wote alafu anaskiliza wazazi anachagua mtu wa kabila lake mwishiwe ndoa zinakufa
Naongea haya sababu yametokea ndani ya familia yangu , niliwahi chumbiwa na mwanaume ambae nilitoka nae mbali sana, kipindi ambacho nimemaliza chuo akaleta barua nyumbani, mwanaume ni mtu wa Dodoma mgogo, wazazi wakamkataa kabisa kisa mkoa anaotoka, wakajakunyoosha mikono juu baada ya mimi kupata ujauzito wa huyo mwanaume, wakamuita haraka na Ndoa ikafungwa haraka haraka bila kupenda na leo ni mwaka wa 11 ndoa ina amani tele
Mdogo wangu wa kiume anaefuta hivyo hivyo akapeleka mwanamke wa kabila tofauti , wakakaa kikao wakamkataa eti hilo kabila halifai kuoa mwisho wa siku akalazimishwa kuowa mtu wa nyumbani, kweli akampata na kumpeleka but si mtu ambae alikuwa moyoni ni basi tu, ndoa ikafungwa , mimba ya kwanza ikakutwa mwanamke ana VVU, kaka akachanganyikiwa, akapimwa zaidi ya mara tatu kwa miezi tofauto akakutwa yupo salama, yule mwanamke ugonjwa alipoutoa haikujulikana
Kikawekwa kikao kiamue mustakabali wa ndoa, wale wale mashangazi waliomkataa mwanamke wa kwanza ndio hao hao wakalazimisha ndoa ivunjwe eti hawataki kaka afe mapema, wakapiga majungu ndoa ikavunjwa sasa hivi wametengana, kaka kuja kushtuka yule mwanamke aliyekataliwa nyumbani kashaolewa na mtu mwingine na maisha yanaendelea vizuri tu
Juzi tena mdogo wangu wa mwisho wa kiume kapeleka taarifa za kutaka kuowa binti wa singida huko nae vile vile ni mtu ambae wanafahamiana tokea shule hadi kutafuta maisha wamesaidiana, home wamemkataa , huyu mdogo wangu wa mwisho ndio kacharuka kabisa ,kawaambia anaowa yeye hawaowi ndugu kwa hasira akaondoka hajarudi tena
Sasa kwa tabia kama hzi vijana mnaotarajia kuowa or kuolewa kuweni makini sana na ndugu , usishinikizwe na mtu kuchagua mtu wa maisha yako, mwanamke au mwanume wa maisha yako ni wewe mwenyewe unamjua,
Ukiowa mwanamke mshenzi kisa ndugu wanamtaka,jua mabalaa yatakukuta wewe hao ndugu watakuwa wanaskia tu huko japo walikuwa mstari wa mbele kukushinikiza, oa au olewa na mtu ambaye umemuelewa na amekuelewa na unajua kumdhibiti na mnaweza kuishi kwa amani na upendo, usioe kabila kama kigezo mtakuja kulia.