JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Tabia ya Watoto kutelekezwa kwa babu na bibi bila kujaliwa na wazazi wao imeonekana kushamiri Mkoani Njombe.
Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto, Willfred Willa anasema watoto wengi wanaopata madhara ni wale ambao wanalelewa na bibi na babu zao huku wazazi wengi wakiwa na migogoro, majukumu, afya au vifo.
“Hata watoto wanaobakwa wengi wao wanaishi na babu na bibi ukiwauliza baba na mama wako wapi watakwambia wapo Dar es Salaam, au anakwambia yupo mjini au anakwambia hamjui,” anasema Willa
Afisa wa Ustawi wa Jamii, Petro Mahanza anasema hali hiyo imekithiri mkoani hapo, wanachofanya ni kuendelea kutoa elimu kwa wazazi kutoa huduma ili kutengeneza kizazi bora cha baadaye.
Source: Azam TV