Tabia za mtu ambaye utotoni mwake amedekezwa sana

Tabia za mtu ambaye utotoni mwake amedekezwa sana

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Mwanaume ambaye utotoni amedekezwa sana

-Anakuwa na misimamo mikali sana (rigid), mwengine anakuwa legelege sana kiasi kwamba kila kitu anamtegea mama yake na dada zake

-Hawezi kudumu na Mwanamke,kwa maana anakuwa anapenda sana ulevi kupindukia, uvutaji bangi,kutumia fedha nyingi sana bila mahesabu,anakuwa na madeni sugu,anakuwa na utovu wa nidhamu kazini hivyo anaweza kufukuzwa kazi mara kwa mara, anaweza kuonekana mzembe sana kazini,mtoro sugu kazini,

Anafanya kazi chini ya viwango,anapenda mishangazi impe fedha za bure ,anakuwa hataki kazi, akipewa mtaji anakula, akitafutiwa kazi anatafuta kisingizio cha kuibua ugomvi kisha anaacha kazi,akipata fedha nyingi sana anatumia zote kwenye pombe na kuhonga wanawake mpaka zinaisha anarudi nyumbani

-Anakuwa na gubu, kisirani, chuki, wivu wa mapenzi uliopindukia,anapenda kususa, kununa, kutishia muachane, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano, kudhalilisha watu wengine kwa makusudi,anataka kusujudiwa

-Anazaa kila mtoto na mama yake lakini hatoi huduma zozote.

Mwanamke ambaye utotoni amedekezwa sana

-Anakuwa na rekodi ya kujenga mahusiano na waume za watu kwa miaka mingi ili apate fedha nyingi sana bila kufanya kazi yoyote

-Anakuwa anapenda sana starehe ikiwemo ulevi kupindukia,kwenda night club,kutumia fedha nyingi sana kwenye sherehe na shughuli,anakuwa na marafiki wengi sana lakini hakuna hata mmoja mwenye dira ya maisha.

-Anaweza kuzaa kila mtoto na baba yake ,hata akiwa na miaka 36 bado anakuwa anavaa nguo fupi,anapenda night club,anachora tattoo,

-Anakuwa anavutiwa kimapenzi zaidi na wanaume ambao wanavaa mlegezo, kucheza kamari, kuvuta bangi,kunywa pombe sana, kubadilisha wanawake mara kwa mara kwa maana anapenda maisha ya anasa.

Wanaume ambao utotoni mwao walideka sana huongoza kwa kujenga ukaribu uliopitiliza na mama zao pamoja na dada zao.

UDHAIFU wao ni kwamba huwa hawana maamuzi yoyote ndani ya familia zao isipokuwa wanategemea maamuzi ya mama na dada zao.

tabia yao husababisha wake zao kuteswa sana na mama zao pamoja na dada zao.

Mama mzazi ambaye ammdekeza mtoto wake wa kiume huwa anaweza kuingia chumbani mwa kijana wake bila kubisha hodi, anaweza kumfukuza mke wa kijana wake na kuleta mwanamke mwingine ambaye kwake yeye ataona ndiyo Mwanamke sahihi kwa kijana wake.

Mwanaume ambaye amedeka sana huwa anaweza kushuhudia mwenza wake anapigwa, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kugombezwa na mam yake mzazi au dada zake lakini haongei chochote.

Mwanaume ambaye amedeka sana husababisha mateso makubwa sana kwa mke wake na watoto wake.

Wengi huishia kuwa walevi kwa sababu hawana uwezo wa kusimama ngangari ndani ya familia zao.

Mama yeyote ambaye anajua mtoto wake wa kiume amedeka sana huwa anapata hofu kuhusu aina ya Mwanamke kijana wake anaweza kuchagua hivyo huamua kumchagulia mke ambaye kwake anajua itakuwa rahisi kumtawala.

Mwanaume ambaye amedeka sana utotoni huwa hawezi kubalance mapenzi yake kwaa mama yake na mapenzi yake kwa mwenza wake yaani kwake anaweza kufanya upendeleo kupitiliza kwa mama yake mzazi au kwa mwenza wake bila kujali kwamba mama ni muhimu sana maishani kwenye nafasi yake kama mama , vilevile mwenza ni muhimu sana maishani mwake kwenye nafasi yake kama mwenza.

Anashindwa kuweka mipaka baina ya mama yake mzazi na Mwenza wake.
 
Mwanaume ambaye utotoni amedekezwa sana

Tabia zake

-Anakuwa na misimamo mikali sana (rigid), mwengine anakuwa legelege sana kiasi kwamba kila kitu anamtegea mama yake na dada zake

-Hawezi kudumu na Mwanamke,kwa maana anakuwa anapenda sana ulevi kupindukia, uvutaji bangi,kutumia fedha nyingi sana bila mahesabu,anakuwa na madeni sugu,anakuwa na utovu wa nidhamu kazini hivyo anaweza kufukuzwa kazi mara kwa mara, anaweza kuonekana mzembe sana kazini,mtoro sugu kazini,anafanya kazi chini ya viwango,anapenda mishangazi impe fedha za bure ,anakuwa hataki kazi, akipewa mtaji anakula, akitafutiwa kazi anatafuta kisingizio cha kuibua ugomvi kisha anaacha kazi,akipata fedha nyingi sana anatumia zote kwenye pombe na kuhonga wanawake mpaka zinaisha anarudi nyumbani

-Anakuwa na gubu, kisirani, chuki, wivu wa mapenzi uliopindukia,anapenda kususa, kununa, kutishia muachane, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano, kudhalilisha watu wengine kwa makusudi,anataka kusujudiwa
-Anazaa kila mtoto na mama yake lakini hatoi huduma zozote.
 
Mwanamke ambaye utotoni amedekezwa sana

-Anakuwa na rekodi ya kujenga mahusiano na waume za watu kwa miaka mingi ili apate fedha nyingi sana bila kufanya kazi yoyote
-Anakuwa anapenda sana starehe ikiwemo ulevi kupindukia,kwenda night club,kutumia fedha nyingi sana kwenye sherehe na shughuli,anakuwa na marafiki wengi sana lakini hakuna hata mmoja mwenye dira ya maisha.
-Anaweza kuzaa kila mtoto na baba yake ,hata akiwa na miaka 36 bado anakuwa anavaa nguo fupi,anapenda night club,anachora tattoo,
-Anakuwa anavutiwa kimapenzi zaidi na wanaume ambao wanavaa mlegezo, kucheza kamari, kuvuta bangi,kunywa pombe sana, kubadilisha wanawake mara kwa mara kwa maana anapenda maisha ya anasa.
 
Mimi nilidekezwa/nadekezwa sana lakini sina hivyo ulivyotaja
Labda kidogo hapo kuvutiwa na wanaume wanaovuta bangi umepatia na milegezo
Asante kwa kuwa mkweli na muwazi halafu naona una enjoy sana vurugu, nimepitia uzi wa mikeka nikaona mambo zako 😂😂😂
 
Asante kwa kuwa mkweli na muwazi halafu naona una enjoy sana vurugu, nimepitia uzi wa mikeka nikaona mambo zako 😂😂😂
Amna bhana 😂
Mie na-enjoy peaceful life,kwani uzi wa kubet umekutana na vurugu gani tena ungenitag 🤣
 
Back
Top Bottom